Mkutano wa CCM Kizota, Novemba 11-13, 2012

Mkutano wa CCM Kizota, Novemba 11-13, 2012

Wanaotegemewa kuchaguliwa leo, utaratibu wa zamani ulikuwa ni wagombea wote wa NEC wanapigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu. Utaratibu wa sasa ni kwamba wajumbe wa NEC wanapatikana kwenye ngazi za chini yaani wilayani na kwenye jumuiya za chama ila bado kuna nafasi nyingine za NEC zitapatikana kupitia huu mkutano mkuu wa chama ambazo ni kumi Tanzania bara na kumi kutoka Zanzibar.

Hivyo mchuano mkali uko kwenye hizo nafasi kumi Tanzania bara ambapo kuna wagombea zaidi ya thelathini.

Mkuu Kurunzi, naomba nikupe thanks kwa uzi huu, tangu umeianzisha, tunaelekea post 360, ila hakuna thanks hata moja zaidi ya thanks yangu!. Natoa witu tuwe ni watu wa appreciation on little things ndipo tutakapo weza kushukuru kwa makubwa!

JF bana, thread hii ingekuwa ni kuhusu mkutano mkuu wa baadhi ya vyama, ungeshangaa ma thanks ya kumwaga!.
P.
 
Lakini leo hii kundi la Mkapa na JK wapo pamoja kwa hiyo chochote kinaweza kuwa na ukweli..

hujakosea kwani Mkapa ni mahiri sana kuzua uenyekiti usivuliwe gamba.Ujasiri wake anapokuwa na hoja nzito kwa watu wasiokuwa wamejiandaa kuisikia ndio utazima ghafla mioto itakayowaka ndania ya CCM,JK huwa anaichekea akisubiri izimike yenyewe.
 
Unajua historia yake kwa kina kipi. Na jambo la faida kwako ni lipi. Kama mwalimu akifundisha wanafunzi darasani si jambo lenye faida kwa taifa?

Mswahili anajibu swali kwa swali!!

Mimi nilitaka kufahamu huyo Mangula alilifanyia nini taifa akiwa Katibu Mkuu wa chama kinachoongoza serikali? Jambo ambalo historia itamkumbuka?

Mimi sijaongelea nafasi zake nyingine alizowahi kushika. Tukienda hivyo chifu, CCM na viongozi wake itazidi kuwa uchi.
 
Lakini leo hii kundi la Mkapa na JK wapo pamoja kwa hiyo chochote kinaweza kuwa na ukweli..

Ni kweli na kuungana kwa kundi la JK na BM sio katika mkutano wa leo, Makundi haya yalianza kuungana kuanzia awamu ya pili ya uongozi wa Ben Mkapa. Makundi haya yaliungana yakiwa na maelengo matatu.
1. Kutafuta pesa ya kumtunza Ben akistaafu
2. Kuweka mtu/kundi litakalo mlinda atakapokuwa amestaafu (na Kundi la Mtandao liliomba kazi hii)
3. Kulitafutia pesa kundi la Mtandao kushinda uchaguzi (kumbuka kulikuwa na upinzani mkali sana toka kwa Salim Ahmed na Mwandosya)

Baada ya Makubaliano hayo, Kundi la Mkapa lililokuwa linatawala likaanzisha deal za Meremeta, Deep Green, EPA na kuchota pesa zilizoliwezesha kundi la Mtandao kufanya kampeini na kushinda uchaguzi.

Na Awamu ya Pili ya kundi la Mtandao yaani mwaka 2006 kundi la Mtandao likaanza kutumia mtindo ule ule wa kundi la Mkapa, kuunda miradi hewa ya Richmond, Mikataba ya Gas na Mafuta ili kumtafutia pesa Edward aweze kufanya kampeini na kushinda uchaguzi wa 2015. Kasi yao ya utafutaji pesa imepunguzwa kiasi fulani na kundi la Samweli Sita (akiwa Spika) na CHADEMA wanaoumia nguvu ya Umma. Lakini matokeo yanaonesha kuwa kundi la Edward linatumia viuzri reources lilizosaidiwa kuzikusanya na watawala, kundi la mtandao.
 
Hakuna % wala nini ni kusubiri mzee mtei na vizee vya kichaga vikiamua kwenye vikao vya mbege.

ha ha..wachaga hawana vizee,wana wazee.Vizee vina maeneo yao huko.Huwa vikiongea vinaongea kidhaifu,vinaongea vitu ambavyo si lazima viwe applicable.Wachaga wana wazee wenye command kwa busara,kwa personalities na uzito wa maneno wayasemayo.

vile vizee vya dar vinajulikana.Kwanza ni vichawi,vina njaa,vibasha, vinachunguliana huko uswahili akina mama wakioga and the sort.Sasa kama watu uchawi ndio nguvu yao wataitwaje wazee.

By the way its funny kuwa akina Mtei ndio wataamua hatima ya kina E.L na Membe.
 
Mkuu Kurunzi, naomba nikupe thanks kwa uzi huu, tangu umeianzisha, tunaelekea post 360, ila hakuna thanks hata moja zaidi ya thanks yangu!. Natoa witu tuwe ni watu wa appreciation on little things ndipo tutakapo weza kushukuru kwa makubwa!

JF bana, thread hii ingekuwa ni kuhusu mkutano mkuu wa baadhi ya vyama, ungeshangaa ma thanks ya kumwaga!.
P.

watu wanaogopa kuonekana dhaifu!!
 
Kama nilivyoeleza katika thread yangu niliyoitoa wiki mbili zilizopita ni kuwa kuna Mpambano mkali kati ya Mh Bernard Membe (anaewakilisha Kundi la Wapinga ufisadi) na Mh Edward Lowasa(aliye katika kundi la Mafisadi) katika kuwania kuteuliwa kupeperusha bendera ya Chama chetu mwaka 2015. Matokeo ambayo yamejiri hivi karibuni, kwangu mimi naona hadi sasa Scoreboard inaonyesha Lowasa anaongoza 2-1 na sasa ni Half time.

Lowasa ndie aliyetangulia kupata bao baada ya kumsambaratisha vibaya Membe katika chaguzi za NEC wilaya mbalimbali Tanzania. Katika chaguzi hizo, Lowasa alimtimulia vumbi vilivyo bwana Membe kwa kambi yake kushinda kwa ushindi wa kishindo.

Wakati Membe akishangaashangaa, Lowasa alipiga bao la pili fastafasta baada ya Kundi lake lenye nguvu kubwa ya kifedha kutwaa Jumuia zote za chama ie Wazazi, Vijana na Wanawake na kumwacha Membe akin'gaa macho!

Membe, baada ya vipigo hivyo viwili vitakatifu nae alijufutafuta vumbi na kujipatia bao moja ambapo Mwanachama mzoefu na Mwadilifu na anayeuchukia kwa dhati Ufisadi Mh P. Mangula kuchaguliwa kua Makamu Mwenyekiti wa CCM Tz Bara na wajumbe wa NEC. Kwa hakika kitendo cha kuchaguliwa Mangula ni pigo kubwa kwa kundi la Lowasa kwani Mangula ni mtu anayeichukia rushwa kwa dhati na DAIMA haoni aibu kuweka bayana msimamo wake huo. Mwaka 2005 akiwa Katibu Mkuu wa CCM hakusita kusema katika kamati ya maadili ya chama kua JK na kundi lake la akina Rostam hawafai Urais kutokana na matumizi yasio halali ya pesa ! Kutokana na kitendo hicho ccm ilimpotezea kabisa. Alijaribu kugombea Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa na kugoma kabisa kutoa rushwa na matokeo yake akashindwa na mhuni Sanga aka Jah People. Akagombea NEC na kuhutubia sera za CCM wakati wenzake wakigawa rushwa nako akaishia kukosa! Hivyo, kuchaguliwa kwa Mangula ni pigo kubwa kwa kundi la Lowasa.

