Mkuu wa Mkoa asitisha hotuba kupisha adhana

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,591
20,748
Katika hali ambayo haijazoeleka miongoni mwa jamii, leo jijini Arusha katika uzinduzi wa Kampeni za Uhamasishaji wananchi kujiunga na vifurushi vipya vya Bima ya Afya, Mkuu wa Mkoa huo alisitisha hotuba kwa dakika kadhaa ili kupisha Adhana iliyokuwa ikisikika kutoka jirani na eneo la uzinduzi.

Hali hiyo haikuleta taharuki ila baadhi ya wananchi waliokuwepo uwanjani hapo waliuliza nini maana yake, pamoja na adhana kuwepo kila siku sehemu mbalimbali ila haijapata kutokea kiongozi ambaye ni mgeni rasmi kusitisha kwa muda hotuba ili sheikh anayeazini amalize.

Wataalam wa itifaki mnaweza kutiririka hapa chini, hii inakuwaje?

=====
Mwaka mmoja Rais Julius Nyerere alifanya ziara mkoani Tanga, baada ya kusikiliza kero za wana Tanga, kuna mambo kadhaa aliyabaini.

Watu wa Tanga walikuwa hawataki kuwatumia wanyama wao kwa shughuli za kipato mfano kilimo, kuteka maji na kubebea mizigo wanyama hao kama punda na ngombe wakidai ni dhambi kwa Mungu.

Mwalimu alikuwa na akili nyingi sana akaona hapa ntawambiaje hawa watu waachane na imani hizi? .

Ndipo akampandisha jukwaani Waziri wake wakati huo Alhaj Ali Hassan Mwinyi(aliyekuwa ameongozana nae kwenye ile ziara)Mwalimu alimtaka Mzee Mwinyi awaeleze wana Tanga uislamu na Qur an unaelezeaje matumizi ya wanyama kama punda na ngombe?.

Ndipo hapo Mzee Mwinyi(mahiri na fasaha sana wa Qur an na lugha) akaanza kutoa baadhi ya aya na hadith za Mtume kuonyesha kuwa sio dhambi na yafaa kabisa wanyama kutumika kwenye shughuli za kuzalishia mali ila tu haki zao zilindwe(ikiwemo kutokuchoshwa sana, kupewa maji na chakula kwa wakati, kutofanyishwa kazi wanyama wazee, wadogo wagonjwa na wenye mimba)

Baada ya kushuka jukwaani wana Tanga wakawa wameewelewa uzuri kabisa kuhusu matumizi ya wanyama na hapo ikamsaidia Mwalimu kufikisha ujumbe wake.

Lakini tazama hekima za Mwalimu, aliona pamoja na umahiri wake wa kushawishi na kutoa hotuba lakini aliona hapa maneno ya kisiasa hayatoweza kusaidia kitu, tutumie maneno haya haya ya dini tena toka kwenye kitabu chao(qur an tukufu) ambacho wanamiamini.

Nimeleta mfano huu kuonyesha kuwa kuvumiliana hata kama tunapishana kiimani ni tamaduni toka enzi na enzi.
Mwalimu hakuwa muislamu lakini aliona hapa ili nieleweke vyema nimlete mtu mfasaha wa dini ya kiislamu kunisaidia kueleza hiki ninachotaka kuwaelimisha hawa kwa kuwa idadi ya hawa ninaowahutubia ni Waislamu

Ni hayo tu kwa sasa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli ametumia busara kubwa sana, ingawa yeye ni wa imani nyingine. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, big up RC, ingekuwa ni Bashite angeitumia hiyo opportunity ku-create mgogoro usiokuwa na ulazima.
Mrisho ni imani nyungine mkuu?
 
Kwa kweli ametumia busara kubwa sana, ingawa yeye ni wa imani nyingine. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, big up RC, ingekuwa ni Bashite angeitumia hiyo opportunity ku-create mgogoro usiokuwa na ulazima.
RC wa Arusha Ni Muislamu! Ameonyesha Kushika Dini yake Vilivyo. Huwezi ukawa unaongea na kuingilia adhana inayosema Allah Mkubwa Allah Mkubwa na wewe ukaweka misauti yako na udogo wako ulonao!

