Not so fast...
Kama ungekuwepo uwanjani, ungefikiri upya kuhusu, naamini Sugu kama kweli anabebeka, leo atakuwa amepata onyo kubwa...
Wanafunzi walalamika kulazimishwa kuhudhuria maandamano ya CCM leo
Na Emmanuel Lengwa 16th July 2011
Wanafunzi wa shule za Sangu, Meta na Ivumwe zinazomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi mkoani Mbeya, wamelalamikia hatua ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani hapa kuwalazimisha kuhudhuria maandamano ya chama hicho yanayotarajiwa kufanyika leo jijini Mbeya.
Wakizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa majina yao, wanafunzi hao wamedai kuwa viongozi wa CCM wamekwenda kwenye shule zao na kuwaamuru walimu wawashinikize wanafunzi kuhudhuria maandamano hayo.
Walisema viongozi hao wa CCM wameahidi kuwapelekea magari yatakayowabeba kutoka kwenye shule zao kwenda mahali pa kuanzia maandamano na kisha kuwarejesha shuleni baada ya maandamano kumalizika.
Walisema kitendo hicho cha kuwalazimisha sio kizuri kwa kuwa na wao wanayo hiyari ya kwenda au kutokwenda kwenye maandamano hayo.
"Pamoja na kwamba hizi shule za wazazi zinamilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ambayo ipo chini ya CCM, lakini watambue kuwa na sisi tunazo itikadi zetu za kisiasa ambazo zinapaswa kuheshimiwa," alisema mmoja wa wanafunzi hao.
Mwanafunzi huyo ambaye alionekana kuwa kiongozi wa kundi kubwa la wanafunzi waliofika katika ofisi za gazeti hili kulalamika, alisema wao hawako tayari kuhudhuria maandamano hayo kwa kuwa wanayo kazi moja tu ya kujisomea.
"Wao kama wanataka wanafunzi waongeze idadi ya watu kwenye maandamano yao, wawachukue wale wa O- level, lakini sisi kwanza ni watu wazima wenye maamuzi yetu na pia tunajiandaa na mitihani kwani sisi tunaona kama muda hautututoshi," alisema.
Mwalimu mmoja wa shule ya Sekondari Meta ambaye pia hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alithibitisha kuombwa na viongozi wa CCM ili wawaruhusu wanafunzi wa shule hiyo kuhudhuria maandamano hayo.
"Ni kweli viongozi wa CCM wamefika hapa na kutuomba wanafunzi waende kwenye maandamano yao, kwa kuwa wao ndio wamiliki wa shule hizi na ndio waajiri wetu, sisi hatuna uwezo wa kuwakatalia, lakini pia sioni ubaya wowote kwa wanafunzi kwenda kwenye maandamano hasa ukizingatia kuwa kesho (leo) sio siku ya masomo," alisema.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Verena Shumbusho, alisema suala hilo sio la kwake na kama lipo wanaopaswa kuulizwa ni walimu wa wanafunzi hao au viongozi wa Jumuiya ya Wazazi.
"Hilo mimi halinihusu, kawaulize walimu wao na kama hutaridhika waone viongozi wa Jumuiya ya Wazazi kwa sababu wao ndio wamiliki wa shule hizo," alisema Shumbusho.
Maandamano cha CCM yanayotarajiwa kufanyika leo yamepangwa kuanzia eneo la Mafiati na kuishia viwanya vya Rwandanzovwe.
CHANZO: NIPASHE