Mlimani city "kama nawatch movie"!

Mlimani City kwani nayo mall hiyo? Hata strip malls za mbele ni kali kuliko hiyo Mlimani City. Kwanza imekaa kama banda flani la kuku wa mayai hivi....

Location Ngabu! Ukiwa Bongo utaipenda Mlimani City. Sasa hivi unaiponda kwa vile uko Marekani, ila ukiwa Bongo hakuna eneo zuri zaidi ya Mlimani City.

Mojawapo ya sababu zinazofanya ipendwe ni ina eneo kubwa ambalo liko air-conditioned. Watu wakiwa mle ndani wanapigwa kipupwe na hewa ni safi haina vumbi wanajiona kama wako Ulaya. Maana jua la nje ni kali kuliko, na vumbi ni jingi. Bongo iko tofauti ... Marekani jua linatafutwa, Bongo jua linakimbiwa.
 
duh Nyani Ngabu kanivunja mbavu humu! Alafu NN kwenye hii thread katoka na Swaga za hashcool wa JF mpaka nahisi ni the same person aisee!
 
Mlimani City ni ufisadi...haiikaribii hata Waterfront Cape Town. Ni sawasawa na godown lenye AC na mbwembwe. Hamna kitu cha kushangaza pale.
 
nyie ndo akina mange wa pili mnatuharibia vijana wetu kwa kuwatamanisha arrrrghh..........
 
mh! Hapa naona kila kitu kigeni, kama niko ndotoni vile! Hebu nisepe zangu mie
 
Wabongo bwana..Mall itakuwa mlimani city mpk walete mapozi wakiwa mle ndani? Watu watembee kdg waone tulivyo upupu mbele ya Mall za wenzetu....
Acha waterfront hata Cavendish pale Claremont ( Cape town) haifikii!! Kalagabaho...
 
Mlimani City ni KUBWA SANA
hivi unajua humo wanajaa Tembo wangapi?

Haya utalinganisha na duka la mpemba au genge la mangi?

Mbona mnalinganisha utamu wa nyama na chungwa?

Linganisha nyama kwa nyama na chungwa kwa chungwa

Heavy weight hawezi pigana na Light weight.

Najua mnajua ni kubwa saana hata twiga anaingia na hajikunji

Wabongo bwana..Mall itakuwa mlimani city mpk walete mapozi wakiwa mle ndani? Watu watembee kdg waone tulivyo upupu mbele ya Mall za wenzetu....
Acha waterfront hata Cavendish pale Claremont ( Cape town) haifikii!! Kalagabaho...
 
mkuu hapo kwenye! red .. nilipata shori flani alinambia tukutane hapo.. ebana balaa.. niliingia vichomi! ilibidi nimwambie ebana bili si nusu kwa nusu ...
ungejifanya tu kidume, na huyo shori unaye mpaka leo?
 
Huu mjengo pembeni ya Sam Nujoma Road unambwembwe zake ukiingia mle ndani watu wanabehave kama vile si watz, kama vile hii nchi haina matatizo (umeme) watu wanaspeak kwa Swaga balaa..mara "you know" or "actually" nasema haya coz nilizungumza watu tofauti mle ndani nkasema may be huku siko tz nnayoijua,watu wako class ,happy ,watanashati ,health ! mazingira hayo yakapelekea nione kama Nawatch aina fulani ya movie!
watu tumetofautiana, mie mlimani city sijui napaonaje, yani binafsi sipapendi. ni mtazamo tu
 
ishu siyo majuu nao wanakuja huku'najua tumekuzwa na magenge nauliza bongo malls za ukweli !
Hivi wewe unataka kujidai mgeni sana au? Yaani uko hapa Bongo halafu unajidai unauliza kuhusu mall za ukweli? Na umetoka kusema jamaa wasanii sana hapo Mlimani City, hivi unataka kutuambia nini kuhusu wewe mwenyewe, halafu we si mate wangu kule Arusha wewe, usiniangushe bana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom