hakuna mtu mnafiki kama sitta..kigeu geu sana yule mzee
Kwa ufupi, idadi ya watu ilikuwa kubwa sana, hii ni ishara kuwa CCM yenye uelekeo wa kipiganaji ni tishio kubwa kwa uhai wa Chadema mjini Mbeya.
Yaliyoongelewa kwa ufupi.
MWAKYEMBE:
...Aliahidi kuwa Wabunge wa CCM Mbeya hawataukacha mji wa Mbeya, watautetea na kufanya kila liwezavyo kuleta maendeleo katika mji huu, kwa sababu Mji wa Mbeya ni kioo cha mkoa wa Mbeya.
..Alisikitishwa na kauli za Sugu, kuwaponda Mwandosya, Mwakyusa na yeye, amemponda Sugu kwa kutoshiriki katika harakati za kuupigania mkoa na badala yake kupoteza muda mwingi akizungukazunguka tu kisanii.
...Alimsifu Rais Kikwete na kuwahakikishia wananchi wa mbeya kuwa ana nia ya dhati ya kuibadisha CCM, na kuwa Mafisadi na ufisadi hauna nafasi sasa ndani ya CCM
...Alimkejeli Lowasa (bila kumtaja jina) kuwa maamuzi magumu si ajabu na ata majambazi pia uyafanya kwa kuchukua uamuzi mgumu kuvamia nyumba bila kujua mwenye nyumba ana zana gani ndani, alisema jambo la muhimu zaidi kuliko maamuzi magumu ni maamuzi MAKINI NA SAHIHI, na kuwa CCM iliyojivua gamba siku zote italizingatia hili.
...Aliwahakikishia wananchi wa Mbeya kuwa katika mwaka huu wa fedha, Km 28 za lami zitawekwa mjini Mbeya kwa msaada wa Benki ya Dunia.
MARY MWANJELWA
...Alitangazwa kuwa anafanya kazi sasa kama Mbunge wa Mbeya Mjini, na kupitia uwakilishi wake Serikali ya CCM itatekeleza ilani ya CCM katika mji wa Mbeya.
HILDA NGOWI
...Alikitaja CHADEMA kama chama cha kikanda, na chenye ubaguzi, na kuwa pamoja na Mbeya kuwa mkoa wa pili kwa kumpa kura Dr.Slaa, kura zilizotumika kuteulia Wabunge wa Viti Maalumu, lakini CHADEMA iliwajaza wabunge kutoka Kaskazini na Mkoa wa Mbeya haukupewa ata Mbunge mmoja.
OLE SENDEKA.
...Aliwamasisha sana wananchi kwa kuelezea mwelekeo wa CCM mpya iliyojivua gamba katika kupambana na vitendo vya dhuruma na kujali maslahi ya umma.
...Alisikitishwa na tuhuma za kupika zinazoelekezwa kwa Kikwete na Mtoto wake.
LAZARO NYALANDU.
...Kwa hisia kubwa aliitaja miaka 50 ya uhuru kuwa ni alarm ya kuuanza mwanzo mpya wenye mwelekeo wa kuongeza nguvu zaidi katika kuwaletea wananchi maendeleo.
...Aliahidi kuwa serikali kupitia wizara yake itajizatiti katika kuwaongezea wananchi uwezo wa kipato na kuwa uwanja wa Ndege wa Mbeya utakaokamilika kabla ya December, utatumiwa kama chachu ya kuufungua mkoa wa Mbeya kiuchumi.
...Aliahidi kuwa serikali itawanyang'anya wote waliochukua viwanda vilivyokuwa vya serikali na kushindwa kuviendeleza.
SAMWELI SITTA.
...Kwanza aliwaomba msamaha wa wananchi wa Mbeya kwa niaba ya Serikali ya CCM kwa kuwa kwenye mgawo wa umeme kwani nchi yenye rasilimali kama zetu, haistahili kuwa kwenye matatizo ya umeme.
...Alisema mgawo huu ni matokeo ya vitendo vya kifisadi vilivyokuwa vinalitafuna taifa.
