Mkutano wa CCM Jangwani: CCM yafa Rasmi

hivi hiki chama kina mwenyekiti kweli?mbona ni kama hawaelewi wanachokifanya!!!
 
Shukran SEBM kwa kutupa muhtasari, niliongalia mkutano kwa dakika kama 2 basi maana kwa hali ya sasa ni vigumu sana kumsikiliza mwana-CCM unless uwe umekunywa konyagi chupa kadhaa.

Ukisoma taarifa za wadau kuhusu mambo yaliyoongelewa leo na CCM Jangwani unaweza kupata picha moja tu kwamba CCM wanaamini wamefanya mambo mengi mazuri tena mazuri ajabu tangu tupate uhuru! Na leo hii walikuwa na kazi ya kuwakumbusha watanzania ni jinsi gani wameibadilisha hii nchi for the better! Ndio maana tumeskia Wassira akiongea kuhusu utitiri wa shule, mipango ya kujenga viwanda vipya vya sukari, huku Magufuli akiongea kilometa za lami.

Mimi yangu ni machache na ni swali kwa CCM. Tanzania tulipata uhuru katika kipindi kimoja na nchi hizi Singapore na Malaysia (nasema kipindi kimoja kwa sababu ni miaka karibu sawa). Na kati ya hizi nchi naweza kusema ni Tanzania pekee ndiyo yenye rasilimali nyingi kushinda zote. Tuna, Gold, Diamond, Tanzanite, Nickel, Copper, bahari, ardhi nzuri, mito, mbuga za wanyama, milima na mabonde, na sasa Uranium, Natural gas, Oil bila kusahau rasilimali watu. Lakini hebu tuangalie miaka 50 baadae uchumi wa hizi nchi ukoje?

1. Tanzania - USD 23 billion
2. Singapore - USD 208 billion
3. Malaysia - USD 237.8 billion

Sasa ningetaka kujua toka kwa CCM, kwanini Tanzania ni maskini? Kwanini hawa wenzetu wamepiga hatua sisi bado tunaomba vyandarua vya mbu? CCM wanatakiwa wajue watanzania wanauliza swali gani na sio kutoa story za shule za kata. Miaka 50 tuko wapi?
 
Magufuli alitangaza kuwa ameongea kwa muda mrefu na amemaliza muda wake lakini anatambua kuwa kuna watu wanataka kurudisha kadi za CCM (akabadili ghafla na kusema za vyama vingine) waziwasilishe.

Yaani huyu nae roho tayari ishajua haipo CCM, Wamebaki mwili tu.
 
Shukran SEBM kwa kutupa muhtasari, niliongalia mkutano kwa dakika kama 2 basi maana kwa hali ya sasa ni vigumu sana kumsikiliza mwana-CCM unless uwe umekunywa konyagi chupa kadhaa.

Ukisoma taarifa za wadau kuhusu mambo yaliyoongelewa leo na CCM Jangwani unaweza kupata picha moja tu kwamba CCM wanaamini wamefanya mambo mengi mazuri tena mazuri ajabu tangu tupate uhuru! Na leo hii walikuwa na kazi ya kuwakumbusha watanzania ni jinsi gani wameibadilisha hii nchi for the better! Ndio maana tumeskia Wassira akiongea kuhusu utitiri wa shule, mipango ya kujenga viwanda vipya vya sukari, huku Magufuli akiongea kilometa za lami.

Mimi yangu ni machache na ni swali kwa CCM. Tanzania tulipata uhuru katika kipindi kimoja na nchi hizi Singapore na Malaysia (nasema kipindi kimoja kwa sababu ni miaka karibu sawa). Na kati ya hizi nchi naweza kusema ni Tanzania pekee ndiyo yenye rasilimali nyingi kushinda zote. Tuna, Gold, Diamond, Tanzanite, Nickel, Copper, bahari, ardhi nzuri, mito, mbuga za wanyama, milima na mabonde, na sasa Uranium, Natural gas, Oil bila kusahau rasilimali watu. Lakini hebu tuangalie miaka 50 baadae uchumi wa hizi nchi ukoje?

1. Tanzania - USD 23 billion
2. Singapore - USD 208 billion
3. Malaysia - USD 237.8 billion

Sasa ningetaka kujua toka kwa CCM, kwanini Tanzania ni maskini? Kwanini hawa wenzetu wamepiga hatua sisi bado tunaomba vyandarua vya mbu? CCM wanatakiwa wajue watanzania wanauliza swali gani na sio kutoa story za shule za kata. Miaka 50 tuko wapi?

