Mliosoma Zoology naomba mtoe maoni yenu

Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
24,139
56,590
Hivi wanyama mfano Simba na wao hubaniana kama binadamu tulivyo?

Wanadamu wa ajabu sana. Wale mliosomea tabia za wanyama wengine ukiacha binadamu,na wao hubaniana ? Kama hapana kwa nini binadamu hawa Homo sapiens hubaniana sana?

Note: Namaanisha kubaniana katika maisha. Kuwa na roho ya korosho, yaani unafanya juu chini ili mwenzako asifanikishe jambo lake.
 
Hakuna ufalme wenye mambo mabaya kama ufalme wa simba. Hivi unajua kuwa simba dume akikuta simba jike mwenye watoto anawaua wote ili yeye aweze kuzaa na yule jike na uzao wake uendelee?

Hivi unajua simba wanaishi katika makundi yanayojuana kwenye maeneo yao na akionekana simba mwingine anauawa kwani anaonekana ni tishio kwa upatikanaji wa chakula?

Hivi unajua simba anaweza kuwinda na akaja simba mwingine mwenye nguvu akamnyanganya na hakuna mahali popote pa kwenda kushtaki?

Hivi unajua simba wanashirikiana kuua lakini mara wanapoanza kula kuna utaratibu unaotakiwa kufuatwa na madume ndiyo yanakuwa ya kwanza kula zile sehemu nzuri nzuri? Yako mengi hujasikia ule msemo wa unyama unyama?
 
Akili yangu imewaza mbali hebu sana ongeza nyama ili wachangiaji tujue huo mbaniano ni wa kwenye nini, au ni kwenye yale mambo yetu ya wapogoro ?
 
macho_mdiliko
Duh, I never knew that aisee. Huwa nawaona wanaishi kwenye pride zao. Sikujua kuwa kila pride inaweza kugundua nani hahusiki kwenye pride yao.
 
Akili yangu imewaza mbali hebu sana ongeza nyama ili wachangiaji tujue huo mbaniano ni wa kwenye nini, au ni kwenye yale mambo yetu ya wapogoro ?
Mambo ya wapogoro ndo yapi ?
 
Hivi wanyama mfano Simba na wao hubaniana kama binadamu tulivyo ? Wanadamu wa ajabu sana. Wale mliosomea tabia za wanyama wengine ukiacha binadamu,na wao hubaniana ? Kama hapana kwa nini binadamu hawa Homo sapiens hubaniana sana ?
Note: Namaanisha kubaniana katika maisha. Kuwa na roho ya korosho,unafanya juu chini ili mwenzako asifanikishe jambo lake.
Shemeji ng'wangaluka, wamishaga kinehe...
 
Victoire,

Hayo mambo yapo ni hatari yaani ukishakuwa na vyeo kitu muhimu ni kuwa karibu na Mungu tu.
Maana kila mtu anapenda hizo nafasi wewe unadhani watu wote wanapenda ulivyokuwa? Duniani wengi wanapenda sana tufanane na tuwekatika hali moja lakini hiko kitu hakiwezekani.
 
Na mbaya zaidi huna sehemu ya kulalamika sembuse kushtaki.

Acha kabisa mkuu. Nilishamkuta mmoja yuko peke yake mpweke balaa Mpaka nikamuonea huruma. Nikajua tu huyu kashachezea kichapo cha haja.

Nilitamani nimfuat nimliwaze ila nikaogopa maana hasira zote ningeshushiwa mimi. Yaani huko maporini hakuna demokrasia kabisa ni undava undava tu.

Mwenye kisu kikali ndio anakula nyama. 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Sibonike,

Simba jike ndo huwinda ila kula anaanza simba dume. Hii ni kweli ? Ila kwa mfano simba wa pride nyingine akikamata nyati, wa pride nyingine wanaweza kuja kula pia?
 
Hayo mambo yapo ni hatari yaan ukishakuwa na vyeo kitu muhimu ni kuwa karibu na Mungu tu. Maana kilamtu anapenda hizo nafasi ww unazani watu wote wanapenda ulivyokuwa? Duniani wengi wanapenda sana tufanane na tuwekatika hali moja lakini hiko kituhakiwezekani.
Binadamu ni hatari.Kuna mwingine mkiwa wote mnafurahi kumbe nyuma anatamani hata ufe. Mimi nimefikia hatua kwa mfano tupo tumeenda lunch,nikisimama kwenda maliwaton let say nimeacha maji. Nikirudi siyanywi tena. Full kuwindana.
 
Kila kiumbe kina wivu wa ajabu - hasa kwa majike. Wewe angalia jogoo tu. Hataki kuona jogoo mwenzie anakatiza - itakuwa vita.

Kama una king'amuzi chenye channel za National Geographic- (Nat -Geo wild), ukiangalia utafurahi sana. Wanaonyesha tabia za wanyamapori wote. Wana wivu kuliko binadamu.

Wivu ni katika kupata "mademu" na katika kupata mlo. Vivyo hivyo ndivyo binadamu alivyo- hataki upate riziki. Na kwenye wivu kuhusu mwanamke ndio hivyo pia. Halafu wanawake bwana !!! Anakaa tu kimyaa.... wakati wanaume wanampigania.

Anaposhinda mmoja "demu" anaondoka naye. Kwa hiyo isimshangae demu wako anapokuacha akamfuata mtu mwingine mwenye "mpunga" kukuzidi. Ni asili ya wanawake - wa binadamu na wanyama.
 
Victoire,

Ila kwa mfano Simba wa pride nyingine akikamata nyati. Wa pride nyingine wanaweza kuja kula pia ?

Hamna kitu kama hiyo....ukisogea utapigwa mpaka ukachakae
 
Back
Top Bottom