Lihakanga
JF-Expert Member
- Dec 17, 2016
- 4,829
- 6,376
Asante mkuu, kidogo nmeanza kuelewa.ADC wa prezidaa nijuavyo huwa anakuwa mmoja sema anakuwa na backup incase ya emergency. Uteuzi wake mara nyingi anafanyiwa vetting na inteligencia ya jeshi na inteligencia ya usalama wa taifa kwa kuangalia ubobezi wake katika masuala ya usalama. Hawi mpambe kama mpambe tu wakubeba speech za prezidaa au kusogeza kiti mkubwa akae. Mtu huyu ni well trained katika maswala yote ya ulinzi na inteligencia.
Jukumu kubwa la ulinzi wa prezidaa huwa halibebwi na ADC bali kikosi maalumu cha wanausalama ambao kazi yao ni kumlinda rais wa nchi. Hiki ni kikosi kidogo chenye mafunzo ya hali ya juu na wako wengi hivyo wanakuwa wanafanyiwa rotation kutokana na nature na mazingira rais alipo. Wapo tunaowaona mbele kabisa karibu na rais hata wakati akitembea kwa miguu ama kwenye gari na wapo ambao huwa wanakaa muda wote wamejichanganya na raia. Hawa nao rais hausiki katika uteuzi wao bali mamlaka ya usalama wa taifa.
Kwa uelewa wangu niishie hapa kama kuna mengineyo baadae