Mkuu FJM,
Juu ya kukua kwa uchumi kwa nchi; John Guninita huku akitokwa na Povu alisema kwamba wapinzani wanatupotosha sana kwa kuwa wao wanatueleza ulinganifu wa uchumi na nchi za mbali.Kwamba, kuna nchi za aina tatu katika uchumi.
1.Nchi za ulimwengu wa Kwanza
2.Nchi za Ulimwengu wa Pili
3.Na nchi za ulimwengu wa Tatu ambazo sisi ndo tunatakiwa tujilinganishe nazo.
Alichosema Guninita ni kwamba, Tanzania hatutakiwi kujilinganisha katika maendeleo ya Uchumi na Ulaya na Japan, kwa kwamba nchi size yetu ni Msumbuji, Kongo, Zambia, Rwanda, Malawi(nashangaa kwa nini hakutaja Kenya na Uganda!).
Lakini wote tunafahamu kwamba hata tukijiweka katika ulinganisho na Malawi, Rwanda au Congo pamoja na ukweli kwamba Tanzania(chini ya Nyerere) iliwasaidia Zambia(Southern Rhodesia), wakati wa Ukoloni na Vita; na pia vita hali mbaya ya Rwanda 1993/1994, hali yetu ni mbaya sana ukilinganisha na mataifa hayo.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Wanabodi,
Usiku huu nimepokea ujumbe mfupi katika simu yangu ya kiganjani unaonekana umetoka CCM na nina unukuu kama ulivyotumwa, "Safari ya CCM kushinda uchaguzi 2015 inaanza leo Jangwani DSM. WanaCCM wote imefika sasa tuseme basi juu ya upotoshaji na propaganda za wapinzani. CCM HAITETEREKI", mwisho wa kunukuu.

My take:-
Kama wao wanaona kuwa watashinda uchaguzi ujao kulikuwa na sababu gani kutumia mitandao ya simu kupenyeza ujumbe kwa jamii? Kwanini wasisubiri uchaguzi uje? Au ndo mfa maji..................? Wanabodi naombeni michango yenu.
 
Magufuli nilitaka ufafanuzi kuhus barabara ya Lamadi-Bariadi kilomita 78 ambapo mkandarasi amesimama baada ya serikali kukosa pesa za kuendelea na kazi. Hii ni kutokana na client "serikali ya magamba" imeishiwa pesa.

Makandarasi wa kichina wanaojenga barabara mbalimbali hapa nchini wanaidai serikali ya ccm au tz takribani sh bilioni 400 . Bajeti ya ujenzi kwa mwaka jana ni bilioni hizo hizo je barabara zitajengwa kweli

kuna madk na maprof waongo kweli kweli......tanzania itaendelea pale ccm watakapo wekwa pembeni basi
 
Afadhali wajiani kwamba watashinda ili wabweteke wakati sisi tunaendelea kutoa elimu ya uraia
 
Mkuu FJM,
Juu ya kukua kwa uchumi kwa nchi; John Guninita huku akitokwa na Povu alisema kwamba wapinzani wanatupotosha sana kwa kuwa wao wanatueleza ulinganifu wa uchumi na nchi za mbali.Kwamba, kuna nchi za aina tatu katika uchumi.
1.Nchi za ulimwengu wa Kwanza
2.Nchi za Ulimwengu wa Pili
3.Na nchi za ulimwengu wa Tatu ambazo sisi ndo tunatakiwa tujilinganishe nazo.
Alichosema Guninita ni kwamba, Tanzania hatutakiwi kujilinganisha katika maendeleo ya Uchumi na Ulaya na Japan, kwa kwamba nchi size yetu ni Msumbuji, Kongo, Zambia, Rwanda, Malawi(nashangaa kwa nini hakutaja Kenya na Uganda!).
Lakini wote tunafahamu kwamba hata tukijiweka katika ulinganisho na Malawi, Rwanda au Congo pamoja na ukweli kwamba Tanzania(chini ya Nyerere) iliwasaidia Zambia(Southern Rhodesia), wakati wa Ukoloni na Vita; na pia vita hali mbaya ya Rwanda 1993/1994, hali yetu ni mbaya sana ukilinganisha na mataifa hayo.

Msumbuji, Kongo, na Rwanda zote hizi zimekuwa kwenye vita kwa miaka mingi. Tanzania tulikuwa na tatizo gani?

Zambia, Malawi, wanataka tulinganishe kwa lipi? kwa rasilimali? kwa ukubwa wa bahari au ardhi? kwa nini hasa?

Tatizo CCM hawataki kukubali ukweli. Watanzania wanataka majibu ya kueleweka na sio kuzungukazuka. Miaka 50 wamefanya nini? Singapore na Malaysia tulikuwa nao, daraja moja, sasa wako daraja la pili, sisi bado kule kule, kwanini?

Kenya uchumi wao ni kama mara mbili ya Tanzania, wanaliona hilo?
 
Hizi ndizo kauli za wasichana wanaobishana sokoni kuhusu mvulana yupi ni mzuri. Na ccm imeishaujua ujinga wa watanzania na ndio maana inawatongoza na inapowapata inawatumia ipasavyo.

Ccm inawahadaa watu kama wewe mithili ya mvulana anayemtafuta msichana!!! Inawatongoza kwa vitisheti vya njano na vikofia vya kijani; Inawapa lifti; inawalisha wali kuku; inawatumbuiza kwa taarabu; inawaahidi maisha bora na kisha inawahonga elfu tano!! Kwa ulaini wananchi wanakubali kufanya mapenzi na ccm. Wanapewa mimba, wanazaa ufukara na kisha wanatelekezwa kwa maisha duni!Nionavyo mimi: Watanzania wakiteseka na mazingaombwe ya ugumu wa maisha ni sawa tu!! Ni haki yao!! Waendelee tu kutaabika kwa kuwa dhiki, mahangaiko na ufukara wanavitaka wenyewe!!

Mkuu uko sahihi kabisa!! Haya yote yanatutokea kwa sababu ya uvivu wetu wa kufikiri na kuchukua hatua!! Sasa acha tule kazi ya mikono yetu! Hadi siku hiyo tutakayo amua kuzinduka!!!
 
Nilikuwa makini sana kuangalia waliokuwa wanarudisha 'kadi za ccm or vyama vingine'. Nilichokiona ni kukosekana ushawishi wa kimazingira kufanya umma uamini igizo lile.

Nilichogundua toka kwa viongozi na wapambe wa ccm ni WOGA uliopita mipaka dhidi ya CHADEMA. Wanaongea wakitetemeka kwa hofu, wanajua mwisho wao umefika. Tusubiri tuone jinsi hizo ziara zao zitakavyo backfire. Ingizo jipya la bajeti linakuja soon, watazidi kuchanganyikiwa.
 
Mkutano wa CCM Jangwani: CCM yafa Rasmi
UTANGULIZI

Wote tulisikia kwenye vyombo mbalimbali vya habari juu ya uwepo wa mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwaniulioitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ukiwa na maudhui ya Kutoa Msimamo Wake Juu ya Masuala Yanayogusa Mustakabali wa Taifa hususan katika maeneo makubwa matatu.

(a) Hatma ya Maisha ya Watanzania Katika ajira, miundombinu, Reli, Barabara, umeme, bei ya bidhaa, raslimali n.k)
(b) Mchakatowa Katiba na
(c) Vurugu za Zanzibar

Mkutano huu uliotegemewa kuwa na watu wengi; kwa kweli ulihudhuriwa na maelfu ya wanachamana wafuasi wa CCM ambao wengi wao waliletwa na mabasi, malori n.k. MWANZO WA MKUTANO Kabla ya kufunguliwa mkutano rasmi, kulikuwepo na utambulisho wa viongozi mbali mbali waCCM ambao walitoa salamu zao.

Awali walielezea kwamba ule haukuwa mkutano wa mipasho, bali ulilenga kuwaambia wananchi wa CCM nini kimefanywa na Serikali ya CCM katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Miongoni mwa kauli tata zilizojitokeza ni;-

- CCM kusifiwa kwa kuwa na wanachama wa aina mbali mbali ya watu (makundi yote) tofauti ya vyama vingine vinavyowagawa watu kidini na kikabila (Kaongea mama mmoja nimesahau jina lake)
- Wananchi kuwaogopa wapinzani wanaozunguka nchi nzima kueneza sera zao kwa kuwa haowamefadhiliwa na wazungu/wabebari ambao wana nia ya kuja kuchukua rasilimalizetu (Mwingulu Nchemba).

- Mbunge mmoja alisema wanataka Jamhuri ya Kaskazini na baada ya muda Mbowe akasema alikosea kusema hiyo kauli. Lakini sisi tunasema kuwa mtoto akikosea au akisema jambo basi katumwa na Baba yake na hivyo Mbunge huyo alitumwa na Baba yake – Mbowe (John Guninita)

HOJA ZA MAWAZIRI
Waliandaliwa mawaziri mbalimbali ambao uwepo wao ulilenga kuhakikisha wanatoa majibu kwa wananchi ya nini kimefanywa na serikali ya CCM kwa 2010 – 2015.

Mawaziri hawa ni wasomi wenye sifa za Uprofesa (Tibaijuka, Maghembe) na Madaktari (Mwakyembe na Magufuli) na mwingine sijui elimu yale ( Wassira).

(1) Prof. Jumanne Maghembe

Ni Waziri mwenye dhamana ya Maji. Hakuna la maana alilozungumza hususan utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa 2010 – 2015 zaidi ya kutoa maelezo ya ‘mipango’ ya serikali na wizara yake katika kuleta maji Dar Es Salaam. Muda mwingi aliutumia kuzungumza ‘cubic meter’ za maji zitakazofika Kimara, visima anavyodhamiria kufungua 15/07/2012, na kwamba katika bajeti ya 2012/2013 kutengwa kwa hela (hajazitaja, maana bajeti haijapita, anyway) ka ajili ya kuimarisha upatikanaji wa maji.

(2) Steven Masatu Wassira
Ni waziri mwenye dhamana ya Uratibu na Mahusiano. Alianza mkutano wake kwa kuwafahamisha wananchi kuwa alikuwa anamwakilisha Rais Masetu, Lesotho na baadaye kupanda ndege Johanesburg na kuwahi mkutano Jangwani.

Baadaye akazungumzia juu ya sababu mbali mbali zinazoleta ugumu wa maisha kwa wananchi:

- Uchumi; hali inasababishwa na kuyumba kwa hali ya uchumi duniani.

-Chakula; kwamba Tanzania kama nchi inalima sana na eneo lake kubwa (56%) linatumika kwa kilimo na hivyo nchi majirani za Kenya, Uganda, South Sudan huja Tanzania kubeba chakula karibu chote na hivyo Tanzania kutokuwa na chakula.

- Kupanda kwa bidhaa za mafuta kunatokana na vita inayoendelea huko Iran na Mataifa ya Magharibi.

- Uhaba/gharama ya sukari ; unasababishwana kuwepo kwa viwanda vichache vya sukari (alimaanisha TPC, Kagera, Mtibwa, Kilombero)na hivyo serikali inajenga viwanda vitano zaidi (hakusema kama 100% vitamilikiwa na serikali au vitakuwa tena vya makaburu, wa-madagascar n.k)

- Umeme; hali ya matatizo ya mvua na hivyo mpango unafanyika kujenga mitambo ya gesi asilia kutoka Mtwara –Dar.

Alimalizia wasilisho lake kwakusema kuwa kuna shule nyingi sana na ukilinganisha zamani na sasa; kuna vyuo vikuu vingi na kulikuwa na chuo kikuu chenye wanafunzi 14 wa Sheria pale Lumumba. [ukweli ni kuwa, University of East Africa (Makerere) katika kuhakikisha inapanuka, ilianzisha tawi Tanzania na wanafunzi walikuwa pale Ushirika na walikuwa wanalala Kigamboni wakati kunajengwa UDSM]

(3) Profesa Tibaijuka: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

- Kimsingi sikujua hata alichokuwa anakielezea pale jukwaani zaidi ya kuzungumza kuwa alifika Dar 1970 na yeye ni Mwalimu wa UDSM (Economics) na kuwa alikuwa NJE ambako baada ya kuchuma (alimaanisha mali, ila akaja na kusema kuchuma Ujuzi) alirudi Tanzania.

- Alisema tu kuwa kero za Ardhi Kigamboni na Kurasini zinafahamika na watazifanyia kazi; na kwenye bajeti ya 2012/2013 wametenga fedha kwa ajili ya mipango mingi ya maendeleo.

- Zaidi pia alisema juu ya ujio wa Mji wa Kisasa wa Kigamboni utakaofanana na Dubai na Bahrain na kwamba wananchi waendelee kumpatia kero zao na kuwa kulipa pango kwamiezi 12 ni batili na uhalali ni kulipa kwa miezi 3 tu.

(4) Dr. Harisson Mwakyembe: Waziri wa Uchukuzi.

- Nadhani hakuwa anajua Ilani ya CCM inasemaje au pia hakujua yuko mkutanoni pale kufanya nini, maana alianza kuzungumzia kuhusu Wapinzani kuelezea MADUDU YALIYOBAINIWA NA CAG na kwamba Mamlaka makubwa kapewa CAG na Rais (sikuelewa uhusiano!).

- Zaidi ya kuzungumza juu ya kutozwa nauli ya 1,500 Tegeta; na nauli za Kimara na kutoa namba yake ya simu (0782 24 25 26) ili tumpigie na kumpa kero kwakuwa ‘ana simu kubwa’ hakuna la maana alilozungumza.

