Mlinzi wa Mfalme Oman Mbaroni

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,739
Mlizi wa mfalme wa Oman akamatwa kwa kusafirisha fuvu la taiga kwenda Oman.
hii siyo breaking news kwa wanajf wengi swali langu kama anaesafirisha fuvu anakamatwa vipi waliosafirisha twigs wakiwa Hai..
au kwa kuwa ilikuwa dili la serikali...
 
Serikali iliyopita ya JK ilikuwa ya wapiga dili tu, nani alijali udhibiti wa raslimali za taifa, zilimhusu nini? Kama twiga anaweza kusafirishwa kwenye ndege pasipo kujulikana ni vingapi vilipita kabla? Huyu aliyekamata fuvu leo kwa maana ya taasisi alishindwaje kukamata wanyama zaidi ya 100 akiwamo twiga waliotoroshewa Uarabuni? Intelijensia ya vyombo vyetu vya dola huishia kupiga ramli ya kuwepo uvunjifu wa amani wakati vyama vya upinzani vikitaka kufanya maandamano au mikutano. Lakini intelijensia ya kutambua utoroshwaji wa nyara za taifa, utoroshwaji wa makontena yasiyolipiwa kodi, hujuma za ufujaji wa fedha kwenye taasisi za umma, mikataba mibovu nk, hizo huwa hawaziono.
 
Mlizi wa mfalme wa Oman akamatwa kwa kusafirisha fuvu la taiga kwenda Oman.
hii siyo breaking news kwa wanajf wengi swali langu kama anaesafirisha fuvu anakamatwa vipi waliosafirisha twigs wakiwa Hai..
au kwa kuwa ilikuwa dili la serikali...

Badala ya kupongeza unalaumu kwa hiyo ulitaka wamwachie yaani vijana wa CHADEMA ni janga la kitaifa. ulitakiwa kutoa pongezi kwa sababu huko nyuma walikuwa hawakamatwi.
 
Badala ya kupongeza unalaumu kwa hiyo ulitaka wamwachie yaani vijana wa CHADEMA ni janga la kitaifa. ulitakiwa kutoa pongezi kwa sababu huko nyuma walikuwa hawakamatwi.

Unaonaje akikamatwa yule mpiga deal wenu mkuu akanyoosha maelezo kwa vitu alivyosafirisha na mkiwa mnamsifia kila kwa muda wote?
 
No, akamatwe, kama sheria hairuhusu, kwa nn atozwe faini tu, sheria lazima ichukue mkondo wake
 
Badala ya kupongeza unalaumu kwa hiyo ulitaka wamwachie yaani vijana wa CHADEMA ni janga la kitaifa. ulitakiwa kutoa pongezi kwa sababu huko nyuma walikuwa hawakamatwi.

Mimi huwa nampongeza mama shiku akitokelezea...
 
Unaonaje akikamatwa yule mpiga deal wenu mkuu akanyoosha maelezo kwa vitu alivyosafirisha na mkiwa mnamsifia kila kwa muda wote?

yule siyo kukamatwa tu yule Ni wa kunyonga maana Alisafirisha kontena zima tofauti na fuvu....
 
Kwa hiyo unakiri kuwa awamu ya nne ilikuwa janga..lakini uliitetea kulinda ugali wako

Kwa kuwa wewe ni mtetezi wa ccm sio ajabu awamu ya 6 ikija ukaponda ya 5..

Hao ndivyo walivyo. Hata Pombe alisifu sana safari za mkwere ulaya na US kuwa zinasaidia sana Maendeleo lakini kuingia tuu hotuba ya kwanza kamtukana kabisa kuwa alikuwa anakwenda sana nje kuliko alivyokuwa anaenda kumsalimia mama yake
 
Mlizi wa mfalme wa Oman akamatwa kwa kusafirisha fuvu la taiga kwenda Oman.
hii siyo breaking news kwa wanajf wengi swali langu kama anaesafirisha fuvu anakamatwa vipi waliosafirisha twigs wakiwa Hai..
au kwa kuwa ilikuwa dili la serikali...

Hivi umesikiliza habari kamili au umewahi tu kuleta uzi hapa? Unashindwa kutofautisha Burundi na Rwanda?
Mlinzi wa mfalme wa Oman au Mlinzi wa mfalme wa Qatar? Kama hujui uliza
 
Back
Top Bottom