Mkutano wa CHADEMA viwanja vya NMC Arusha

Mkutano wa CHADEMA viwanja vya NMC Arusha

JKwakati anatangaza baraza lake jana alikuwa na wenge over siafu alikuwa anajua nini anafanya madudu tupu
 
Mimi ni mtu wa Kusini...CCM imetusaliti na CDM siiamini japo kwa punje ya uwele!! Huwa najiuliza, ikiwa CDM inatutupa mkono wakati wa kuitafuta keki ya taifa, je watatukumbuka wakati imeshapatikana!!!? napata shaka hasa nikikumbuka jinsi ambavyo Dr. Slaa alienda kusini kuomba kura! In few hourz, akapiga kampeni kwenye mikoa miwili....lakini bado wanatushawishi kwamba waliibiwa kura! Kama kuna mtu ninayemuona mjinga kuishabikia CDM basi ni mtu wa kusini unless kama ana nasaba na kaskazini!! Mtanzania mwingine yeyote labda anaweza kuishabikia CDM lakini sio mtu wa kusini!

Kutokana na mwenendo huu wa CDM ndio maana naiangalia kauli ya Dogo Janja kwa jicho la pili...!!
Nasdaz, umeandika maneno mengi badala ya kunyoka kwenye pointi yako......Kuhusu swala la chadema kutokufika kusini ilikuwa ni makubaliano ya chadema na CUF, kuwa CUF kwa kipindi hicho ilikuwa inakubalika sana pwani basi wao wachukue maeno hayo wakiwa na maana kamawakichukua pwani na CHADEMA wakachukua bara basi wange waondoa CCM kiurahisi bahati mbaya sana CUF wamewa sariti chadema, lakini kwasasa chadema inajipanga kuingia mikoa yote ya pwani siku si nyingi....Nimekuwa nikikusoma siku nyingi sana kuna kipindi huwa unaonyesha mahaba na chama cha mapinduzi na kuna wakati huwa neutral sijui ndiyo dalili za kujivua gamba....Karibu sana Chadema
 
CDM inawatumia mbumbumbu,wachumia matumbo na wasiotambua malengo yaliyofichwa ya hiki chama.Hakuna ubishi hiki chama ni cha kikabila! Chacha wangwe alipotaka kugombea uenyekiti,mizengwe kibao iliibuliwa,Zitto naye anang'ang'ana hatafanikiwa kamwe! Uenyekiti ni wa wenye chama tu,wachaga.Bob makan aliukwaa uenyekiti baada ya mtei coz ameoa na kujenga uchagani na alikuwa hana maamuzi(rubber stamp).Inatisha sana.

Ninyi hamjioni mnavyotumiwa na ccm kama makarai ya zege ambayo huwa baada ya ujenzi hayana kazi. Poleni sana.
 
Ali Hassan Mwinyi - Wizara ya Afya Tanzania 1972 mpaka 1975
Ali Hassan Mwinyi - Wizara ya Mali asili na utalii Tanzania 1982 mpaka 1983.

Ahmed Hassan Diria - Wizara ya habari na Utangazaji Tanzania - 1989 mpaka 1990.

Unataka niendelee!!!!
Kabla ya kuanza kunitajia ulipaswa kujibu swali la kwanza ndiyo ungeweza kujinafaasi kunitajia...
 
UNAPOONA KATIBA IMEVUNJWA, MWANASHERIA WA NINI?, KWANI MBOWE NI MBUMBUMBU WA SHERIA KAMA UNAVYODHANI,MPAKA HAPO ALIPO UNAMWONAJE?...TAFAKARI....LISSU TUNDU KATIKA KESI YAKE ALIWEKA MWANASHERIA GANI, ALIVUNJA KATIBA KWA KUTOKUWA NA MWANASHERIA?

MBALI ZAIDI: WAKATI WA HARAKATI ZAKE ZA UKOMBOZI KULE SINGIDA, ALIIWAHISHA HAKI YA KUWA MBUNGE?HAPA (NAMAANISHA ALITOA RUSHWA) ALIICHELEWESHA KWA NAMNA YEYOTE ILE?