- Kauli zake nyingi ni zilezile za ‘mipango’ ya kufanya hiki na kile: kuwa na treni Ubungo Maziwa mpaka Stesheni; kufufua TAZARA, kusafisha Bandari. Alimalizia kwa kusema ‘ TUPENI MUDA TUNAYAFANYIA KAZI MATATIZO YENU’

(5) Dr. John Magufuli: Waziriwa Miundo Mbinu.

- Pamoja na kwamba tangu awali nilitegema kusikia idadi yakilometa za lami zinazojengwa na majina ya makampuni, sikutegemea kufahamu kuwa kipaji chake kingine ni kufahamu lugha mbali mbali za Kitanzania.

- Aliendelea tu kutaja kilometa za Lami zinazowekwa huku akitoa ulinganisho wa kilometer za lami tangu uhuru (6,500) hadi sasa (11,154) tofauti la kauli ya awali ya Wassira kuwa uhuru kulikuwa na barabara 3 tu (Dar – Moro. Hii naijua ina kama 200kms; Tanga - Korogwe ; kama 101kms na Arusha – Moshi; kama 90kms.)

- Alizungumza pia kuwa bajeti hii ya 2012/2013 imepanga kutekeleza miradi mingi ya maendeleo ya barabara. Labda tukio la kusisimua ni kuwa, wakati akiwa anaendelea kuongea (huku ikijionyesha dhahiri kuna kitu anakisubiria), Magufuli alitangaza kuwa ameongea kwa muda mrefu na amemaliza muda wake lakini anatambua kuwa kuna watu wanataka kurudisha kadi za CCM (akabadili ghafla na kusema za vyama vingine) waziwasilishe.

Katika hali ya kushangaza, waliibuka watu wa umri mmoja (vijana wa kike na kiume wa umri wa miaka 28 – 33), na ambao walionekana wakiwa wanafahamiana kabla (au kukaa pamoja kabla), na waliokuwa wakicheza wimbo mmojakwa umahiri walirudisha kadi. Kadi hazikuonekana na wala hawakujitokeza katika kuzungumza kwa nini ‘walihama huko walikotoka’ na kujiunga na CCM.

HITIMISHO

- Lazima nikiri, kwa kusikia na kutazama yaliyosemwa na CCM katika mkutano wao leo, ni dhahiri kuwa CCM imefikia mwisho wake kwa kuwa imeshindwa kuwapa majibu sahihi watanzania juu ya shida zao na namna serikali ya CCM ilivyoweza kuwakwamua wananchi na mipango yake thabiti ijayo katika kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa.

- Pamoja na kuwa Kinana alikuja kuelezea kuwa mada nyingine mbili (Katiba na Zanzibar) zitawasilishwa na Kamati/Halmashauri kuu kwaKamati ya Warioba, lakini ukweli ni kuwa walikosa majibu ya kuridhisha.

- Mwanzoni walisema hawako pale kujibu hoja za vyama vingine au kuweka mipasho, lakini kauli zao zilijidhihirisha kuwa hawakuwa na la maana la kusema/kuwaambia wananchi (mfano, salamu ya ‘vyama vingine vidogo’ hoyee, ya Magufuli, Mbowe arudi kuuza Pombe n.k)

- Kimsingi ni kama vile tulikuwa kwenye mkutano wa kampeni, kusikiliza ahadi za nini chama kitafanya na wala si nini kimefanywa na serikali ndani ya 2010 – 2015.

- Walichokifanya mawaziri hawa, wasomi, ni upotezaji wa muda wa wananchi na upotevu wa rasilimali za Taifa kwani wangeweza kuongea waliyoongoea kwa kuwaambia tu manaibu waziri wao wazungumze na wahariri au wazee wa Dar Es Salaam na si kama walivyofanya.

CCM Imejivua nguo rasmi leo; CCM Imekufa Rasmi
 
Well said.
UTANGULIZI

Wote tulisikia kwenye vyombo mbalimbali vya habari juu ya uwepo wa mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwaniulioitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ukiwa na maudhui ya Kutoa Msimamo Wake Juu ya Masuala Yanayogusa Mustakabali wa Taifa hususan katika maeneo makubwa matatu:

(a) Hatma ya Maisha ya Watanzania Katika ajira, miundombinu, Reli, Barabara, umeme, bei ya bidhaa, raslimali n.k)
(b) Mchakato wa Katiba na
(c) Vurugu za Zanzibar

Mkutano huu uliotegemewa kuwa na watu wengi; kwa kweli ulihudhuriwa na maelfu ya wanachamana wafuasi wa CCM ambao wengi wao waliletwa na mabasi, malori n.k. MWANZO WA MKUTANO Kabla ya kufunguliwa mkutano rasmi, kulikuwepo na utambulisho wa viongozi mbali mbali waCCM ambao walitoa salamu zao.

