TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 13,773
- 21,272
Katika hali ambayo haijazoeleka miongoni mwa jamii, leo jijini Arusha katika uzinduzi wa Kampeni za Uhamasishaji wananchi kujiunga na vifurushi vipya vya Bima ya Afya, Mkuu wa Mkoa huo alisitisha hotuba kwa dakika kadhaa ili kupisha Adhana iliyokuwa ikisikika kutoka jirani na eneo la uzinduzi.
Hali hiyo haikuleta taharuki ila baadhi ya wananchi waliokuwepo uwanjani hapo waliuliza nini maana yake, pamoja na adhana kuwepo kila siku sehemu mbalimbali ila haijapata kutokea kiongozi ambaye ni mgeni rasmi kusitisha kwa muda hotuba ili sheikh anayeazini amalize.
Wataalam wa itifaki mnaweza kutiririka hapa chini, hii inakuwaje?
=====
Hali hiyo haikuleta taharuki ila baadhi ya wananchi waliokuwepo uwanjani hapo waliuliza nini maana yake, pamoja na adhana kuwepo kila siku sehemu mbalimbali ila haijapata kutokea kiongozi ambaye ni mgeni rasmi kusitisha kwa muda hotuba ili sheikh anayeazini amalize.
Wataalam wa itifaki mnaweza kutiririka hapa chini, hii inakuwaje?
=====
Mwaka mmoja Rais Julius Nyerere alifanya ziara mkoani Tanga, baada ya kusikiliza kero za wana Tanga, kuna mambo kadhaa aliyabaini.
Watu wa Tanga walikuwa hawataki kuwatumia wanyama wao kwa shughuli za kipato mfano kilimo, kuteka maji na kubebea mizigo wanyama hao kama punda na ngombe wakidai ni dhambi kwa Mungu.
Mwalimu alikuwa na akili nyingi sana akaona hapa ntawambiaje hawa watu waachane na imani hizi? .
Ndipo akampandisha jukwaani Waziri wake wakati huo Alhaj Ali Hassan Mwinyi(aliyekuwa ameongozana nae kwenye ile ziara)Mwalimu alimtaka Mzee Mwinyi awaeleze wana Tanga uislamu na Qur an unaelezeaje matumizi ya wanyama kama punda na ngombe?.
Ndipo hapo Mzee Mwinyi(mahiri na fasaha sana wa Qur an na lugha) akaanza kutoa baadhi ya aya na hadith za Mtume kuonyesha kuwa sio dhambi na yafaa kabisa wanyama kutumika kwenye shughuli za kuzalishia mali ila tu haki zao zilindwe(ikiwemo kutokuchoshwa sana, kupewa maji na chakula kwa wakati, kutofanyishwa kazi wanyama wazee, wadogo wagonjwa na wenye mimba)
Baada ya kushuka jukwaani wana Tanga wakawa wameewelewa uzuri kabisa kuhusu matumizi ya wanyama na hapo ikamsaidia Mwalimu kufikisha ujumbe wake.
Lakini tazama hekima za Mwalimu, aliona pamoja na umahiri wake wa kushawishi na kutoa hotuba lakini aliona hapa maneno ya kisiasa hayatoweza kusaidia kitu, tutumie maneno haya haya ya dini tena toka kwenye kitabu chao(qur an tukufu) ambacho wanamiamini.
Nimeleta mfano huu kuonyesha kuwa kuvumiliana hata kama tunapishana kiimani ni tamaduni toka enzi na enzi.
Mwalimu hakuwa muislamu lakini aliona hapa ili nieleweke vyema nimlete mtu mfasaha wa dini ya kiislamu kunisaidia kueleza hiki ninachotaka kuwaelimisha hawa kwa kuwa idadi ya hawa ninaowahutubia ni Waislamu
Ni hayo tu kwa sasa!!
Sent using Jamii Forums mobile app