Hapa Dodoma kwa sasa, mpambano huu utaendelea kwa nafasi ya Mwenyekiti. Lowasa na kundi lake wanaonekana hawataki J. Kikwete aendelee kua Mwenyekiti kwani wanaona nae ni mmoja kati ya walioshiriki kuharibu nyota ya Lowasa!. Hotuba aliyoitoa Lowasa mwezi Novemba 2011 NEC-Dodoma ambapo alimwaga mboga na ugali kwa pamoja na kumpelekea mwenyekiti mashambulizi makali ambayo Mwenyekiti alishindwa kabisa kuyajibu yanaonyeshafika kambi hiyo isivyo na imani na Mwenyekiti. Aidha,Kitendo cha Bashe, Freddy na Malisa kutapanya mabango mji mzima wa Dodoma kumkataa JK kuendelea kua Mwenyekiti inaonyesha azma hii ya kumkataa Mwenyekiti ambaye upande wa Lowasa unajua fika yuko upande wa Membe. Hivyo JK akichaguliwa tena kuwa mwenyekiti Lowasa atakua kapigwa bao la pili.

Na jambo kubwa na la mwisho linalosubiriwa kwa hamu KUBWA ni kuona kama Membe atafanikiwa kuwemo katika TOP TEN YA NEC. Kundi la Lowasa limetumia "yale mambo yetu" kuwashawishi wajumbe wa NEC kumsabaratisha Membe. Kundi hilo la Lowasa linaamini hiyo ni kazi nyepesi kama kumsukuma mlevi kwani watakaofanya uchaguzi huo wa NEC ni wajumbe wa NEC ambao 90% ndio waliochaguliwa majuzi na wako kundi la Lowasa. Bashe alitamka wazi kwenye press conference kwamba wanafanya kila njia Membe asipite. Katika kuhakikisha wanafanikiwa wameishatayarisha majina KUMI ya watu ambao wanafaa kuingia kumi bora ambapo jina la Membe halimo na wamekua wakiipitisha orodha hiyo kwa wajumbe mbalimbali wa NEC ili Membe atoswe.

Iwapo watafanikiwa hilo, basi huo ndo utakua MWISHO wa hekaheka za Membe kuelekea Ikulu kama vile Sumaye nae alivyoangukia pua na kuishia kulalama tu! Hoja hapa ni kwamba, kwakua chama makini Chadema kinaendelea kuitimulia vumbi CCM kila kukicha hivyo kumpitisha mtu ambaye hata kwenye NEC ya chama chake tu hakubaliki, Watanzania watamkubalije?Kwa upande mwingine, iwapo Membe atashinda litakua ni pigo KUBWA kwa kundi la Lowasa kwa hoja kwamba 90% ya NEC ni wafuasi wa Lowasa, sasa wamewezaje kumchagua Membe?

Yangu macho, hii imekaaje wadau?

Huyo Bashe na Lowassa ndio nyoka ndani ya CCM wenye ndimi mbili, CCM wanatakiwa watafute mtego wa panya na wasitumie fimbo kwani ni mahodari kukwepa!

Hii pesa ya mafisadi iliyofichwa Uswiss itatesa sana bila kujali ni CCM, CDM, CUF, etc
 
1. Kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa Misenyi, Kagera na Kigoma.
2. Kununua meli kubwa zaidi ya MV Bukoba na katika Ziwa Nyasa.
3. Kuzuia hatari ya Kisiwa cha Mazinde, Pangani, kuzama!!
4. Tatizo la umeme kufikia ukomo, mwezi Novemba, 2010.
5. Mtwara na Tanga kuwa miji ya viwanda.
6. Kumpatia kila mwanafunzi kompyuta yenye kuunganishwa na internet.

Kuna uzi mmoja humu wenye kichwa 'ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015', utafute una ahadi zote alizosema.

Aliahidi akiwa na bibi wa kutoka ukanda huo nini?Kama ilivyo kawaida yao ya kuahidi mbingu na nchi hata kwa vitu vinavyokuja warudia sasa anajiabisha.

Wamalawi wanamkumbusha kuwa hiyo meli ingekuwa imewekwa mapema pengine ingeleta confidence zaidi.Bado kuna vitu vingi embarassing.leo anasema kuna nyoka wenye ndimi mbili,sijui aatatuambia na kuna nyoka wenye ndimi moja ktk CCM?
 
1. Kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa Misenyi, Kagera na Kigoma.
2. Kununua meli kubwa zaidi ya MV Bukoba na katika Ziwa Nyasa.
3. Kuzuia hatari ya Kisiwa cha Mazinde, Pangani, kuzama!!
4. Tatizo la umeme kufikia ukomo, mwezi Novemba, 2010.
5. Mtwara na Tanga kuwa miji ya viwanda.
6. Kumpatia kila mwanafunzi kompyuta yenye kuunganishwa na internet.

Kuna uzi mmoja humu wenye kichwa 'ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015', utafute una ahadi zote alizosema.
Nadhani bado ana muda wa kutosha kutekeleza ahadi hizo.....

Anaweza akatekeleza ama kuanza kutekeleza kabla hajaondoka madarakani......Kuna moja ya kujenga Reli kaizungumzia leo, kasema ataanza kuijenga kabla hajaondoka madarakani.....

Tayari miaka miwili imekatika katika miaka yake mitano aliyopewa mwaka 2010......

Katika miaka mitatu iliyobaki kuna uwezekano akatekeleza ahadi hizo ulizotaja hapo juu na nyingine ulizozisahau.......Kama kwenye barabara ,afya na elimu (vyuo) inawezekana kwa nini ishindikane kujenga viwanda Mtwara ama kununua meli ziwa Nyasa na Victoria.....

Nadhani mwaka 2014/2015 utakuwa ni muafaka kumnyooshea kidole kwamba 'hajatekeleza ahadi hii na ile'.........

Bado anao muda wa kutosha kutekeleza ahadi hizo.....
 
85% ya wana Chadema wapo CCM huo ndio ukweli wote kwa pamoja wapo makini kufuatilia kinachoendelea Dodoma.
 
Kujenga barabara za angani ili kumaliza foleni katika jiji la dar es salaam !
Kwenye bajeti ya mwaka huu (kama sikosei) kuna fedha zimetengwa kwa ajili ya flyover eneo la TAZARA......

Nadhani wameanza na TAZARA kwanza.......
 
85% ya wana Chadema wapo CCM huo ndio ukweli wote kwa pamoja wapo makini kufuatilia kinachoendelea Dodoma.
Hapo ndipo naposhindwa mimi kuelewa. Tena wanashauri nani awe kiongozi wa chama na mbora zaidi ya mwingine..
 
Barua aliyomwandikia rais, alisema anastaafu au anajiuzulu?

Nigeria ndiko kulikuwa na tuhuma dhidi yake?

Sikuisoma wala sikuiona hiyo barua.

Nigeria alikwenda kusafisha jina, si ndio mnavyosema au umesahau?
 
tusitegemee kuona mapya katika huu uchaguzi maana ccm ina watu wake ambao siku zote wanafahamika hivyo basi hatushangai kuona sura zilezile zikirudi kwenye hizo nafasi
 
Hapo ndipo naposhindwa mimi kuelewa. Tena wanashauri nani awe kiongozi wa chama na mbora zaidi ya mwingine..

Napata wasiwasi wana Chadema nao wanavutana kweli kweli kuhusu Mangula, wengi wanamsifia na kushangilia...Chadema kitabaki kuwa chama cha upinzani miaka yote. Ikitokea CCM wakampitisha Lowassa kuwa mgombea urais ndio kabisa Chadema itakuwa inaelekea kufa kifo cha kawaida.
 
Hapo ndipo naposhindwa mimi kuelewa. Tena wanashauri nani awe kiongozi wa chama na mbora zaidi ya mwingine..

Kwanza ni vizuri kumjua vizuri mpinzani kwa ajili ya kujenga mikakati.

Bob, utakubaliana na mimi kua nambari one ni CCM!! Inatukera ila bado ni nambari wani
 
Back
Top Bottom