Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 27,916
- 35,397
Naunga mkono hojaHabari wana JF.
Kuna baadhi ya watumishi wa serikali, kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ngazi ya juu kabisa huwa wanajiona wao ni watu maalum sana.
Kama hujawahi kukutana na watu wa aina hiyo, basi nakuhakikishia iko siku utakutana nao. Wengi wao husahau ule usemi wa "cheo ni dhamana". Hao ndio wale ambao shida yako hata kama ilikuwa ni ya kutatuliwa kwa dakika moja (mfano kusaini document hakuhitaji muda mrefu), lakini utashangaa unaambiwa nenda utarudi kesho au mwezi ujao n.k.
Lengo la kuandika huu uzi ni kuwaasa watumishi wote wa serikalini kuanzia watendaji wa vijiji hadi kwa Rais, watambue kwamba wako pale kwa ajili ya kuwahudumia watu na siyo kuwanyanyasa au kuhudumia watu wa aina fulani kwa upendeleo. Na wanatakiwa wafanye hivyo huku wakijua kwamba wako wengi wenye uwezo kuliko wao, lakini hawakupata tu bahati ya kuwa pale walipo.
Naomba kuwasilisha.