Mlinzi adaiwa kumpiga risasi mwananchi Morogoro

Mlinzi adaiwa kumpiga risasi mwananchi Morogoro

Miss Halima

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
307
Reaction score
674
Mlinzi wa kituo cha mafuta cha Puma kilichopo Kata ya Kihonda Magorofani, Manispaa ya Morogoro, anadaiwa kumpiga risasi mwananchi aliyekuwa ameegesha gari katika eneo la kituo hicho.

Kwa mujibu wa mashuhuda akiwemo mwandishi wa TBC, mwananchi huyo alikuwa ameegesha gari katika eneo hilo kwa lengo la kufanya ibada katika msikiti mdogo uliopo ndani ya kituo hicho cha mafuta.

Hata hivyo, bado haijafahamika rasmi chanzo cha tukio hilo wala hali ya mwananchi huyo baada ya kupigwa risasi.

TBC inaendelea kufuatilia taarifa zaidi kutoka kwa mamlaka husika kuhusu tukio hilo.
SaveClip.App_801430336_1055580127104101_113701151167142340_n.jpg
SaveClip.App_801233172_1055580133770767_2908599185334369835_n.jpg
 
Mlinzi kama mlinzi ametuawakilisha vizuri kwenye hilo tukio.
Mna chuki sana wapuuzi nyie! Ndiomaana Samia anadili na nyinyi kiakili na bila kuwaangalia usoni! Nchimbi wenu kampiga chini, maana mlikuwa mnamtia ujinga kuwa kajiwekea ulinzi wakutosha,mara hakuna wakumtisha kanisa lipo nyuma yake!

Kiko wapi sasa na sharubu zake kama mfagio wa chachandu! Na bado mtatiwa sana adabu ....
 
Mlinzi wa Kituo cha Mafuta cha Puma kilichopo Kata ya Kihonda Maghorofani, Manispaa ya Morogoro, anadaiwa kumpiga risasi mwananchi aliyekuwa ameegesha gari katika eneo la kituo hicho.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mwananchi huyo alikuwa ameegesha gari katika eneo la kituo hicho kwa lengo la kwenda kufanya ibada katika msikiti mdogo uliopo ndani ya kituo hicho.

Mpaka sasa chanzo cha tukio hilo bado hakifahamika na Jambo Tv inaendelea kufuatilia kwa mamlaka ili kujua undani wa tukio hilo

HABARI PICHAMlinzi wa Kituo cha Mafuta cha Puma kilichopo Kata ya Kihonda Maghorofani, Manispaa.webp

Mbona hao walinzi wanakuwaga makini? Kwanzia lini wameanza tabia kama za hawa migambo wanaopiga wamama mateke sokoni?
Kama kuna cctv itasaidia sana pande zote kupata haki
 
Mlinzi wa kituo cha mafuta cha Puma kilichopo Kata ya Kihonda Magorofani, Manispaa ya Morogoro, anadaiwa kumpiga risasi mwananchi aliyekuwa ameegesha gari katika eneo la kituo hicho.

Kwa mujibu wa mashuhuda akiwemo mwandishi wa TBC, mwananchi huyo alikuwa ameegesha gari katika eneo hilo kwa lengo la kufanya ibada katika msikiti mdogo uliopo ndani ya kituo hicho cha mafuta.

Hata hivyo, bado haijafahamika rasmi chanzo cha tukio hilo wala hali ya mwananchi huyo baada ya kupigwa risasi.

TBC inaendelea kufuatilia taarifa zaidi kutoka kwa mamlaka husika kuhusu tukio hilo.
View attachment 3666410View attachment 3666407
Nimeomba nipewe bastola huu mwaka wa tano sasa mm nataka bastola serikali inipe bastola.
 
Hivi hawa wanapitia kozi za ulinzi, kichwani huwa wako timamu?
Huyu achukuliwe na mkono was sheria uwe pembeni yake, ila km Taifa tulipofika ni pabaya, 😢😢😢
Hata wewe ungekua mlinzi usingekua timamu
Mtu unalala nje mwezi mzima ili uje kupewa laki mbili na nusu
 
Hivi kama tukio lina ushahidi kwanini bado linatamkwa kuwa inadaiwa kufanya hivi na vile wakati mtuhumiwa kafanya tukio wazi kabisa,
 
Hakuna mahali nimeonesha chuki yangu kwa mtu aliyeuwawa! Na hata dini yake hainihusu. Nimeongelea kwa mtazamo tofauti kabisa na huu wa kwenu. Ni bahati mbaya mmeshindwa kunielewa.

Mimi nimemaanisha mlinzi kukosa weledi kiasi cha kufyatua risasi pasipo na sababu za msingi. Thats why nikasema mlinzi amewakilisha vyema walinzi wa aina hiyo (wasiokuwa na mafunzo sahihi ya kutumia silaha za moto)! Nashangaa mnanishambulia huku mkihusisha mambo ya dini, na Chadema! Wakati mwingine kama hujamuelewa mtu, uliza.
Uandishi wako ndo ulokuponza
 
Back
Top Bottom