Ila nshawahi kugonga mzigo gesti moja ipo karibu na msikiti huku adhana inapigwa!
 
Kwa kweli ametumia busara kubwa sana, ingawa yeye ni wa imani nyingine. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, big up RC, ingekuwa ni Bashite angeitumia hiyo opportunity ku-create mgogoro usiokuwa na ulazima.
Akili zingine hizi,kama hujui siyo lazima uchangie,jina MRISHO na adhana kunaimani tofauti hapo?
 
Hili ni suala tu la Viongozi wa Serikali kuonesha utii kwa mambo ýanayohusu imani. Kwa vile huyu kiongozi ni muislamu na anafahamu taratibu za adhana ilikuwa ni lazima afanye alichokifanya.

Katika tukio linalofanana na hili mwaka 1992 Rais, mstaafu wa Awamu ya II Mzee Mwinyi akiwa anahutubia maelfu ya wananchi wa mji wa Bukoba katika mwanja ujulikanao kama Uhuru Platform maarufu kama uwanja wa Mayunga,alisitisha hotuba yake kwa muda ili kupisha adhana iliyoanza kutolewa wakati anaendelea kuhutubia. Baada ya mtoa adhana kukamilisha, mzee wetu huyu alisema maneno yafuatayo huku akiwa ni mwenye bashasha, "Mji wa Bukoba ni kama Mji wa Makka".
Hivyo, bwana Gambo si wa kwanza kufanya tukio hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka mmoja Rais Julius Nyerere alifanya ziara mkoani Tanga, baada ya kusikiliza kero za wana Tanga, kuna mambo kadhaa aliyabaini.

Watu wa Tanga walikuwa hawataki kuwatumia wanyama wao kwa shughuli za kipato mfano kilimo, kuteka maji na kubebea mizigo wanyama hao kama punda na ngombe wakidai ni dhambi mbele za Mwenyezi Mungu.

Mwalimu alikuwa na akili nyingi sana akaona hapa nitawambiaje hawa watu waachane na imani hizi? .

Ndipo akampandisha jukwaani Waziri wake wakati huo Alhaj Ali Hassan Mwinyi(aliyekuwa ameongozana nae kwenye ziara ile)Mwalimu alimtaka Mzee Mwinyi awaeleze wana Tanga uislamu na Qur an unaelezeaje matumizi ya wanyama kama punda na ngombe?.

Ndipo hapo Mzee Mwinyi(mahiri na fasaha sana wa Qur an na lugha) akaanza kutoa baadhi ya aya na hadith za Mtume kuonyesha kuwa sio dhambi na yafaa kabisa wanyama kutumika kwenye shughuli za kuzalishia mali ila tu haki zao zilindwe(ikiwemo kutokuchoshwa sana, kupewa maji na chakula kwa wakati, kutofanyishwa kazi wanyama wazee, wadogo wagonjwa na wenye mimba)

Baada ya kushuka jukwaani wana Tanga wakawa wameewelewa uzuri kabisa kuhusu matumizi ya wanyama na hapo ikamsaidia Mwalimu kufikisha ujumbe wake.

Lakini tazama hekima za Mwalimu, aliona pamoja na umahiri wake wa kushawishi na kutoa hotuba lakini aliona hapa maneno ya kisiasa na kifalsafa hayatoweza kusaidia kitu, tutumie maneno haya haya ya dini tena toka kwenye kitabu chao(qur an tukufu) ambacho wanakiamini.

Nimeleta mfano huu kuonyesha kuwa kuvumiliana hata kama tunapishana kiimani ni tamaduni toka enzi na enzi.
Mwalimu hakuwa muislamu lakini aliona hapa ili nieleweke vyema nimlete mtu mfasaha wa dini ya kiislamu kunisaidia kueleza hiki ninachotaka kuwaelimisha hawa kwa kuwa idadi ya hawa ninaowahutubia ni Waislamu

Ni hayo tu kwa sasa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom