Wizara ya Ardhi na Makazi pamoja na Serikali ya mkoa wa Pwani na wilaya ya Kisarawe chukueni hatua haraka

Ndama Jeuri

JF-Expert Member
Jul 9, 2015
1,503
1,472
Kwenu Mheshimiwa Waziri wa Ardhi na Makazi mh! Angelina Mabula, mkuu wa mkoa wa Pwani mh Abubakar Kunenge, mh mkuu wa wilaya ya Kisarawe Nikki wa Pili.

Nachukua fursa hii kuwafikishia vilio vya wananchi wa kijiji cha Kifuru kilichopo wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani kilometa chache tu kutoka Kisarawe Mjini.

Vilio hivi vinahusu mgogoro wa ardhi unaofukuta kwa miaka kadhaa sasa, na mgogoro huu wa ardhi umegawanyika katika sehemu mbili, ya kwanza ni baina ya kijiji na kijiji, yani kijiji cha Kifuru na Kola, na pili ni mgogoro wa wanakijiji wenyewe wa kijiji cha Kifuru.

Na viongozi wengi waliofika kujaribu kutatua huo mgogoro hususani wa wilaya walitoa matamko na maelekezo kwa serikali ya kijiji bila kusimamia utekelezaji wake mpaka mwisho,ikawa ni sawa na hakuna walichokifanya.

Sasa hali imekuwa mbaya zaidi kwa wanyonge wa kijiji cha kifuru kwani matajiri wamevamia hiko kijiji,na kuweza kuwanunua viongozi wa kijiji na kushinikiza kuuziwa mashamba na wanakijiji kwa bei ya kutupwa,huku wakifoji mihuri kutoka vijiji vingine vya jirani kama kisanga na kola.kwani mihuri ya kijiji cha kifuru,inavyosemekana halmshauri ya wilaya ya kisarawe iliichukua ili kusifanyike mauziano ya ardhi ya aina yoyote ile.

Lakini licha ya hiyo mihuri kuchukuliwa imekuwa ni kazi bure kwa maana bado watu wenye pesa wameweza kutumia pesa zao kununua ardhi kwa nguvu.

Nina sema kwa nguvu kwa sababu nilizungumza na mzee mmoja aliyefahamika kwa jina moja tu la"Ndolite",yeye ni muhanga wa kulazimishwa kuuza ardhi kwa nguvu,kwani serikali ya kijiji ilimpa pori asafishe ili liweze kuwa shamba lake,baada ya kusafisha na kupanda mazao kwa misimu tisa ya mavuno,akaibuka tajiri mmoja aliyefahamika kwa jina moja la "BOSS KIGULU" kwa kushirikiana na viongozi wa serikali ya kijiji na kumshawishi amuuzie lile shamba yule tajiri,yule mzee aligoma.

Baada ya kugoma yule tajiri alimuahidi kuwa atamuonesha cha mtema kuni,kwani atafukia bangi kwenye lile shamba,kisha ataenda kuwatonya polisi kuwa yule mzee anauza bangi ili wakija wazikute zile bangi na yule mzee akafungwe,akishafungwa yule tajiri(BOSS KIGULU) atamiliki shamba kirahisi,kwani yule mzee hana familia yeyote ile.

Yule tajiri alibadili mbinu ya kupata lile shamba kwani alimpanga mwanakijiji mmoja aliyefahamika kwa jina la( Bene) na kujifanya kuwa ni mmiliki wa lile shamba,akampa kiasi cha fedha na kisha yule tajiri kudai kuwa lile shamba ni lake kauziwa na Bene.

Hivyo huyo mzee ni mmoja kati ya wanakijiji wengi wa kifuru wanaotapeliwa kinguvu na matajiri,pale tu wanapogoma kuudha ardhi zao.

Sasa hivi hali imekuwa mbaya zaidi kwani kuna viashiria vya uvunjifu wa amani,kwa watu kutishiana kutoana uhai! Serikali kupitia wizara husika fanyeni jambo haraka kurudisha mshikamano msisubiri watu watoane roho ndo muanze kutoa matamko makali!
 
Back
Top Bottom