Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,701
- 6,937
Mlinzi wa Dk Slaa,Kangezi,muda huu yupo makao makuu ya Chadema,akiwa na hali mbaya baada ya kushambuliwa na kuanzia asubuhi kwa tuhuma za kutaka kumuwekea sumu bosi wake
Kangezi alianza kupigwa kuanzia saa tatu asubuhi baada ya kuchukuliwa na walinzi wa Chama hicho na kupekuliwa nyumbani kwake kwa ajili ya kutafuta kitu kitakachomuhusisha na Nape,Mwigulu, Kinana na Mzee Mangula
Ikumbukwe Kangenzi licha ya kuwa msaidizi wa Karibu wa Dk Slaa ndiye alikuwa akilipwa fedha kidogo za mshahara kiasi kisichozidi sh. 400000 kwa mwezi
Huko kupiga kiasi hicho sio sahihi kwani ni kinyume ha haki za binadamu. Cha msingi ilikuwa kumhoji ili kupata ukweli. Kwa mfano huyo mlinzi akikatika, maneno ya Nape juu ya red guard si yatakuwa yametimia juu ya ugaidi.