Barua ya wazi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi kuhusu mgogoro wa ardhi kata ya Maroroni wilayani Arumeru

Nov 24, 2014
45
18

BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAKAZI – ANGELINA MABULA KUHUSU MGOGORO WA ARDHI ARUMERU ARUSHA KATA YA MARORONI KIJIJI CHA KWA UGORO​

CC: Naibu waziri

Mh. Waziri Salam sana zikufikie popote pale ulipo, pole na hongera kwa majukumu mazito ya kujenga taifa letu la Tanzania hasa kupitia wizara nyeti unayosimamia. Dhumini la barua hii ya wazi ni kukufahamisha na kukualika uingilie kati mgogoro wa shamba la Kwa ugoro ambalo limedumu kwa muda mrefu sasa na baadhi ya viongozi na watangulizi wako walishuhulikia lakini hawakufanikiwa kulimaliza.

JOGRAFIA YA SHAMBA

Eneo la shamba lipo katika Kijiji cha Kwa Ugoro kata ya maroroni wilaya ya Arumeru Kilometa 15 Kutoka barabara kuu ya Arusha-Kilimanjaro kutokea Maji ya chai au mji mdogo wa Usariva.

HISTORIA YA TATIZO

Mh. Waziri Baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 Mwalimu Julius Nyerere Rais wa Kwanza wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuwaondoa wakoloni, wananchi waliingia kufyeka pori na sehemu ya shamba la mkonge la mwekezaji mzungu alieitwa Valeska kwaajili ya kufungua mashamba ya kulima. Mnamo mwaka 1977 – 1980 chama cha ushirika cha ARIDECO kupitia serikali ya mkoa kIliwaomba wananchi kupanua Zaidi mashamba kwa kufyeka ili chama cha ushirika kiwekeze, na wananchi wangelipwa Tsh 800 kwa kila heka itakayofekwa.

Hata hivyo mwaka 1983 wakati zoezi linaendelea ARIDECO Iligawanyika na kuunda vyama viwili vya ushirika yaani RIVACU na ACU. RIVACU ikawa katika Mkoa wa Manyara (MBULU) na ACU ikabaki katika mkoa wa Arusha. Mwaka 1984 ACU iliendelea kuhamasisha wananchi kufyeka na kupanua shamba kwa malipo ya 800 kwa heka moja. Hata hivyo ACU haikuwalipa wananchi kiasi hicho cha fedha kama walivyoahidi, badala yake mwaka 1990 wanakijiji walianza kukodishiwa mashamba hayo kwa Tsh 1000 kwa heka moja.

Gharama za kukodisha ziliendelea kupanda kila wakati hadi kufikia 50,000 kwa heka moja na hivyo kupelekea wananchi kushindwa kulipia na wakaanza kufatilia serikalini ili wamilikishwe na walime kwa uhuru. mara kadhaa viongozi wa Kijiji Walisafiri kwenda Dodoma ili kuonana na viongozi wenye dhamana ya ardhi kwaajili ya mchakato wa umilikishaji. Mwaka 2011 Aliekuwa naibu Waziri wa ardhi Godlack Ole Medeye alitoa maelekezo kwamba wananchi wa Kijiji cha Kwa Ugoro wamilikishwe shamba hilo na zoezi hilo lisimamiwe na Kamishna wa ardhi kanda ya Kaskazini washirikiane na Mkuu wa Wilaya. kwaanzia wakati huo ACU hawakuendelea kuwakodishia wananchi mashamba hayo yenye ukubwa zaidi ya Heka 4000.

Wakati mchakato wa ugawaji linakaribia kuanza, aliekuwa diwani wa kata ya Maroroni nae akaandika barua kwa Waziri kuomba heka 500 kwaajili ya Kijiji cha Jirani cha Maroroni anakotoka yeye jambo ambalo lilizua mtafaruku na mgogoro mkubwa na baadhi ya watu kuumizwa. Baadae Ikabidi zoezi la umilikishaji lisimame kwasababu watu wa maroroni nao walihitaji, na Kijiji cha Jirani cha Valeska kilihitaji pia sehemu ya shamba hilo lakini Valeska walistahili kwasababu nao wana ardhi ambayo hapo awali ilikuwa chini ya mwekezaji.

Wakati huo huo aliekuwa mkuu wa wilaya Alexander Mnyiti aliingilia kati na kuwazuia wanakijiji wa Maroroni kuingilia mchakato huo wa ugawaji kwasababu haikuwa haki yao wala hawakuwa na sehemu katika shamba hilo, pia Mbuge Joshua Nasari aliwasihi wananchi waache fujo na waendelee na majukumu yao kila Kijiji na sehemu yake, Aliomba msaada kutoka kwa Waziri wa Ardhi Simba Chawene wakati huo ambao kwa Pamoja walifika hadi shambani kushuhulikia swala hilo lakini hawakufanikiwa kukamilisha umilikishaji Zaidi ya kuwasihi wananchi kwamba kila Kijiji Kibaki katika eneo lake na swala lingeshuhulikiwa na kuisha.

