Mlinzi adaiwa kumpiga risasi mwananchi Morogoro

Mlinzi adaiwa kumpiga risasi mwananchi Morogoro

Mlinzi wa kituo cha mafuta cha Puma kilichopo Kata ya Kihonda Magorofani, Manispaa ya Morogoro, anadaiwa kumpiga risasi mwananchi aliyekuwa ameegesha gari katika eneo la kituo hicho.

Kwa mujibu wa mashuhuda akiwemo mwandishi wa TBC, mwananchi huyo alikuwa ameegesha gari katika eneo hilo kwa lengo la kufanya ibada katika msikiti mdogo uliopo ndani ya kituo hicho cha mafuta.

Hata hivyo, bado haijafahamika rasmi chanzo cha tukio hilo wala hali ya mwananchi huyo baada ya kupigwa risasi.

TBC inaendelea kufuatilia taarifa zaidi kutoka kwa mamlaka husika kuhusu tukio hilo.
View attachment 3666410View attachment 3666407
ni vizuri kuzingatia sheria za maegesho ya magari na kuheshimu watu kwenye maeneo yao ya kazi.

Lakini pia ni muhimu sana wananchi wote kua wastahilivu na wenye subra wakati mamlaka za uchunguzi wakifuatilia ukweli wa songombingo hiyo ya fedheha sana 🐒
 
Back
Top Bottom