Awali walielezea kwamba ule haukuwa mkutano wa mipasho, bali ulilenga kuwaambia wananchi wa CCM nini kimefanywa na Serikali ya CCM katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Miongoni mwa kauli tata zilizojitokeza ni;-

- CCM kusifiwa kwa kuwa na wanachama wa aina mbali mbali ya watu (makundi yote) tofauti ya vyama vingine vinavyowagawa watu kidini na kikabila (Kaongea mama mmoja nimesahau jina lake)
- Wananchi kuwaogopa wapinzani wanaozunguka nchi nzima kueneza sera zao kwa kuwa haowamefadhiliwa na wazungu/wabebari ambao wana nia ya kuja kuchukua rasilimalizetu (Mwingulu Nchemba).
- Mbunge mmoja alisema wanataka Jamhuri ya Kaskazini na baada ya muda Mbowe akasema alikosea kusema hiyo kauli. Lakini sisi tunasema kuwa mtoto akikosea au akisema jambo basi katumwa na Baba yake na hivyo Mbunge huyo alitumwa na Baba yake – Mbowe (John Guninita)

HOJA ZA MAWAZIRI
Waliandaliwa mawaziri mbalimbali ambao uwepo wao ulilenga kuhakikisha wanatoa majibu kwa wananchi ya nini kimefanywa na serikali ya CCM kwa 2010 – 2015.

Mawaziri hawa ni wasomi wenye sifa za Uprofesa (Tibaijuka, Maghembe) na Madaktari (Mwakyembe na Magufuli) na mwingine sijui elimu yale ( Wassira).

(1) Prof. Jumanne Maghembe
Ni Waziri mwenye dhamana ya Maji.

- Hakuna la maana alilozungumza hususan utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa 2010 – 2015 zaidi ya kutoa maelezo ya ‘mipango’ ya serikali na wizara yake katika kuleta maji Dar Es Salaam. Muda mwingi aliutumia kuzungumza ‘cubic meter’ za maji zitakazofika Kimara, visima anavyodhamiria kufungua 15/07/2012, na kwamba katika bajeti ya 2012/2013 kutengwa kwa hela (hajazitaja, maana bajeti haijapita, anyway) ka ajili ya kuimarisha upatikanaji wa maji.

(2) Steven Masatu Wassira
Ni waziri mwenye dhamana ya Uratibu na Mahusiano.

- Alianza mkutano wake kwa kuwafahamisha wananchi kuwa alikuwa anamwakilisha Rais Masetu, Lesotho na baadaye kupanda ndege Johanesburg na kuwahi mkutano Jangwani.

- Baadaye akazungumzia juu ya sababu mbali mbali zinazoleta ugumu wa maisha kwa wananchi:

- Uchumi; hali inasababishwa na kuyumba kwa hali ya uchumi duniani.

- Chakula; kwamba Tanzania kama nchi inalima sana na eneo lake kubwa (56%) linatumika kwa kilimo na hivyo nchi majirani za Kenya, Uganda, South Sudan huja Tanzania kubeba chakula karibu chote na hivyo Tanzania kutokuwa na chakula.

- Kupanda kwa bidhaa za mafuta kunatokana na vita inayoendelea huko Iran na Mataifa ya Magharibi.

- Uhaba/gharama ya sukari ; unasababishwana kuwepo kwa viwanda vichache vya sukari (alimaanisha TPC, Kagera, Mtibwa, Kilombero)na hivyo serikali inajenga viwanda vitano zaidi (hakusema kama 100% vitamilikiwa na serikali au vitakuwa tena vya makaburu, wa-madagascar n.k)

- Umeme; hali ya matatizo ya mvua na hivyo mpango unafanyika kujenga mitambo ya gesi asilia kutoka Mtwara –Dar.

Alimalizia wasilisho lake kwakusema kuwa kuna shule nyingi sana na ukilinganisha zamani na sasa; kuna vyuo vikuu vingi na kulikuwa na chuo kikuu chenye wanafunzi 14 wa Sheria pale Lumumba. [ukweli ni kuwa, University of East Africa (Makerere) katika kuhakikisha inapanuka, ilianzisha tawi Tanzania na wanafunzi walikuwa pale Ushirika na walikuwa wanalala Kigamboni wakati kunajengwa UDSM]

(3) Profesa Tibaijuka: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

- Kimsingi sikujua hata alichokuwa anakielezea pale jukwaani zaidi ya kuzungumza kuwa alifika Dar 1970 na yeye ni Mwalimu wa UDSM (Economics) na kuwa alikuwa NJE ambako baada ya kuchuma (alimaanisha mali, ila akaja na kusema kuchuma Ujuzi) alirudi Tanzania.

- Alisema tu kuwa kero za Ardhi Kigamboni na Kurasini zinafahamika na watazifanyia kazi; na kwenye bajeti ya 2012/2013 wametenga fedha kwa ajili ya mipango mingi ya maendeleo.

- Zaidi pia alisema juu ya ujio wa Mji wa Kisasa wa Kigamboni utakaofanana na Dubai na Bahrain na kwamba wananchi waendelee kumpatia kero zao na kuwa kulipa pango kwamiezi 12 ni batili na uhalali ni kulipa kwa miezi 3 tu.

(4) Dr. Harisson Mwakyembe: Waziri wa Uchukuzi.

- Nadhani hakuwa anajua Ilani ya CCM inasemaje au pia hakujua yuko mkutanoni pale kufanya nini, maana alianza kuzungumzia kuhusu Wapinzani kuelezea MADUDU YALIYOBAINIWA NA CAG na kwamba Mamlaka makubwa kapewa CAG na Rais (sikuelewa uhusiano!).

- Zaidi ya kuzungumza juu ya kutozwa nauli ya 1,500 Tegeta; na nauli za Kimara na kutoa namba yake ya simu (0782 24 25 26) ili tumpigie na kumpa kero kwakuwa ‘ana simu kubwa’ hakuna la maana alilozungumza.

- Kauli zake nyingi ni zilezile za ‘mipango’ ya kufanya hiki na kile: kuwa na treni Ubungo Maziwa mpaka Stesheni; kufufua TAZARA, kusafisha Bandari. Alimalizia kwa kusema ‘ TUPENI MUDA TUNAYAFANYIA KAZI MATATIZO YENU’

(5) Dr. John Magufuli: Waziriwa Miundo Mbinu.

- Pamoja na kwamba tangu awali nilitegema kusikia idadi yakilometa za lami zinazojengwa na majina ya makampuni, sikutegemea kufahamu kuwa kipaji chake kingine ni kufahamu lugha mbali mbali za Kitanzania.

- Aliendelea tu kutaja kilometa za Lami zinazowekwa huku akitoa ulinganisho wa kilometer za lami tangu uhuru (6,500) hadi sasa (11,154) tofauti la kauli ya awali ya Wassira kuwa uhuru kulikuwa na barabara 3 tu (Dar – Moro. Hii naijua ina kama 200kms; Tanga - Korogwe ; kama 101kms na Arusha – Moshi; kama 90kms.)

- Alizungumza pia kuwa bajeti hii ya 2012/2013 imepanga kutekeleza miradi mingi ya maendeleo ya barabara. Labda tukio la kusisimua ni kuwa, wakati akiwa anaendelea kuongea (huku ikijionyesha dhahiri kuna kitu anakisubiria), Magufuli alitangaza kuwa ameongea kwa muda mrefu na amemaliza muda wake lakini anatambua kuwa kuna watu wanataka kurudisha kadi za CCM (akabadili ghafla na kusema za vyama vingine) waziwasilishe.

Katika hali ya kushangaza, waliibuka watu wa umri mmoja (vijana wa kike na kiume wa umri wa miaka 28 – 33), na ambao walionekana wakiwa wanafahamiana kabla (au kukaa pamoja kabla), na waliokuwa wakicheza wimbo mmojakwa umahiri walirudisha kadi. Kadi hazikuonekana na wala hawakujitokeza katika kuzungumza kwa nini ‘walihama huko walikotoka’ na kujiunga na CCM.

HITIMISHO

- Lazima nikiri, kwa kusikia na kutazama yaliyosemwa na CCM katika mkutano wao leo, ni dhahiri kuwa CCM imefikia mwisho wake kwa kuwa imeshindwa kuwapa majibu sahihi watanzania juu ya shida zao na namna serikali ya CCM ilivyoweza kuwakwamua wananchi na mipango yake thabiti ijayo katika kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa.

- Pamoja na kuwa Kinana alikuja kuelezea kuwa mada nyingine mbili (Katiba na Zanzibar) zitawasilishwa na Kamati/Halmashauri kuu kwaKamati ya Warioba, lakini ukweli ni kuwa walikosa majibu ya kuridhisha.