HAYA SI MALUMBANO YA HOJA, BALI NI NGUVU YA HOJA KUHUSU UHALALI WA F.A MBOWE KUJADILIANA NA MWANASHERIA KUHUSU UHALALI WA MTU KUPEWA UBUNGE ASUBUHI NA UWAZIRI JIONI HATA KABLA YA KUAPISHWA NA SPIKA KTK UHALALI WA UBUNGE WAKECCM WANA FRUSTRATIONS HIVYO HAWAWEZI,:whoo: HII NCHI TENA.
 
Ukweli ni kwamba kwa mwamuko ulioko Mbeya, Mwanza, Shinyanga. Simiyu, Geita, Songea, Dar...na kwingineko chadema inapaswa kuanza kuchanga karata zake vizuri maana mwaka 2015 wao ndiyo wataongoza nchi hii....
 
nzenga kaya, unaifahamu vizuri historia ya CDM kweli, hiki chama ni mali ya umma, hata wewe ukija unapokelewa tu hakina chuki binafsi. hakuna mwenye hati miliki ya chadema, nakwambia hata mzee mtei aliyekianzisha hana, hati miliki ya chadema iko mikononi mwa wananchi wote pamoja na wewe. neno umma lina maana pana sana.hivyo hiki ni chama cha umma, tena sio umma dhaifu bali umma wenye nguvu, wenye maamuzi,umma mkomavu,mkakamavu,umma mpevu,umma unaofahamu vizuri nguvu zake.

achana na ile sera ya ccm mtu kachaguliwa na umma halafu serikali ya chama inasema amestaafishwa kwa manufaa ya umma.niulize umma upi huo ambao wana hisa hawakutaarifiwa? kwanini uwafiche kuhusu kipenzi chao?.cdm ilipowasimamisha madiwani kwa manufaa ya umma kule arusha iliushirikisha umma.ilifanya mikutano katika kila kata ambayo diwani ametoka na kuwaeleza sababu za kutowakubali tena.

umma una nguvu, na si chadema kama chama, bali sera safi na za uwazi za chadema ndio zinawapa umma nguvu ya maamuzi..katika kuishiriki hiyo keki ya taifa bila upendeleo.kila mtu lazima aionje utamu wake-hapa namaanisha huduma zote za kijamii na si za kifisadi za kubaguana na kujilimbikizia mali.

umma una nguvu kuliko upepo upitao, upepo wa kisulisuli,kuliko dhoruba,kuliko kimbunga chochote ulichowahi kukisikia au hata kukiona. usiombe hiyo nguvu ikakushukia..hakika utabadilika.kama ni dhambi unaacha zote, unasafishwa na kuwa safi kama dhahabu safi,unatakata ndugu yangu.
 
CDM inawatumia mbumbumbu,wachumia matumbo na wasiotambua malengo yaliyofichwa ya hiki chama.Hakuna ubishi hiki chama ni cha kikabila! Chacha wangwe alipotaka kugombea uenyekiti,mizengwe kibao iliibuliwa,Zitto naye anang'ang'ana hatafanikiwa kamwe! Uenyekiti ni wa wenye chama tu,wachaga.Bob makan aliukwaa uenyekiti baada ya mtei coz ameoa na kujenga uchagani na alikuwa hana maamuzi(rubber stamp).Inatisha sana.
Nionyeshe chama ambacho wafuasi wake hawna kabila ili tukisapoti.
 
Mungi, Crashwise na makamanda wengine big up sana. Nimesoma na kuhabarika.
 
Hapa kidogoo nimekuwa shocked.......picha ninayopata kumbe ni kweli mwanachama maarufu wa CDM alitamka kauli hiyo mbele ya kadamnasi, hata hivyo mwenyekiti wa chama akakanusha na kutamka wazi kwamba hiyo si kauli ya CDM bali ni ya Mwanachama wake!!

Iwavyo vyovyote, ni pale atakapotokea mwenyekiti mwendawazimu tu ndipo angeweza kukiri kwamba kauli hiyo ni ya chama!! Hivyo basi, sishangai kusikia Mbowe akikanusha!

Picha nyingine ninayopata hapa ni kwamba, hiyo inaweza isiwe kauli ya chama lakini haimaanishi kwamba sio agenda ya chama! Kauli na agenda ni vitu viwili tofauti. Panaweza kuwa na agenda lakini kauli rasmi kuhusu agenda husika ikawa haijatolewa....je, Dogo Janja aliropoka kabla ya wakati muafaka?!

Kuna hii picha nyingine! Inawezekana kabisa kwamba hiyo isiwe kauli wala agenda ya chama....lakini kumbe kuna "wanachama maarufu" wenye agenda ama mawazo kama hayo kwenye mitazamo yao...hili si jambo jema hata kidogo!!

Wengi wanaituhumu CDM na Ukaskazini.....!!! Sina hakika katika hili ingawaje jambo lililo wazi ni kwamba matendo ya CDM yana-reflect tuhuma zinazotolewa dhidi yake!! Kuna harakati za kufa mtu za kuijenga CDM kanda ya Kaskazini lakini harakati hizo hazionekani kwenye maeneo mengine ya nchi hususani pwani na kusini!! Baada ya uchaguzi mkuu 2010, CDM walitangaza kufanya uamsho nchi nzima....inakaribia miaka miwili hivi sasa lakini maeneo wanayozungukia ni yaleyale....!!! Wenyewe wanaita hizo ni strategic areas huku wakitarajia kuchukua nchi kupitia wapiga kura wa ukanda mmoja tu!!!

Mimi ni mtu wa Kusini...CCM imetusaliti na CDM siiamini japo kwa punje ya uwele!! Huwa najiuliza, ikiwa CDM inatutupa mkono wakati wa kuitafuta keki ya taifa, je watatukumbuka wakati imeshapatikana!!!? napata shaka hasa nikikumbuka jinsi ambavyo Dr. Slaa alienda kusini kuomba kura! In few hourz, akapiga kampeni kwenye mikoa miwili....lakini bado wanatushawishi kwamba waliibiwa kura! Kama kuna mtu ninayemuona mjinga kuishabikia CDM basi ni mtu wa kusini unless kama ana nasaba na kaskazini!! Mtanzania mwingine yeyote labda anaweza kuishabikia CDM lakini sio mtu wa kusini!

Kutokana na mwenendo huu wa CDM ndio maana naiangalia kauli ya Dogo Janja kwa jicho la pili...!!

Nas Daz,

..suala ni wananchi wa kusini muamue wenyewe kujiunga na harakati za CDM.

..yaani unataka watoke watu toka maeneo mengine ya Tanzania waje kusini kuwaelekeza na kuwafundisha kwamba mnapaswa kuikataa CCM??

..Why not start ur own movement huko Kusini halafu muunganishe nguvu na CDM,TLP,TPP Maendeleo, baada ya kuona malengo yenu yanafanana?

NB:

..Nassary siyo mtu wa kwanza kutoa kauli za kutaka kujitenga nchi hii.

..kuna wabunge kama Selelii wa CCM amewahi kutoa kauli kama hizo ndani ya bunge.

..pia wako wabunge wa maeneo mengine kama Kigoma, na hata wabunge wa kusini wamewahi kutoa kauli kama hizo.

..msiikuze sana kauli ya Nassary as long as Mwenyekiti wake amemkosoa hapo hapo.
 
Jamani acheni propaganda za kusema CDM haifiki maeneo mengine... mbona tunafika Serengerema, Shinyanga, Mbeya Songea, Dar, Dodoma, Singida, na hata Iringa? tatizo ni kwamba huko tukifika watu wa huko si watu wakutoa update coz labda mitandaohaiko huko au watu hawajahamasika katika kutoa data mitandaoni... Next week tunaelekea Mtwara Lindi, Tandahimba na maeneo mengine ya kusini.. sasa mseme hatifiki huko.. wakati hamtoi update mtandaoni.. Mfano leo Wenje alikuwa Temeke Dar lakini sijui kama hizi update watu wamezipata au lah!
Tatizo ni kupashana habari kunachelewa kuhusu mikutano yetu.....
Tusilaumiane juu ya Arusha..
 
Mkuu Tanganyika ni moja, ila ni maoni ya mleta mada kuwa basi ikiwezekana tujitenge nao....hapa naona alimaanisha kuwa Chadema iko kila mahali, Jamani Tanga hakuna chadema? hapana niliona bendera nyingi tu za chadema wakati naenda Tanga mwanzoni mwa mwaka huu....sawa cuf wapo na chadema wapo? Bagamoyo pia ile barabara ya kwenda sadan national park niliziona njiani, pale mandera niliona chache sana ila nilipofika miono nilikuta kadhaa, tokea hapo nilikuwa nikiuliza maeneo mengina kama eneo linaloitwa kwa mwala, huko wanaishi ndugu zetu wale wamasai wa kikwavi na wanaijua cdm vizuri.

miloko huko mnisahihishe kama kweli bado zipo au ndio kusema tayari "wenyenchi wameshawatisha wana wa nchi"kuwa maendeleo hayatafika wakiikubali cdm.
 
Ali Hassan Mwinyi - Wizara ya Afya Tanzania 1972 mpaka 1975
Ali Hassan Mwinyi - Wizara ya Mali asili na utalii Tanzania 1982 mpaka 1983.

Ahmed Hassan Diria - Wizara ya habari na Utangazaji Tanzania - 1989 mpaka 1990.

Unataka niendelee!!!!

Mkuu wangu Mtanzania punguza nondo wakati mwingine usiwe unatoa majibu mazito kama haya kumbuka kuna vijana wengi humu JF wamejifunzia siasa humu JF.

Historia za siasa za Tanzania zimeanzia Chadema utakapomwambia mambo ya mwaka 1976 ni kumuonea bure kutoka na umri wake.

JF Daima.
 
Last edited by a moderator:
Nasdaz, umeandika maneno mengi badala ya kunyoka kwenye pointi yako......Kuhusu swala la chadema kutokufika kusini ilikuwa ni makubaliano ya chadema na CUF, kuwa CUF kwa kipindi hicho ilikuwa inakubalika sana pwani basi wao wachukue maeno hayo wakiwa na maana kamawakichukua pwani na CHADEMA wakachukua bara basi wange waondoa CCM kiurahisi bahati mbaya sana CUF wamewa sariti chadema, lakini kwasasa chadema inajipanga kuingia mikoa yote ya pwani siku si nyingi....Nimekuwa nikikusoma siku nyingi sana kuna kipindi huwa unaonyesha mahaba na chama cha mapinduzi na kuna wakati huwa neutral sijui ndiyo dalili za kujivua gamba....Karibu sana Chadema

