Mliooa mlipata wapi wake zenu?

nyie ndo walee mnaotafuta wanawake wenye sijui wezere kubwa,ooo awe na sura nzuri,pua ndefu,mguu wa bia,macho ya kulegea,mrefu,awe na pozi.......badala ya kutafuta wenye sifa za kumcha mungu,,ndo mana matokeo yake mnaishia kupata micharuko
 
Hongereni wana jf kwenye thread hii mmenishangaza maana wengi wenu mmeongea point....haleluuuuuuyaaaaa
 

asante sana.. na nimeipenda
 
Mimi nilimpatia kwenye computer kozi alikuwa mwanafunzi wangu, kwanza nilimpenda kwa muonekano wake, tabia yake na nilipogundua kabila na dini yake vitaendana na matakwa yangu na kuwafahamu ndugu zake na tabia zao bila hata yeye kufahamu kwamba ninafanya uchunguzi niliamua kujaribu kuanzisha uhusiano, na kweli nilipomuomba kutoka nae hakukataa. Katika maongezi yetu swali la kwanza aliloniuliza ni kama mimi ni mume wa mtu au la, nilipomjibu kwamba mi sijaoa nilimuona ametabasamu na kuwa na amani sana. Tulianza urafiki wetu bila kujificha kabisa na ndugu zetu walijua toka miezi miwili ya mwanzo. Kusema ukweli kabla ya hapo nilikuwa kicheche nakwenda disko na marafiki zangu mpaka saa nane za usiku na huko kila mtu anachukua changudoa, tulikuwa na tabia ya kuchukua machangu tu, tulikuwa hatutaki kabisa kuwa na GF tuliona ni usumbufu usiokuwa na maana, unamchukua changu kesho hamjuani tena. Ila nilipompata mke wangu mpaka marafiki ilibidi nitengane nao kabisa kwenye mambo ya starehe, mpaka ilifikia wakawa wanasema nimelishwa limbwata. Ndugu yangu kitu cha muhimu ni kufanya uchunguzi na kujua tabia, elimu, dini, mila (kabila) kama vitaendana na matakwa yako na umuombe Mungu akusaidie umpate Mke mwema. Usiweke mbele tamaa za mwili na kufanya mapenzi ovyo, usimwambie kwamba unataka kumuoa kabla ya kufanya maamuzi. Tabia yako inaweza kukufanya kazi ya kumpata mke ikawa ngumu au rahisi sana jichunguze.
 

nikishafikiria shubiri ya ndoa ndo nakatika hamu ya ndoa kabisa....
mi sinaga tabia mbaya..
 
micharuko kila sehemu, ata hakuna pa kutokea!! sijui mi ndo nna gundu.. au ndo hali ilivyo ila lile neno ambalo lipo kwenye kiapo na linasisitizwa sana 'uvumilivu' linachukua nafasi yake!!
aise wake walishaisha

Wapo wengi sana tena wa kumwaga.....sema tu wewe ndo umeishiwa ujanja...Omba tu wataalamu wakusaidi ku-recharge!!

Uko tayari nikugawie mmoja wa wale nilionao??

Nataka kudispose mmoja ili nitafute mupya!!

Babu DC!!
 
Kwanza jiulize ulishajitambua ni mwanamke wa aina gani unamtaka

ndio, ni common awe mwelewa, mchapakazi, awe active si passive kila kitu niamue mimi na UAMINIFU
 
Leo hii ukiniuliza nilimpataje mama Ngina hata sikumbuki...................... haya mambo huwa yanatokea Automatikale.

ngoja nisubiri zamu yangu nami ata kama inachelewa, teh teh teh
 
Pole sana, wanawake kwa kiasi kikubwa wanachagua nani waolewe nao. Bado hujachaguliwa. Pili, ndoa ni zao la mahusiano halinunuliwa sokoni. Ukitafuta kama bidhaa sio rahisi kupata. Jipende utapedwa tu. Kila la kheri
 
micharuko kila sehemu, ata hakuna pa kutokea!! sijui mi ndo nna gundu.. au ndo hali ilivyo ila lile neno ambalo lipo kwenye kiapo na linasisitizwa sana 'uvumilivu' linachukua nafasi yake!!
aise wake walishaisha

fumba macho na masikio ziba

 
Kama una kwama waambie wazazi waku-postie. Ukizingatia ndoa za zamani za kupangiwa zilidumu zaidi

zamani wake walikua wengi ndo maana, siku iz wameisha!! wazazi ndo kwanza wanakwambia usituletee wa suruali za kubana, wao hata hawatii mguu kukutafutia wa sketi ya marinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…