Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius S. Mtatiro aapishwa kuwa Wakili

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
691
878
MTATIRO AAPISHWA KUWA WAKILI

Katika sherehe za 66 za kupokea Mawakili wapya leo, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Julius S. Mtatiro Esq. ni miongoni mwa mawakili wapya 335 walioapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma kuwa Mawakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama zilizopo chini yake isipokuwa Mahakama za Mwanzo.

DC Mtatiro ana shahada za juu takribani nne, ambazo ni Shahada ya Sanaa katika elimu (BAED), Shahada ya Sheria (LLB), Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Umma (MPA), Shahada ya Uzamili ya Sera za Umma (MAPP), Stashahada ya Juu ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo (PDLP), Cheti cha Juu cha Uongozi na Cheti cha Juu cha Tafsiri na Ukalimani kati ya Lugha ya Kiingereza na Kiswahili na vyeti vingine vingi.

IMG-20220708-WA0004.jpg
IMG-20220708-WA0005.jpg
IMG-20220708-WA0006.jpg
 
Huyu jamaa anaonekana ana uwezo wa kusoma saana.

sasa ilitakiwa apewe kazi inayoendana na huo uwezo.labda hata kuwa Ded au Ps wa wizara hiv.naona kama Dc hahitaji mavyeti yote hayo.kwa sababu Dc hana vitu vingi sana vya kusoma soma
 
Naona hapo kwenye paji la uso haviendani na jina lake.
 
huyu mwamba nilivyokuwa o level yeye alikuwa form six nafikiri ifakara secondary alikuwa ana mbwembwe alikuwa anahusika na mambo ya vyakula this dude kwenye foleni ya chakula ukizingua alikuwa anapita na wewe mzima mzima ha ha
 
Ifakara secondary alikuwa kiongozi, halafu alikuwa mnoko sana, kuna siku alimletea noma mshikaji anaitwa victor Mtitu aka Mdundo. Issue ilikuwa ndogo lakini ilifika mpaka kwa walimu.
 
Naona hapo kwenye paji la uso haviendani na jina lake.
Chama alichokua awali kabla ya kuingia Lumumba ndo kilimbadili kutoka kuwa mgalatia na kuwa mmadina . si unajua chama kile wafadhili wake ni itikadi Kali ?
 
Ifakara secondary alikuwa kiongozi, halafu alikuwa mnoko sana, kuna siku alimletea noma mshikaji anaitwa victor Mtitu aka Mdundo. Issue ilikuwa ndogo lakini ilifika mpaka kwa walimu.
ha ha kaka tutakuwa tunajuana aisee mm nilikuwa bweni la castro sikupi code halafu seems tunaweza kuwa group moja la ifakara alumni ha ha
 
Ifakara secondary alikuwa kiongozi, halafu alikuwa mnoko sana, kuna siku alimletea noma mshikaji anaitwa victor Mtitu aka Mdundo. Issue ilikuwa ndogo lakini ilifika mpaka kwa walimu.
mwamba wewe ndio victor mtitu nini wazee wa upper layer hiyo 2001 nafikiri
 
Back
Top Bottom