Mlionunua ardhi mkoa wa Pwani na kisha mkaitelekeza tegemeeni haya...

mzee wa ndoto

Member
Jul 10, 2020
57
125
Salam kwenu wote WanaJF,

Kama ulibahatika kupata kipande cha ardhi kwa maeneo ya mkoa Pwani hasa wilaya Bagamoyo na Chalinze na huifanyii kazi.

Tegemea kukutana na changamoto hizi kwenda kwenye ofisi za Kiselikali kuomba mtu fulani ama kampuni fulani watoke kwenye eneo lako ili uweze kulifanyia kazi.

Sasa ikisha fika hali hiyo kuna mawili hapo mwenye kisu kikali ndio hula nyama nasema hayo kwa Sababu Hali imekuwa ngumu kwa waliouza aridhi hapo awali pesa zimiisha na washazoea kushika mabunda.

Hivyo kwa sasa wamekuwa hawana woga imefikia hatua baadhi ya watu kuyauza mashamba yao kwa mara nyingine kisha kulichukua jina la aliyeuziwa awali kulipeleka kwa sangoma kupigwa kipapayo.

Wateja wao wakubwa jamii ya kifugaji ambao idadi yao inawazidi wakazi. Malipo yanafanyika popote haina haja ya ofisi kikubwa anaeuza eneo ajue mipaka tu.

Hivyo ndugu yangu popote ulipo kama unakipande chako cha aridhi maeneo hayo niliyotaja fika na ifanyie kazi sehemu yako kuepusha usumbufu usiokuwa wa lazima.

Nawasilisha

#chuma kigonge kingari moto
 
PROF NDUMILAKUWILI

JF-Expert Member
Mar 25, 2016
9,376
2,000
Sehemu hizo zinahitaji uangalifu kununua eneo kuna jamaa humu alisema wenyeji wanapokupeleka kuona eneo watafanya jitihada wapate nyayo zako utapokanyaga mchanga wanachota kifuatacho ukishalipia wewe unasahau kurudi hapo kabisa kitauzwa kwa mwingine mchezo unaendelea
 
Omulasil

JF-Expert Member
May 5, 2015
3,569

Natafuta eneo Kibaha iwe hata mita 100 toka Moro to Dar road.
Kuhusu mchanga wa nyayo nitakuja nazo kabisa hata kama ni nywele za kwapa na kwa Wanazengo waje na kiwembe nawapa tu.
Mi nataka eneo liwe heka 2 hv
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
9,477
2,000
Wilaya za Kisarawe, Bagamoyo na Kibaha hii ndio michezo yao. Kuna ndugu yangu kalizwa milioni nane na ushei wiki mbiki zilizopita maeneo ya Fukayose Bagamoyo. Mauziano yalifanyika ndani ya ofisi ya Serikali ya Mtaa na akalipa na asilimia fulani ya hela kwa ajili ya Ofisi. Lakini baada ya kutaka kuanza kujenga mabanda wakatokea watu wengine watatu tofauti wakidai nao wameuzia eneo hilohilo.

Kurudi serikali ya Mtaa wanaambiwa eti wale waliokuwepo kwenye ofisi wakati wa mauziano hawatambuliki kama viongozi na hawajukikani kabisaa!!!!. Iliyobakia hapo ni mizozo tu na habari iliyopo ni kua eneo husika limeshauzwa zaidi ya mara mia!!!

Kuna mtandao mkubwa sana wa matapeli wa ardhi na ngao yao kubwa ni ushirikina. Ni kweli watu baada ya kununua hawakanyagi tena kwenye maeneo waliyonunua/waliyopigwa
 
uberimae fidei

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
1,712
2,000
Natafuta eneo Kibaha iwe hata mita 100 toka Moro to Dar road.
Kuhusu mchanga wa nyayo nitakuja nazo kabisa hata kama ni nywele za kwapa na kwa Wanazengo waje na kiwembe nawapa tu.
Mi nataka eneo liwe heka 2 hv
Umepata,karibu pm
 
pmwasyoke

JF-Expert Member
May 27, 2010
3,949
2,000
Nisisitize alichosema mkuu Tabutupu: Unaponunua ardhi ni vema ukawa na fedha ya kuanzisha uendelezaji kabisa. Leo unalipia kesho unaanza.
 
Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
684
1,000
Epukeni matatizo.Tunauza viwanja vilopimwa nyuma ya stendi kuu ya Kibaha, eneo la Pangani: piga 0713039875 ,eneo limezungukwa na makazi na viwanda
 
Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
684
1,000
Natafuta eneo Kibaha iwe hata mita 100 toka Moro to Dar road.
Kuhusu mchanga wa nyayo nitakuja nazo kabisa hata kama ni nywele za kwapa na kwa Wanazengo waje na kiwembe nawapa tu.
Mi nataka eneo liwe heka 2 hv
Karibu kwa viwanja vilopimwa, Kibaha mjini
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
9,477
2,000
Epukeni matatizo.Tunauza viwanja vilopimwa nyuma ya stendi kuu ya Kibaha, eneo la Pangani: piga 0713039875 ,eneo limezungukwa na makazi na viwanda
Tatizo viwanja vyenu mnavyopima vinakua vidogo sana tena ghali maana bei zenu ni per m². Sijui kwanini maeneo kama Kibaha mnapima kiwanja cha 400m² au 500m² pamoja na mapori yoote hayo.!!!!!

Pimeni maviwanja makubwa hadi 4000sqm² watu wajenge nyumba zenye nafasi. Ndio maana watu wanakimbilia kununua mashamba ili waweke nyumba na mabanda ya kufanya mambo mawili matatu na matokeo yake wananchi wanaishia kupigwa na matapeli
 
Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,357
2,000
Uzoefu unaonyesha wengi walio nunua hasa mashamba hawajawahi faidika nayo... hata kama ni miaka 5 lakini uwe na project ya kueleweka.. achana na wanao sema ardhi haiozi..
Je kama nina mpango wa miaka 5 ijayo nisijiandae? Ikiwa kipato hakitoshelezi kununua na kuanzisha mradi kwa wakati mmoja?
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,819
2,000
Ndio maana ilitengenezwa bunduki, Serikali iachie kwanza kesi kama hizi tumalizane wenyewe halafu baada ya hapo kila mtu atamuheshimu na kumuogopa mwenzake..

Unachukua hela ya mtu hujui ameipataje, halafu hakuna cha muhimu unachokwenda kufanyia zaidi ya kuhonga malaya na kufanya starehe hovyo..
Ilitakiwa kufanyika operation maalum kwa wajinga kama hawa na kuwaua na jamii ijue tu unauwawa ukifanya ujinga kama huo au kama vipi tandika uhujumu uchumi tu hakafu uone kama baada ya miaka mitano kutakuwa na hao wajinga..
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,819
2,000
Tatizo viwanja vyenu mnavyopima vinakua vidogo sana tena ghali maana bei zenu ni per m². Sijui kwanini maeneo kama Kibaha mnapima kiwanja cha 400m² au 500m² pamoja na mapori yoote hayo.!!!!!

Pimeni maviwanja makubwa hadi 4000sqm² watu wajenge nyumba zenye nafasi. Ndio maana watu wanakimbilia kununua mashamba ili waweke nyumba na mabanda ya kufanya mambo mawili matatu na matokeo yake wananchi wanaishia kupigwa na matapeli
kwa ukubwa wa ardhi tulionao hakuna haja ya kupima high density, inatakiwa viwanja vianza low mpaka medium density mwisho...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom