Wadau amani kwenu...
Kuna jambo linanitatiza na kunisumbua sana kichwa. Nimedokezwa humu JF kuna watu al-maarufu kama "vipenyo" yaani watu kutoka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) ambao wana access ya kumfikia mzee baba.
Ninaomba wanisaidie kumuuliza nini faida na manufaa yaliyopatikana kufuatia maamuzi haya kama nchi.
(1). Nini faida ya kuzipiga "ban" vyombo vya habari vilivyokuwa vinakosoa Serikali na kuibua matendo ya ufisadi?
(2). Nini faida iliyopatikana kwa kukataza vyama kufanya siasa kwa miaka mitano iliyopita?
(3). Nini faida ya wazi iliyopatikana kwa kuwapiga, kuwatesa, kuwafunga wapinzani ambao nao ni Watanzania?
(4). Nini faida iliyopatikana kwa kuwatimua wale wanafunzi 8000 huko UDOM na kuitwa "vilaza"?
(5). Nini faida iliyopatikana/inayopatikana kwa kwenye kwa kuchoma nyavu za wavuvi ziwa Victoria tena kwa kupigwa wengine kuuliwa?
(6). Kuna faida gani iliyopatikana kwa kuhusisha JWTZ kuvamia na kupora fedha katika maduka ya kubadilisha fedha huko Arusha?
(7). Nini faida iliyopatikana kwa uamuzi wa kupora fedha za wafanyabiashara Benki kwa "task force" badala ya wataalamu wa kodi?
(9). Nini itakuwa faida ya kuwa na Bunge lisilokuwa na wapinzani kwa uamuzi uliofanywa na dola isiyo ya kikatiba?
(10). Nini faida ya kiuchumi tutakayopata kwa kujitenga na dunia katika vita dhidi ya Covid-19?
Ndugu zangu, tunaweza kumlaumu Rais Magufuli kumbe kuna faida nyingi tutapata kwa maamuzi haya. Hebu tujadiliane kwa hoja pengine uwezo wangu wa kuona Mambo ni mwembamba. Msalimieni.