- Mwanzoni walisema hawako pale kujibu hoja za vyama vingine au kuweka mipasho, lakini kauli zao zilijidhihirisha kuwa hawakuwa na la maana la kusema/kuwaambia wananchi (mfano, salamu ya ‘vyama vingine vidogo’ hoyee, ya Magufuli, Mbowe arudi kuuza Pombe, CCM wataweka lami na CHADEMA waandamane kwenye hizo lami n.k)

- Kimsingi ni kama vile tulikuwa kwenye mkutano wa kampeni, kusikiliza ahadi za nini chama kitafanya na wala si nini kimefanywa na serikali ndani ya 2010 – 2015.

- Walichokifanya mawaziri hawa, wasomi, ni upotezaji wa muda wa wananchi na upotevu wa rasilimali za Taifa kwani wangeweza kuongea waliyoongoea kwa kuwaambia tu manaibu waziri wao wazungumze na wahariri au wazee wa Dar Es Salaam na si kama walivyofanya.

CCM Imejivua nguo rasmi leo; CCM Imekufa Rasmi
 
Msumbuji, Kongo, na Rwanda zote hizi zimekuwa kwenye vita kwa miaka mingi. Tanzania tulikuwa na tatizo gani?

Zambia, Malawi, wanataka tulinganishe kwa lipi? kwa rasilimali? kwa ukubwa wa bahari au ardhi? kwa nini hasa?

Tatizo CCM hawataki kukubali ukweli. Watanzania wanataka majibu ya kueleweka na sio kuzungukazuka. Miaka 50 wamefanya nini? Singapore na Malaysia tulikuwa nao, daraja moja, sasa wako daraja la pili, sisi bado kule kule, kwanini?

Kenya uchumi wao ni kama mara mbili ya Tanzania, wanaliona hilo?

Ongezea na hili:-

Miaka hiyo ya uhuru uchumi wa Tanzania ulikuwa juu kuliko wa KOREA KUSINI, leo ni sawa na Mbingu na kuzimu. Magamba ndo wametufikisha hapa!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Linyungu usishange hao mawaziri kupiga porojo. CCM wamekurupuka kuonesha kama bado wapo...hawakujiandaa na huu mkutano, umekuja ghafla mno kwao. Kwa sasa CCM ipo kwenye wakati mgumu,ndani ya chama kuna mgogoro wa kuvuana gamba.Kule serikalini wameshaonyesha uzadhaifu wa kuongoza. Nje Chadema wanawapeleka puta. Kule "site" wanachama wao wanarudisha kadi kwa hiari yao wenyewe.CCM inakufa.
 
Ongezea na hili:-

Miaka hiyo ya uhuru uchumi wa Tanzania ulikuwa juu kuliko wa KOREA KUSINI, leo ni sawa na Mbingu na kuzimu. Magamba ndo wametufikisha hapa!

Anko Sam, mpaka kufikia mwaka 2010 GDP ya Korea Kusini ilikuwa USD 1.01 trillion, narudia USD 1.01 trillion. sisi tuko kwenye 23 billion! Huu ni uhaini.
 
Ama kwa hakika kumekuwa na upotoshaji mkubwa ktk mkutano wa leo hususani kwa wale wasioitakia mema CCM.Nikianza na huyu bwana alie leta mada hii,yeye binafsi amejalibukutoa baadhi ya maelezo ambayo kimsingi si ya kweli;mfano mojawapo ni kuhusu suala la wanachama kuletwa kwa magari,sasa nalo hili linahitaji propagana:hivi hata kama ni wewe ukihitaji leo kuelekea ktk mkutano wa CDM KUSIN hivi hautapanda GARI?Je,watu wakutafsiri kuwa umehongwa na cdm.Hapa swala la msingi NI KULETA HOJA ZENYE MSINGI. HALAFU WEWE NA CHAMA CHAKO MKUWA NA TABIA YA KUBATIZA MAJINA VIWANJA VYOTE MNAVYO FANYIA MIKUTANO YENU.HIVI HAMUON HAYA HATA KIDOGO
 
Acha upotoshaji wakati mwingine si lazima sana kuchambua mambo ya CCM, ambayo ni dhahiri yapo nje ya uwezo wako, ukweli ni kwamba umeupindisha ukweli na umepotosha kwa kiasi kikubwa yale yaliyozungumza kwenye Mkutano wa leo.
Tujuze wewe uliyoyasikia!
 
Back
Top Bottom