Pablo Blanco
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 7,328
- 6,656
@="macho_mdiliko, Kwa hiyo hata Simba kumbe wana shida na single mothers
Sio kuwatumia £ huyu ndio alie wawezesha kimaisha, ndio maana wamemroga ili wazihozi mali zake.Jamani. Angejua wala asingerudi. Angejikalia zake UK tu. Inawezekana alikuwa anawatumia pound za kutosha kipindi yupo UK. Yote hayo wamesahau.
Hii kali. Ila hapa inaonekana Simba dume hufukuzwa ili wakaanzishe pride zao ? Au ndo ili wasijisevie majike ndani ya pride ?@="Victoire,
Victoire kawaida ambae hufukuzwa kwenye pride ni Simba dume na wanaomfukuza ni Simba dume mwenye mamlaka (dominant male) akishirikiana na wengine.
Lakini majike huwa hayafukuzwi...na sababu kubwa hapa sio chakula tu ila ni kulinda wanawake zao. Hii inatofautiana sana na fisi..kwa fisi wanawake ndio huwa na mamlaka..na fisi jike mwenye mamlaka ndio ana haki ya kujamiiana na madume wote wa fisi walio katika kundi!
Umenikumbusha Mané alimpa makavu live Salah sababu ya hiyo uloandika hapo.Baadhi ya wachezaji mpira wanalazimisha afunge goli yeye hata kama mwenzake yupo sehemu nzuri zaidi ya kugunga goli.Na hivyo ndivyo wanaadamu tulivyo,tunapenda na kujali sifa na manufaa yetu kwanza na sio ya wengine.
Marafiki zetu ni wale ambao watatusaidia kutunyanyua na kutufanya tuwe mabwana wakubwa,nadra bosi kumchukia mtumishi dhalili mtiifu asohoji haki zake hata kama zimekanyagwa.
[emoji23][emoji23] endelea kumkomesha mpaka aelewe kuwa ww sio saiz yake, ashike adabu ni chuki na wivu usiokuwa na sababu ya msingi.Umeongea logic sana kuna jamaa dizain anataka kuleta mashindano alafu mi sina time kila nnachofanya anaiga then anaangukia pua. Basi chuki ndio inazidi mi huwa nawaambia wapambe wake mwambieni jamaa yenu mi sina mashindano manake am not that ambitious vitu vyangu nafanya kwa plan na kila move iko calculated yeye anaingiaga kichwa kichwa.
Mimi huwa nahusisha binadamu alivyo na mikakati ya Mungu katika hii dunia. Duniani tunapitishwa ili kujaribiwa Imani zetu. Ukiweza kuishi na mwanadamu jinsi Mungu anavyotaka kiimani unakuwa umeimarika sana,hata shetani atakuwa anakuogopa hivyo mengine yatakuwa mepesi sana kwako. Hata Roman Catholic kuna kitu inaitwa AMRI KUU YA MAPENDO,ambayo ni msingi mkuu wa Maisha ya mwanadamu. Hii ni Imani niliyonayo mimi mkuu.Mi huwa najiuliza hivi hawa wenye roho mbaya hizi stori za moto wa milele hawazisikii au mtu anaamua kujilipua duniani alafu huko mbinguni potelea mbali akaishi kwa shida milele manake kuna watu wa katili sijapata ona. Mtu utakuta hamuingiliani kwa lolote ila anakuchukia tu
Nature ni complex sana. Atleast kwa wanyama vitu vinakuwa wazi wazi,mfano hao madume wanapofukuzwa kwenye pride ni idea nzuri ili wakafight kivyao.@="Victoire, post:
Wale Simba dume waliozaliwa ndani ya pride wakishakuwa vijana ndio hufukuzwa ili wakaanzishe familia zao, lakini pia ni kupunguza au kuondoa ushindani na Simba dume mmiliki (dominant males).
Sasa hawa wanapoondoka ndio huenda kuvamia pride zingine huko ndio hupambana na wale madume wanaomiliki pride zile...hii pia iko kwa Nyani (baboons)! hii kwenye tabia za wanyama inaitwa kwa kimombo "Female defense polygamy"
Kuna tabia nyingine hii huitwa "Resource defense polygamy" hapa dume hulinda malisho kuvutia majike..tabia hii naiona pia kwa binadamu, wanaume wengi hushindana kumiliki mali na hata kuwabania wengine ili tu kuwavutia wanawake..maana kwa asili (hii pia ni kwa wanyama) wanawake hupenda kushiriki (associate) na dume/mwanaume ambaye atawahakikishia "future" ya watoto wao..kwa kifupi ni kama Mungu alivyomuumba Adam na Eva na kuaambia "endeni mkazaane"..Basi hii kauli ndio hutafsiri maisha ya binadamu na wanyama pia..
kwa viumbe hawa hasa wanyama..the meaning of life is reproduction...na wanawake na wanaume (kwenye wanyama) wana uwekezani tofauti ili kufanikisha lengo la kuzaana...wanaume huwekeza kwenye nguvu (hii naiona pia kwa wanadamu) lakini wanawake huwekeza kwenye ubora..
.umeshawahi kujiuliza kwanini wanaume huzalisha sperm nyingi na ndogo kwa size na kila siku, wakati wanawake huzalisha yai moja au mawili kubwa kila mwezi na kwa umri maalumu tu (miaka 45 kwa binadamu)...kwa sababu hii wanawake huwa na uchaguzi wa nani kushirikiana nae....na hii inapelekea ushindani mkubwa sana kwa wanaume.
Hivi wanyama mfano Simba na wao hubaniana kama binadamu tulivyo?
Wanadamu wa ajabu sana. Wale mliosomea tabia za wanyama wengine ukiacha binadamu,na wao hubaniana ? Kama hapana kwa nini binadamu hawa Homo sapiens hubaniana sana?
Note: Namaanisha kubaniana katika maisha. Kuwa na roho ya korosho, yaani unafanya juu chini ili mwenzako asifanikishe jambo lake.