Mliompigia debe Magufuli nawauliza swali...

Hahhhaahahaaaaa.....umemjibu vizuri sana huyu ambaye hamjui JPM ni nani kiundani....chadema mtabaki na chadema yenu na Mbowe wenu,na Lowasaaa wenu na Lema wenu, sisi tuacheni na JPM wetu mpenda wanyonge....naipenda CCM hadi naumwaaaaaaaaaaaaaaa
Wanyonge wanakulaga hela za rambirambi za waathirika?
 
And I don't think I'll ever vote for CCM in my lifetime.

Miafrica tunachagua kwa kigezo cha mihemko. Si mtu wala sera.

Lowasa alishinda kwenye uchaguzi kwa 62% hutaki acha.

Tunaisoma namba wote bila kupepesa macho Miafrica ndivyo Tulivyo.
 
Uwanja wa kwako refa wa kwako na washabiki wa kwako ...... na tayari mpinzani wako ameshapewa kadi ya njano,ngum sana kushinda hyo mechi
 
Sawa kama mimi ni kichaa nakubali na kila Binadamu ana ukichaa kwa namna moja au nyingine, tusubiri 2020 tuone kama kuna atakayemzidi kwa kura Magufuli wetu!
Unajipendekeza ili uonekane mwema.?!
 
magufuli ana kura zote za familia yangu yenye members zaidi ya 30,toa takataka zingine.Huyu mtu ni kiboko amerudisha nidhamu,kuna watu nawajua wengine wamo humu jf walikuwa wanatumbua siyo mchezo,waulize sasa wanajambajamba tu.Ujanjaujanja na utapeli kwishnei,hongera JPM
 
Kwanza mlitakiwa mfahamu kwa nini mlizungusha mikono na kudeki sana barabara..bahati mbaya hamkujua mlikua mnachochea moto wa gesi..mlitakiwa mjue kuwa kilichoifikisha nchi pale hadi mkataka mabadiliko ni urafiki, mitandao ya uchaguzi na wafanyabiashara..huyo wenu alikuwa navyo vyote hivyo..sisi tuliojiongeza na tuliofahamu rise and fall ya jk tukaona anayetufaa ni yule asiye na mitandao ya uchaguzi, wafanyabiashara na marafiki..na lengo lilitimia na nyote mashahidi..kwa Tanzania tulipofikia tulihitaji sana Kiongozi wa karba ya magufuli kuliko kufanya mahaba na mihemko..hata hivyo naona jpm Bado anatudekeza sana..kama kashindwa na yeye apishe wengine nchi isonge
 
Namba tumeshazisoma bado za kirumi?ndio tuishi kama mashetani kabisa.
 
Tanzania hakuna haki tena. Kilichobaki ni udhalimu wa chama tawara. Natamani Rev Mtikila angekuwepo, inauma kuona haki za binadamu mtu ajiwekee mikononi.
 
JPM ameshushwa kuja kuiokoa tz,piga picha lile Lowassa angekuwa president,wahuni wote wangekuwa serikalini,wapigaji wote serikalini,kapuku kama mimi ni wa kukojolea tu
 
Swali zuri ...hivi kati ya EL na JPM yupi Chadema ilitusaidia kumjua vizuri zaidi? In short Chadema ilifanikiwa sana kumbomoa EL na mwisho kushindwa hadi kupitia chama chao. Labda nikuulize ....hivi unamtemaje Dr Slaa miezi michache kabla ya uchaguzi (ingawa wengine watasema alitoka mwenyewe bila kujua steps). Tumevurugwa na Chadema sana ....kama akili zako zipo sawa unahitaji PHD ya kumuelewa EL ili kumpa kura badala ya JP ambaye humjui kivileee ...

Mkuu mimi sio mwanachama wa cdm lakini ni shabiki wa kutupwa wa cdm, kama kuna kitu kilinisikitisha kwa cdm ni kumchuku EL siku za mwisho na kisha kumpa nafasi ya kugombea urais. Kama kuna kosa la mwaka cdm walifanya basi ni lile, ukijaribu kuangalia ujio wa Lowassa cdm ndio umekuwa anguko lake hivi leo. Kwa sasa hivi tumebaki sisi washabiki wabishi ndio wangalau tunapambana, cdm kama chama hakina ile amshaamsha kwani wamefundishwa siasa za kikondoo na huyo mamluki. Kibaya zaidi sasa hivi ccm wala hawatishwi na cdm kwani tunamtumia kapi lao kupambana nao. Leo hii mkuu wa ccm anafanya anavyotaka na hakuna wa kumhoji tumebaki tunapiga kelele huku mitandaoni lakini hatufurukuti, tumebakiza muda mchache hata huku mitandaoni tutapigwa stop. Cdm ndio kilikuwa cdm kinachoweza kuhoji serekali ikatekeleza, kumbuka mpaka mchakato wa katiba mpya ilikuwa ni nguvu ya cdm. Leo hii tunaambiwa eti katiba sio lazima nchi inanyooshwa!!! Huyo mamluki eti anasema tuache harakati tuwe wanasiasa wakati mwenyewe hathubutu hata kuitisha mkutano wa kupongeza waliompa kura. Huwa ninajiuliza kweli hivi tulikosa mgombea kabisa mpaka tukampa huyo jamaa? Leo hii kapewa nchi ambaye anaongooza nchi kama mali yake binafsi kisa hatuna ajenda ya kumuhoji chochote maana hata wananchi hawajui tunasimamia nini. Kuna huyo katibu mkuu kijana kuliko huyo Slaa japo naye Slaa aliondoka kwa kuzira, lakini huyo katibu mkuu ndio amekuwa mzee kimatendo na Slaa amekuwa ni kijana kuliko yeye. Mbowe hana ushawishi ule aliokuwa nao tena, sasa hivi kila kitu mpaka amuulize Lowassa!! Akina Lissu walifurukuta mwanzo lakini watanzania wakaitwa wanyonge wakakubali, sasa hivi kila mtu kabaki kuahidiwa maisha bora huko mbeleni kwani mifumo inawekwa sawa lakini hakuna kuhoji. Yaani sipati picha huku mkenge cdm walioingizwa wakati mwingine mpaka naona EL ni kama pandikizi la kuja kuia cdm.
 
