Mliompigia debe Magufuli nawauliza swali...

Mliompigia debe Magufuli nawauliza swali...

Kwanza mlitakiwa mfahamu kwa nini mlizungusha mikono na kudeki sana barabara..bahati mbaya hamkujua mlikua mnachochea moto wa gesi..mlitakiwa mjue kuwa kilichoifikisha nchi pale hadi mkataka mabadiliko ni urafiki, mitandao ya uchaguzi na wafanyabiashara..huyo wenu alikuwa navyo vyote hivyo..sisi tuliojiongeza na tuliofahamu rise and fall ya jk tukaona anayetufaa ni yule asiye na mitandao ya uchaguzi, wafanyabiashara na marafiki..na lengo lilitimia na nyote mashahidi..kwa Tanzania tulipofikia tulihitaji sana Kiongozi wa karba ya magufuli kuliko kufanya mahaba na mihemko..hata hivyo naona jpm Bado anatudekeza sana..kama kashindwa na yeye apishe wengine nchi isonge
Mbona mlipata kura chache sana kuliko wakati wowote wa historia za uchaguzi?
 
Swali zuri ...hivi kati ya EL na JPM yupi Chadema ilitusaidia kumjua vizuri zaidi? In short Chadema ilifanikiwa sana kumbomoa EL na mwisho kushindwa hadi kupitia chama chao. Labda nikuulize ....hivi unamtemaje Dr Slaa miezi michache kabla ya uchaguzi (ingawa wengine watasema alitoka mwenyewe bila kujua steps). Tumevurugwa na Chadema sana ....kama akili zako zipo sawa unahitaji PHD ya kumuelewa EL ili kumpa kura badala ya JP ambaye humjui kivileee ...
Ha ha watanzania bana kazi kweli kweli mtoa uzi hajamtaja Lowassa ila wewe umekuja ukamtaja lala bana
 
Uchaguzi ukiitishwa leo kwa mazingira ya 2015 atachaguliwa tena tu...
 
Hakukua na competitor hivyo kuliko kupigia kura jiwe wenye akili zao waliamua kimpigia kura.

Nani ana uhakika Dr yupo nyuma ya haya yanayotokea? Tumeona yaliyotokea kwa machinga Mwanza. Kwa busara alizonazo Dr Magufuli bila shaka ataingilia kati suala la Max. JF ina mchango mkubwa kuchaguliwa kwa Dr Magufuli kuwa Rais na uzi huu ni ushahidi tosha kwamba kampeni ya kumchagua Magufuli ilipigwa humu.

Kama Max angekua si Mzalendo angeweza kuachia Mods wafunge threads zote zilizokua zinampigia debe Magufuli.
 
img-20161122-wa0031-jpg.437677
 
Sema ana kura yako,sio zetu.zetu na nani anamtaka?
Hata Leo hii JPM ana kura yangu . ...siasa haziendeshwi kwa hasira kwa ajili ya mtu mmoja tu ambaye ana uroho wa madaraka . .hivyo yuko tayari atumie pesa yake kuvuruga kile kizuri . ...HAPANA KABISA HAIENDI HIVYO KABISA
 
Magufuli ndio alikuwa na sifa pekee za kuwa raisi wetu.
 
Magufuli anisamehe kwa kum-underestimate sababu nilichoshwa na uongozi mbovu wa awamu ya nne ila 2020 kura yangu itarudi kwa magufuli asilimia 101.....hana mpinzani
 
Labda tujiulize ....hivi mliompigia kura EL ...mliipigia kura Chadema au EL? ....Kama mlipigia chadema ....chadema ni nini? Mbowe? Mliwahi kuhoji kauli za viongozi wenu kabla hamjafanya uchaguzi? K
ama mliichoka CCM ...CCM ni watu ...je mlichoka jina la CCM au watu waliowafikisha hapa? Mliokuwa mkiwapigia debe mnawatenganisha vipi na hili? Tuache siasa tujitambue na kusimamia haki kwa faida ya taifa la kesho.
Kusimamia haki zipi ambazo zinasiginwa kila siku? Au kwako haki ina tafsiri gani?
 
Haya sasa...naona tarakimu zinaanza kusomeka vizuri kwa wote.

Sasa naomba niwaulize swali nyote nyie mliomuunga mkono MTUKUFU Magufuli na CCM yake kwenye uchaguzi mkuu ulopita [2015].

Hivi ni kitu gani mlichokiona kwa huyo jamaa hadi mkaamua kumuunga mkono na kumpigia debe awe ndo amiri jeshi mkuu?

Mliamua hivyo kwa hasira za kusalitiwa na CHADEMA au mliamua hivyo kwa kuangalia sifa alizokuwa nazo?

Na kwani ilikuwa ni lazima mumuunge mkono yeye? Manake wagombea hawakuwa Lowassa na yeye tu.

Oh well....acha tu hizo tarakimu zisomeke sasa. Labda ndo tutatia akili huko mbeleni.

Huyo mtu ana mazuri yake machache mno na mabaya yake ni mengi zaidi.
Siku ukitia mguu huku wewe straight to Ruvu River
 
Back
Top Bottom