Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Majidi amefanya ziara ya kutembelea vyanzo vya maji katika Kata ya Mamba iliyoko Halmashauri ya Mlele ambapo amekerwa kwa kuona mifuko ya saruji iliyotakiwa kutekeleza mradi wa kutengeneza tanki la maji imeganda kwa sababu ya kuhifadhiwa bila utaratibu mzuri.
Musitafa Kipeta ambaye ni Diwani wa Kata ya Mamba amesema kucheleweshwa kwa mradi huo kitaisababishia Serikali gharama huku Joshua Mbwana ambaye ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Mlele amesema fedha za Serikali inatoa pesa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi lakini baadhi ya watu si waaminifu katika kuthamini pesa za serikali.
Mradi huo wa tanki endapo utakamilika utanufaisha Kata ya Mamba, Kata ya Kasansa na Maji Moto ambapo ni zaidi ya wananchi laki mbili.