Haya sasa...naona tarakimu zinaanza kusomeka vizuri kwa wote.

Sasa naomba niwaulize swali nyote nyie mliomuunga mkono MTUKUFU Magufuli na CCM yake kwenye uchaguzi mkuu ulopita [2015].

Hivi ni kitu gani mlichokiona kwa huyo jamaa hadi mkaamua kumuunga mkono na kumpigia debe awe ndo amiri jeshi mkuu?

Mliamua hivyo kwa hasira za kusalitiwa na CHADEMA au mliamua hivyo kwa kuangalia sifa alizokuwa nazo?

Na kwani ilikuwa ni lazima mumuunge mkono yeye? Manake wagombea hawakuwa Lowassa na yeye tu.

Oh well....acha tu hizo tarakimu zisomeke sasa. Labda ndo tutatia akili huko mbeleni.

Huyo mtu ana mazuri yake machache mno na mabaya yake ni mengi zaidi.
.
Hata familia yake inafahamu hilo.
Mabaya yake ni mengi mno mbali na mazuri yake!
 
Swali zuri ...hivi kati ya EL na JPM yupi Chadema ilitusaidia kumjua vizuri zaidi? In short Chadema ilifanikiwa sana kumbomoa EL na mwisho kushindwa hadi kupitia chama chao. Labda nikuulize ....hivi unamtemaje Dr Slaa miezi michache kabla ya uchaguzi (ingawa wengine watasema alitoka mwenyewe bila kujua steps). Tumevurugwa na Chadema sana ....kama akili zako zipo sawa unahitaji PHD ya kumuelewa EL ili kumpa kura badala ya JP ambaye humjui kivileee ...

Mkuu mimi sio mwanachama wa cdm lakini ni shabiki wa kutupwa wa cdm, kama kuna kitu kilinisikitisha kwa cdm ni kumchuku EL siku za mwisho na kisha kumpa nafasi ya kugombea urais. Kama kuna kosa la mwaka cdm walifanya basi ni lile, ukijaribu kuangalia ujio wa Lowassa cdm ndio umekuwa anguko lake hivi leo. Kwa sasa hivi tumebaki sisi washabiki wabishi ndio wangalau tunapambana, cdm kama chama hakina ile amshaamsha kwani wamefundishwa siasa za kikondoo na huyo mamluki. Kibaya zaidi sasa hivi ccm wala hawatishwi na cdm kwani tunamtumia kapi lao kupambana nao. Leo hii mkuu wa ccm anafanya anavyotaka na hakuna wa kumhoji tumebaki tunapiga kelele huku mitandaoni lakini hatufurukuti, tumebakiza muda mchache hata huku mitandaoni tutapigwa stop. Cdm ndio kilikuwa cdm kinachoweza kuhoji serekali ikatekeleza, kumbuka mpaka mchakato wa katiba mpya ilikuwa ni nguvu ya cdm. Leo hii tunaambiwa eti katiba sio lazima nchi inanyooshwa!!! Huyo mamluki eti anasema tuache harakati tuwe wanasiasa wakati mwenyewe hathubutu hata kuitisha mkutano wa kupongeza waliompa kura. Huwa ninajiuliza kweli hivi tulikosa mgombea kabisa mpaka tukampa huyo jamaa? Leo hii kapewa nchi ambaye anaongooza nchi kama mali yake binafsi kisa hatuna ajenda ya kumuhoji chochote maana hata wananchi hawajui tunasimamia nini. Kuna huyo katibu mkuu kijana kuliko huyo Slaa japo naye Slaa aliondoka kwa kuzira, lakini huyo katibu mkuu ndio amekuwa mzee kimatendo na Slaa amekuwa ni kijana kuliko yeye. Mbowe hana ushawishi ule aliokuwa nao tena, sasa hivi kila kitu mpaka amuulize Lowassa!! Akina Lissu walifurukuta mwanzo lakini watanzania wakaitwa wanyonge wakakubali, sasa hivi kila mtu kabaki kuahidiwa maisha bora huko mbeleni kwani mifumo inawekwa sawa lakini hakuna kuhoji. Yaani sipati picha huku mkenge cdm walioingizwa wakati mwingine mpaka naona EL ni kama pandikizi la kuja kuia cdm.
 
things fall apart

kila kitu kimesambaratika,mambo yako hovyohovyo
 
Back
Top Bottom