Shida mnaanzisha thread halafu kuleta updates hamleti mkitegemea wengine wafanye hivyo! Kama huwezi kuleta updates pamoja na picha tafadhali kaa pembeni waachie wenye nia na uwezo wafanye hivyo. Hata thread yenyewe maelezo nusu nusu - hayajitoshelezi. Ungekuwa serious ungetueleza yafuatayo:- - Muonekano na matayarisho hapo uwanjani kwa ujumla yakoje hadi sasa - bendera za chama, majukwaa, vikundi vya ngoma, dansi, n.k. - Viongozi gani wanatarajiwa kuwepo kwenye huo mkutano - viongozi wa wilaya, mkoa, taifa, madiwani, wabunge, n.k. - Viongozi gani mpaka sasa wameshawasili au wako maeneo ya mkutano - viongozi wa wilaya, mkoa, taifa, madiwani, wabunge, n.k. - Mwitikio na hamasa ikoje - waliovalia mavazi na nembo zingine za chama, gari ya matangazo, vipeperushi, mabango, n.k. -Jamaa wa intelijensia vipi? Wameshaanza kuranda randa maeneo ya karibu, migari yao ya kuwasha, n.k. - Ni mambo gani hasa makubwa yanayotarajiwa kujiri katika mkutano wa leo - wengine tunasikia kuna maelfu ya wana-CCM watakaorudisha kadi; Je, ni kweli? n.k. Halafu, kwa taarifa yako sio "Mpango" ni "Operesheni".