Serikali iliyopita ya JK ilikuwa ya wapiga dili tu, nani alijali udhibiti wa raslimali za taifa, zilimhusu nini? Kama twiga anaweza kusafirishwa kwenye ndege pasipo kujulikana ni vingapi vilipita kabla? Huyu aliyekamata fuvu leo kwa maana ya taasisi alishindwaje kukamata wanyama zaidi ya 100 akiwamo twiga waliotoroshewa Uarabuni? Intelijensia ya vyombo vyetu vya dola huishia kupiga ramli ya kuwepo uvunjifu wa amani wakati vyama vya upinzani vikitaka kufanya maandamano au mikutano. Lakini intelijensia ya kutambua utoroshwaji wa nyara za taifa, utoroshwaji wa makontena yasiyolipiwa kodi, hujuma za ufujaji wa fedha kwenye taasisi za umma, mikataba mibovu nk, hizo huwa hawaziono.