...Alisema CCM iliyojivua gamba, itaitazama mikataba yote ya umeme yenye ishara za kifisadi na kutafuta vyanzo vipya vya umeme, na kuahidi kuwa ndani ya miaka 4 hii kabla ya uchaguzi ujao, tatizo la umeme litakuwa historia.
...Alieleza changamoto ambazo yeye na wapiganaji wengine walikumbana nazo katika kupambana na ufisadi ata kufikia hatua ya kutaka kuvuliwa uanachama wa CCM, ata hivyo alisema kuwa waliamua kupambana ndani ya CCM na matokeo yake sasa yanaonekana.
...Alisikitishwa na kitendo cha vyama vya upinzania ambavyo vilimuomba sana agombee Uraisi kupitia vyama hivyo, leo hii vinamsimanga na kumponda kwa uzalendo wake wa kuusimamia ukweli.
...Alizungumzia kauli yake aliyoitoa Bungeni wiki iliyopita kuhusu unafiki wa Wabunge wa vyama vya upinzani kuhusu posho, na kuahidi kuwa serikali ipo mbioni kuboresha posho za Madktari, Manesi, waalimu n.k ili kuwafanya waboreshe utendani wao wa kazi na kuwa posho zisizo za lazima zitafutwa kama ilivyoainishwa katika mpango kazi wa miaka 5.
...Aliiponda Chadema kuwa bado haina uwezo wa kuongoza nchi, alisema wana viongozi wachache sana wenye uwezo.
NAPE NNAUYE.
...Alifafanua zana nzima ya kujivua gamba, CCM iliyojivua gamba itakuwa na sumu kali zaidi kuiwezesha kupambana vikali zaidi na vitendo vyote vinavyohatarisha maslahi ya umma na kupambana na watendaji wote wa serikali wanaozitumia nafasi zao kujinufaisha.
...Aliahidi kuwa CCM mpya itasimama kwenye misingi ya Mwl Nyerere, na haitalivumilia kundi la wenye pesa kukiodhi chama.
...Aliahidi kuwa CCM iliyojivua gamba kuisimamia Serikali kwa ukaribu katika kuhakikisha kuwa inatekeleza kwa umakini mkataba wa chama na wananchi(ilani ya uchaguzi), kiongozi yeyote wa serikali atakayeshindwa kutekeleza kazi kwa ufanisi hatavumiliwa.
...Alidokeza kuwa kampeni hii ya kujivua gamba sio yake binafsi bali ni ya chama, na kuwa kama ingelikuwa ni yake binafsi, basi wale wanaoshutumiwa wasingeanza kujiondoa wenyewe kama walivyoanza kufanya, amewaahidi wananchi kuwa chama kitawaondoa wale ambao hawatachukua hatua za kujiondoa kwa hiari yao.
...Amemponda Dr.Slaa kwa uchu wake wa madaraka, na kumtaka ayaweke mbele maslahi ya wananchi kuliko uchu wake binafisi.Aliwatahadharisha wananchi kutokubali kutumiwa na watu wachache wenye uchu wa madaraka walio tayari kuwatoa wananchi wauawe au kupata vilema kwa ajili ya maslahi yao ya kisiasa kama ilivyotokea Arusha.
PRINCE MWAIHOJO, MGOMBEA UBUNGE WA CUF 2010.
...Alisikitishwa na kitendo cha Mbunge wa Mbeya kuhamasisha vurugu kwa kauli yake ya kuwataka wananchi wa Mbeya wawapige mawe viongozi wa Serikali,alisema kauli kama hizo hazina maslahi kwa wananchi wa Mbeya na zinapaswa kupingwa na wana Mbeya wote.
...Alihoji uadilifu wa Dr.Slaa kwa kutaka kuingia Ikulu na mke wa mtu.
...Alihojji ufisadi uliopo Chadema katika uteuzi wa viti maalumu, amehoji uhalali wa wabunge wengi wa viti maalumu Chadema kutoka wilaya tatu za Kilimanjaro.