Mwaka jana mwishoni na January mwaka huu 2022 kumetokea vuta nikuvute kati ya viongozi wa Kijiji wa kwaugoro na Mkuu wa wilaya ambae alitaka shamba hilo ligawanywe kwa usawa kwa vijiji vyote vitatu kila Kijiji hekta mia tano (500) na sehemu ya shamba inayobaki takriban heka elfu mbili mia tano (2500) itumike kama mradi wa halmashauri kwa kuuza, kufungua dampo, kufidia na miradi mingine. Wananchi walipojaribu kupinga swala hilo, viongozi wa Kijiji waliswekwa rumande kwa muda wa wiki mbili baadae waliachiliwa lakini kesi ipo mahakamani.

Mh. Waziri hadi naandika barua hii zoezi la kupima shamba linaendelea likisimamiwa na ofisi ya mkuu wa wilaya na Polisi, na wananchi wamezuiwa kufanya chochote, hata baadhi ya mashamba ambayo yana chakula hakuna mtu anaeruhusiwa kwenda bila kibali maalum kinachotolewa na Afisa mtendaji. Jambo la kusikitisha ni kwamba hao wananchi wanaozuiwa ndio waliofyeka hayo mashamba miaka hiyo, wamelima miaka yote tangu uhuru wa Tanganyika, Leo hii wananyanganywa mashamba yao, serikali inachukua sehemu kubwa, kidogo kinachobaki kinagawanywa kwa vijiji vya mbali ambavyo wanachi wake wana mashamba katika vijiji vyao. Hatari inayoweza kutokea ni mgogoro usioisha na hata mauwaji yanaweza kutokea baina ya vijiji kwasababu haki haionekani ikitendeka. Katika usimamiaji wa zoezi hili, inaonekana Mh Mkuu wa Wilaya wenda amedanganywa na wasaidizi wake au baraza la madiwani ambao baadhi ndio wanaohitaji shamba hilo kwaajili ya vijiji wanavyoviongoza.

MAPENDEKEZO
  • Mh. Waziri Tunaomba ufike Arumeru kukutana na viongozi wa wilaya, wananchi Pamoja viongozi wa halmashauri ya Kijiji na wadau wengine kutoka shirika la ACU, Kamishana wa ardhi, kupitia nyaraka mbalimbali kuona jinsi viongozi waliotangulia walivyojaribu kutatua swala hili.
  • Shamba lina Zaidi ya hekari 4,000. Kwasababu wananchi wa Kwaugoro wamelitumia kwa muda mrefu, ndio waliofyeka zamani na ndio chanzo kikuu cha vipato vyao, na wameshafatilia kwa muda mrefu serikalini ili wamilikishwe, tunaomba wizara iamue kwa haki angalau kwa kuwapatia heka 2500 kama walivyowahi kuwasilisha ombi hilo wizarani na kukubaliwa. Vijiji vingine hasa cha maroroni wanataka kunufaika kwa faida ya bure kwasababu tu viongozi wa kata na diwani wanatoka katika Kijiji hicho lakini kwakweli wasingestahili chochote kwasababu ni Kijiji cha mbali na wana mashamba yao.
  • Kila Kijiji Kibaki na mashamba ambayo wananchi wake wamekuwa wakiyalima tangu zamani, historia ya mashamba hayo izingatiwe ili kuondoa mgogoro ambao unaweza kuleta maafa hapo baadae. Kama wananchi wa Kijiji A hawajawahi kuwa na mashamba katika Kijiji B iweje leo wapewe? Maroroni wabaki katika mipaka ya eneo lao, Kwa Ugoro wabaki katika mipaka ya eneo lao, vivyo hivyo Valeska nao wabaki katika mipaka ya eneo lao. Historia izingatiwe katika utatuzi wa mgogoro.
  • Mh Waziri Chunguza pia kama kuna watu wametanguliza maslahi binafsi ambao wanahitaji mashamba hayo ili wananchi watakapo nyang'anywa wanunue kwa bei ndogo na wamilikishwe kinyemela. Tunaomba serikali ifatilie vizuri ili hata kama kuna mwekezaji anaehitaji eneo ambalo serikali itabaki nalo baada ya wananchi kupewa haki yao basi sheria za uwekezaji zifatwe barabara.
  • Baada ya serikali kutoa shamba hilo kwa wananchi, tunaomba wasimamie pia Ugawaji wa shamba ili kila mwananchi anaehusika apate hata kama Ada ndogo inaweza kupangwa ili kugharamia zoezi hilo ili wananchi wote wanufaike.
Mwisho, tunaamini mara upatapo barua hii utaanza kufatilia swala hili haraka kwa kusimamisha ugawaji wa shamba kwa vijiji viwili tu (Kwa Ugoro na Valeska) na baadae kuja kuzungumza na wanachi na ikikupendeza zungukia vijiji vyote, zungumza na watu wote wanaohusika maana mwisho wa siku utafahamu ukweli. Hatuna mashaka kwamba utafanyia kazi swala hili maana umeonekana sehemu mbalimbali ukitatua changamoto za ardhi na Mh Rais Samia amekuamini hivyo nasi tunaamini hili litashuhulikiwa kwa wakati.

Wako katika ujenzi wa Taifa
Wananchi wa Kijiji cha Kwaugoro
 
Bora angekuwa Lukuvi huyu ni tatizo pamoja na msaidizi wake mpigaji.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom