Mlinzi atimuliwa kazi kwa ndoto.

Mlinzi atimuliwa kazi kwa ndoto.

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
3,811
Reaction score
1,607
Bosi alimuaga mlinzi wake kuwa kesho yake jioni anasafiri kuenda SA.
Usiku ule mlinzi akaota kunatokea ajali ya ndege ambayo bosi angesafiri.
Asubuhi yake akamjulisha bosi kuhusu ndoto yake ya ajali ya ndege, na bosi hakufanya ukaidi, akavunja safari.
Na kweli, ndege ile ilianguka na abiria wote walifariki. Usiku ule mlinzi alipokuja kazini, akakutia kuna mlinzi mwengine.
Alipokwenda kumwuliza bosi wake kulikoni, bos akajibu:
"Kazi basi, nilikuajiri ulinzi wa usiku, na sio kulala mpaka unaota ndoto. Kesho pita ofisini kwangu kuchukua mafao yako".
 
Hongera sana boss. Timua huyo, umemwajiri alinde ye analala!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom