Mkutano wa CHADEMA viwanja vya NMC Arusha

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Mkutano ni saa nane watu wameshanzaa kutia timu ama kweli watu wana usongo...

Picha za awali

=====
IMG_0905.jpg
IMG_0895.jpg
======
View attachment 53517View attachment 53525
View attachment 53518
View attachment 53519
View attachment 53520
View attachment 53521
View attachment 53522View attachment 53524
Baada ya kuona makamanda wanaendelea vema kuripoti yanayoendelea NMC nimeona bpra nishughulie na picha zaidi

Picture 001.jpg
Picture 002.jpg
Peoplesssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssss
Picture 003.jpg
Picture 004.jpg
Picture 005.jpg
Picture 006.jpg Movement For Change - Vua Gamba Vaa Gwanda.....Hakuna kulala mpaka kieleweke...
Heche!! Tunafurahi sana kuwa hapa leo!! Mara ya mwisho kuzungumza hapa ni wakati wa kufukuza madiwani wakorofi!!

Siku zote tulisema na tunaendelea kusema kuwa kwa miaka hamsini CCM imeshindwa kupambana na maadui watatu, tuwasamehe kina Millya kwani wametambua makosa na sasa wamejiunga nasi!!

Vyama vyote vingine vipo kwa maslahi ya chama tawala....

Juzi Kikwete ameteua wabunge na ameteua mwenyekiti wa chama kimoja cha upinzani na leo mnashuhudia watu tuliowasema sana wanjidhiri, tunakwenda Mtwara na Lindi kupokea wanachama kama tunavyofanya hapa!

Watu wanalalamika kuhusu maisha magumu, anavunja baraza la mawaziri 50 na kutengeneza la mawaziri 55, angalia mwandosya hana wizara maalumu na tunamuhudumia kwa kodi zetu hapa..

Sisi tunasema mawaziri walioiba kwa mfano Maige analeta Kiburi cha Chenge!! Anaona millioni mia saba ni kidogo, hii ni ishara ya kutuongezea hasira zaidi..

Moshi mjini Ndesamburo anapokea wenyeviti na mabalozi zaidi ya kumi na nane

Wenje yuko kitunda anaendelea kupokea wanaojiuzulu...

D. Kamara amekataliwa kijijini kwake anapelekwa ubelgiji

Serikali ya kishkaji inaliangamiza Taifa...

Nassari; Mkono mmoja kifuani kumkumbuka m/kiti wetu aliyeuawa!!

Mimi niko Arusha na niko Arumeru, sikupata ubunge sababu ya fedha wala historia ya familia

Nilikuwa DOdoma naibana Serikali na wananchi wa A/mashariki wanabana mafisadi katika ardhi!!

Nimekaa bungeni siku kumi na moja nimeona namna hii nchi inavyoliwa, serikali inamiliki magari ya sh trl 5, bajeti ya serikali ilikuwa trl 11, kwa maaana hiyo nusu ya bajeti ni magari, fedha za maendeleo hazifiki na

Kama wananitishia kuniua nilishakufa toka mwaka juzi!!

Hizi harakati ndio kwanza zimeanza, tuko tayari kufa lakini hatutaacha mpaka kieleweke!!

Kule Sumbawanga jimbo liko wazi mtasikia mziki wake- Heche!!

Mbowe; Pipooooooooooooooooooooz!!

Arusha nawaamini, nataka tupige pipoz pawa mpaka wale tumewakaribisha wajue wameingia katika moto wa gesi!!

Ndg zangu, CDM leo ni chama kinachojiandaa kuchuku Serikali kwa hiyo kila dk kila sekunde ni lazima tuzungumze mambo ya busara!! Nimekuja leo kzungumza mambo machache ya msingi

Umoja wetu kama Taifa, tunapenda makabila yote, dini zote, na watu wa kila aina, vijana wana moto wa gesi lakini inatokana na maudhi ya CCM, Kauli ya Dogo janja ilikuwa kauli ya hamasa..

Tanzania ni moja na tutapigana tukomboe nchi yote na sio nusu ya nchi

Tumekuja kuwapokea wenzetu walio toka CCM, ujio wa hawa watu una nia njema!!


Kwa taarifa, namwambia Nape katika wabunge 200 wa CCM, 70 wameshaomba nafasi!!

Wakichelewa tunafunga safina,

Kikwete katika baraza lako la mawaziri unaloapisha j3, 9 wameshabuku nafasi..

Sasa anayesema CCM ipo ni nani??

Jana Kikwete amevunja katiba mara mbili
Baraza la mawaziri linachaguliwa toka miongoni mwa wabunge, wabunge hawajaapishwa lakini wanakuwa mawaziri!

Tunamsubiri Kikwete Dodoma na Baraza lake la mawazi!! Lituambie limepata wapi madaraka na hao mawaziri wliopewa vyeo bandia tunataka watueleze ni wapi wamepata mamlaka hayo.
 
Makamanda mliopo Arusha kulikoni mbona kima katika hili tunata updates za uko nini kinaendelea mkutano si umeanza saa 4 hii? Tuwekeeni hapa kinachoendelea maeneo hayo.
Mkutano ni saa nane...
 
nasikia James Millya ameachana na uamuzi wake wa kuhamia CDM na amekiomba radhi chama chake cha CCM. na hii ni baada ya Nanyaro kumwambia atakaa benchi kwa muda usiopungua miaka 5 bila hata cheo cha m/kiti wa kata CDM.
 
nasikia James Millya ameachana na uamuzi wake wa kuhamia CDM na amekiomba radhi chama chake cha CCM. na hii ni baada ya Nanyaro kumwambia atakaa benchi kwa muda usiopungua miaka 5 bila hata cheo cha m/kiti wa kata CDM.
Leo tunaanza na UVCCM na UW-Arusha tuna zizika kabisa...
 
nasikia James Millya ameachana na uamuzi wake wa kuhamia CDM na amekiomba radhi chama chake cha CCM. na hii ni baada ya Nanyaro kumwambia atakaa benchi kwa muda usiopungua miaka 5 bila hata cheo cha m/kiti wa kata CDM.
Gamba kazini!:flame:
 
Nimefika hapa uwanjani upepo ukiwa umetulia,baridi kama kawa hapa Arush na watu wameanza kujitokeza ktk mkutano huu uliomahsusi kuzindua mpango uitwao 'VUA GAMBA VAA GWANDA' karibuni sana ktk eneo hili maarufu 'chadema square' 2peane updates..

Shida mnaanzisha thread halafu kuleta updates hamleti mkitegemea wengine wafanye hivyo! Kama huwezi kuleta updates pamoja na picha tafadhali kaa pembeni waachie wenye nia na uwezo wafanye hivyo. Hata thread yenyewe maelezo nusu nusu - hayajitoshelezi. Ungekuwa serious ungetueleza yafuatayo:-

- Muonekano na matayarisho hapo uwanjani kwa ujumla yakoje hadi sasa - bendera za chama, majukwaa, vikundi vya ngoma, dansi, n.k.
- Viongozi gani wanatarajiwa kuwepo kwenye huo mkutano - viongozi wa wilaya, mkoa, taifa, madiwani, wabunge, n.k.
- Viongozi gani mpaka sasa wameshawasili au wako maeneo ya mkutano - viongozi wa wilaya, mkoa, taifa, madiwani, wabunge, n.k.
- Mwitikio na hamasa ikoje - waliovalia mavazi na nembo zingine za chama, gari ya matangazo, vipeperushi, mabango, n.k.
-Jamaa wa intelijensia vipi? Wameshaanza kuranda randa maeneo ya karibu, migari yao ya kuwasha, n.k.
- Ni mambo gani hasa makubwa yanayotarajiwa kujiri katika mkutano wa leo - wengine tunasikia kuna maelfu ya wana-CCM watakaorudisha kadi; Je, ni kweli? n.k.

Halafu, kwa taarifa yako sio "Mpango" ni "Operesheni".
 
Back
Top Bottom