Crashwise,
Labda nikiri jambo....ni wewe pekee am,bae mara kwa mara umekuwa ukikiri udhaifu wa CDM Pwani na Kusini kwa ujumla wake!!
Tuanze na hilo la uswahiba wa muda ambao mliujenga kati yenu na CUF! Sina hakika pangekuwa na utofauti wowote hata kama msingejenga ushoga wa muda! Hapa nimeshawahi kuzungumza...mid 2010 alikuja ndugu yangu wa damu toka bush kwe2(Kusini)! Swali la kwanza kumuuliza ni nguvu ya CDM pale Bush...akanijibu haipo kabisa! Honestly, nilikuwa very disappointed hasa nikizingatia kwamba kile kijiji ni kikubwa sana...kukosekana kwa CDM pale, nikajiuliza wht abt kwenye vijiji vidogo!! Nikauliza kama ameshawahi kuja kiongozi yeyote wa CDM angalau toka mkoani....akajibu haijawahi kutokea!!!! NIKACHOKA!
Kwanini nimekumbushia hayo ambayo kama unanisoma basi unafahamu nimeshawahi kuyaeleza haya....! maana yangu ni kwamba hata kama msingefanya maafikiano na CUF bado msingepata chochote kusini kwavile hamkuwa na base!! Angalau CUF tayari walishakuwa na foundation....and am sure, kama si pale bush kwetu kuwa pua na mdomo na bush kwa Mheshimiwa Membe, basi am certain kwamba CUF wangekuwa wanafanya vizuri pale kwavile walishajenga base! CDM wanachotakiwa si kwenda sehemu wakati wa uchaguzi bali kujenga foundation! Politics is almost like business....popote penye matatizo ni political opportunity against agent wa matatizo husika....sina shaka hili ndilo lilifanya upinzani kushamiri Kigoma! CDM wakakosa kutumia hiyo opportunity kwenye maeneo mengine!

Tukirudi kwenye mahaba na CCM....!!!
Sina mahaba na CCM lakini serikali (sio CCM) inapofanya mazuri, sina bias....nitasema na kushabikia!! Bahati mbaya, nazani ni ngumu kidogo kutofautisha kati ya CCM na serikali lakini mtu akitaka kufanya hivyo, ataweza tu! Na kama watafanya jambo nisilokubaliana nalo, nitasema tu....na hapo ndipo wakati mwingine unapokuja kuniona ni kama Gamba na wakati mwingine Neutral!! Likewise, CDM hawana serikali....hivyo, kama Chama wakifanya jambo ninalohisi sikubaliani nalo, nitasema tu....!!! In short, mie ni bidhaa ambayo haijapata mnunuzi wa kisiasa....Si CCM, CDM wala CUF!!
CCM wameshindwa kuongoza
CDM hawaoneshi nia ya dhati ya kujitanua maeneo mengine ya nchi na hivyo kuonekana ni chama cha kikanda zaidi
CUF...Mdogo wangu ni CUF damu, nilimuuliza kama CUF hawatumii Uislamu ni kwanini mikutano yao (wakati ule wana nguvu) walikuwa wanapenda sana kuifanya Ijumaa?! hakuwa na jibu! Sababu zinazonifanya nisiishabikie CDM ndiyo hiyo hiyo inayonifanya nisiishabikie CUF!
 
Malumbano ya kuwa CDM haiendi mikoa mingine ni potofu. Kwanza huu sio wakati wake.

Kwani Ritz ulikuwa na ratiba ya mikutano ya CDM kwa mwaka huu?
 
kiukweli niseme tu tunashukuru kwa kuliweka hili sawa.cdm mwanzo mwisho
 
Nas Daz,

..suala ni wananchi wa kusini muamue wenyewe kujiunga na harakati za CDM.

..yaani unataka watoke watu toka maeneo mengine ya Tanzania waje kusini kuwaelekeza na kuwafundisha kwamba mnapaswa kuikataa CCM??

..Why not start ur own movement huko Kusini halafu muunganishe nguvu na CDM,TLP,TPP Maendeleo, baada ya kuona malengo yenu yanafanana?

NB:

..Nassary siyo mtu wa kwanza kutoa kauli za kutaka kujitenga nchi hii.

..kuna wabunge kama Selelii wa CCM amewahi kutoa kauli kama hizo ndani ya bunge.

..pia wako wabunge wa maeneo mengine kama Kigoma, na hata wabunge wa kusini wamewahi kutoa kauli kama hizo.

..msiikuze sana kauli ya Nassary as long as Mwenyekiti wake amemkosoa hapo hapo.

You're talking like u're immature in politics....Jokakuu, u're not that immature bana!!! What (assume) kama watu wa huko hawana mwamko?! Should you leave them kwavile hawana mwamko?! come on chuck!
 
Back
Top Bottom