Mkuu wa zamani wa Majeshi ya Ulinzi is NO MORE

Watu waliotoa michango ya ukweli kwa Taifa letu (kama kina Shaban Robert, Prof Haroub Othman, Gen Mayunga, Gen Walden, Mzee Pwagu, Mzee Jongo na jabali la muziki Marijani Rajabu nikitaja wachache tu) serikali na vyombo vya habari uchwara (specifically Clouds) hawawapi umuhimu unaostahili! Lakini kina Kanumba (mtu ambae ni mzazi wa mtoto mdogo hapa ajitokeze kama angependa Kanumba awe role model wa mwanae) wanapewa coverage ya ajabu! Sina shida na Kanumba kupendwa/kuheshimiwa na watu wa aina yake, lakini kupewa sura ya kitaifa!!!??? Naungana na Rev Masanilo kwenye thread yake ya kutuzodoa Watanzania.

Tunaendeleza mkakati wa kuunda Taifa kubwa la kiswahili swahili Duniani. Hatujui tunafanya nini...tunaenda na jinsi upepo unavyovuma.
 
Nadhani kwa kuonesha utofauti wetu ..wa kimtazamo...na utaifa wetu ...,wana JF tuonyeshe njia ....tuwape umuhimu mkubwa wiki hii yote ...

mkuu wa jeshi la polisi mstaafu harun mahundi
mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama mstaafu Ernest Mwita Kiaro...

Kwa kuwa hawa wanafiki na wapambe wao wanapita humu wataona aibu ....na kujirekebisha.....

1. Tuweke thread stick ya kuwakumbuka mashujaaa waliotukuka ernest mwita kiaro na harun mahundi
2.tuweke picha zao angalau ndogo kwenye home page yetu hadi ijumaaa

MoD Naomba kutoa hoja......kwa minajili ya kunyoosha taifa ....na kurudisha misingi na priorities kadiri inavyotakiwa.....
Kwa kweli naunga mkono hii hoja kwa asilimia zote.
 
RIP Gen Kyaro. . . Swali la kizushi kwanini wakuu wengi wa majeshi wanatoka mkoa wa Mara ?.
Mkoa wa Mara kila kijana wa kiume anaezaliwa, anazaliwa akiwa Mwanajeshi kamili sasa humu jeshini huwa wanakuja kuandikishwa tu, Mkoa wa Mara ndio unaongoza kwa watu jasiri na hata uchaguzi Mkuu uliopita Jimbo la Musoma mjini ndio lilikuwa la kwanza kumtangaza Vicent Nyerere kwamba ameshinda, maana NEC wanafahamu vyema watu wa Mara hawahitaji mzaha.
Lakini haya Maswali mengine ni ajabu hivi unategemea Mmatumbi, Mluguru, Mkwerre na Mpemba awe CDF kweli?
 
Ha ha ha ha! Mbona tuna Amiri Jeshi Mkuu? Chunga maneno yako mkuu.
 
Ha ha ha ha! Mbona tuna Amiri Jeshi Mkuu? Chunga maneno yako mkuu.
Hivi hujui tofautI kati ya Amiri Jeshi na CDF? Raia yeyote anaweza kuja kuwa Amiri jeshi, lakini CDF ni lazima uwe mwanajeshi na sio cheo Ceremonial.
Si afadhali hata JK jeshini alikuwa Luten Kanal kuliwa huyu Ben Mkapa (kipipa )
 
we are all nearing home.................the eternal one..................nothing to worry about except if you despise OUR LORD and SAVIOUR JESUS CHRIST.........
 
Mungu amlaze mahala pema peponi. Huyu alikuwa kamanda kweli na si kamanda wa kujilimbikizia mali. Alikuwa hataki ration ya nyama toka jeshini yeye alikuwa akisema chakula cha mwanajeshi ni dry ration yaani biskuti na mikate! Watoto wake walikuwa wakila chakula cha mchana pale Tambaza na kupanda UDA na daladala kama wavuja jasho wengine.
 
Hivi hujui tofautI kati ya Amiri Jeshi na CDF? Raia yeyote anaweza kuja kuwa Amiri jeshi, lakini CDF ni lazima uwe mwanajeshi na sio cheo Ceremonial.
Si afadhali hata JK jeshini alikuwa Luten Kanal kuliwa huyu Ben Mkapa (kipipa )

Kwa viwango Huyu ...lt col Jakaya khalfan Mrisho KIkwete .....pamoja na kuwa amepata kuwa askari ....hamfikii Ben Mkapa kwa uongozi wake Kama amiri jeshi mkuu....
 
Unajua PM mimi niliamini askari akishakuwa officer lazima awe sawasawa kimaadili, kiistrategy na kadhalika. Sasa huyu Col au sijui Luten Col yeye alikuwa Geshi gani? Maana tunayoyaona ni tofauti na yanayoendelea jeshini

Hiri ri Kanari letu la sasa ririkkuwa li siasa...harikuwa ripiganaji au hata ripiganishaji......wenzake kina komba,Nnauye...etc
 
Ha ha ha ha duh huko Mara hakufahi kabisa kila nyumba ina mjeshi.

Mkoa wa Mara kila kijana wa kiume anaezaliwa, anazaliwa akiwa Mwanajeshi kamili sasa humu jeshini huwa wanakuja kuandikishwa tu, Mkoa wa Mara ndio unaongoza kwa watu jasiri na hata uchaguzi Mkuu uliopita Jimbo la Musoma mjini ndio lilikuwa la kwanza kumtangaza Vicent Nyerere kwamba ameshinda, maana NEC wanafahamu vyema watu wa Mara hawahitaji mzaha.
Lakini haya Maswali mengine ni ajabu hivi unategemea Mmatumbi, Mluguru, Mkwerre na Mpemba awe CDF kweli?
 
Unajua PM mimi niliamini askari akishakuwa officer lazima awe sawasawa kimaadili, kiistrategy na kadhalika. Sasa huyu Col au sijui Luten Col yeye alikuwa Geshi gani? Maana tunayoyaona ni tofauti na yanayoendelea jeshini

Aliona hapamfai, kulikua na thread hapa mwaka jana au mwaka juzi ya kwnn alitoka jeshini

they say, "if u cant handle the heat, get out of the kitchen"
 
Back
Top Bottom