Mkutano wa CCM Jangwani: CCM yafa Rasmi

Mkutano wa CCM Jangwani: CCM yafa Rasmi

UTANGULIZI

Wote tulisikia kwenye vyombo mbalimbali vya habari juu ya uwepo wa mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwaniulioitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ukiwa na maudhui ya Kutoa Msimamo Wake Juu ya Masuala Yanayogusa Mustakabali wa Taifa hususan katika maeneo makubwa matatu:

(a) Hatma ya Maisha ya Watanzania Katika ajira, miundombinu, Reli, Barabara, umeme, bei ya bidhaa, raslimali n.k)
(b) Mchakato wa Katiba na
(c) Vurugu za Zanzibar

Mkutano huu uliotegemewa kuwa na watu wengi; kwa kweli ulihudhuriwa na maelfu ya wanachamana wafuasi wa CCM ambao wengi wao waliletwa na mabasi, malori n.k. MWANZO WA MKUTANO Kabla ya kufunguliwa mkutano rasmi, kulikuwepo na utambulisho wa viongozi mbali mbali waCCM ambao walitoa salamu zao.

Awali walielezea kwamba ule haukuwa mkutano wa mipasho, bali ulilenga kuwaambia wananchi wa CCM nini kimefanywa na Serikali ya CCM katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Miongoni mwa kauli tata zilizojitokeza ni;-

- CCM kusifiwa kwa kuwa na wanachama wa aina mbali mbali ya watu (makundi yote) tofauti ya vyama vingine vinavyowagawa watu kidini na kikabila (Kaongea mama mmoja nimesahau jina lake)
- Wananchi kuwaogopa wapinzani wanaozunguka nchi nzima kueneza sera zao kwa kuwa haowamefadhiliwa na wazungu/wabebari ambao wana nia ya kuja kuchukua rasilimalizetu (Mwingulu Nchemba).
- Mbunge mmoja alisema wanataka Jamhuri ya Kaskazini na baada ya muda Mbowe akasema alikosea kusema hiyo kauli. Lakini sisi tunasema kuwa mtoto akikosea au akisema jambo basi katumwa na Baba yake na hivyo Mbunge huyo alitumwa na Baba yake – Mbowe (John Guninita)

HOJA ZA MAWAZIRI
Waliandaliwa mawaziri mbalimbali ambao uwepo wao ulilenga kuhakikisha wanatoa majibu kwa wananchi ya nini kimefanywa na serikali ya CCM kwa 2010 – 2015.

Mawaziri hawa ni wasomi wenye sifa za Uprofesa (Tibaijuka, Maghembe) na Madaktari (Mwakyembe na Magufuli) na mwingine sijui elimu yale ( Wassira).

(1) Prof. Jumanne Maghembe
Ni Waziri mwenye dhamana ya Maji.

- Hakuna la maana alilozungumza hususan utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa 2010 – 2015 zaidi ya kutoa maelezo ya ‘mipango’ ya serikali na wizara yake katika kuleta maji Dar Es Salaam. Muda mwingi aliutumia kuzungumza ‘cubic meter’ za maji zitakazofika Kimara, visima anavyodhamiria kufungua 15/07/2012, na kwamba katika bajeti ya 2012/2013 kutengwa kwa hela (hajazitaja, maana bajeti haijapita, anyway) ka ajili ya kuimarisha upatikanaji wa maji.

(2) Steven Masatu Wassira
Ni waziri mwenye dhamana ya Uratibu na Mahusiano.

- Alianza mkutano wake kwa kuwafahamisha wananchi kuwa alikuwa anamwakilisha Rais Masetu, Lesotho na baadaye kupanda ndege Johanesburg na kuwahi mkutano Jangwani.

- Baadaye akazungumzia juu ya sababu mbali mbali zinazoleta ugumu wa maisha kwa wananchi:

- Uchumi; hali inasababishwa na kuyumba kwa hali ya uchumi duniani.

- Chakula; kwamba Tanzania kama nchi inalima sana na eneo lake kubwa (56%) linatumika kwa kilimo na hivyo nchi majirani za Kenya, Uganda, South Sudan huja Tanzania kubeba chakula karibu chote na hivyo Tanzania kutokuwa na chakula.

- Kupanda kwa bidhaa za mafuta kunatokana na vita inayoendelea huko Iran na Mataifa ya Magharibi.

- Uhaba/gharama ya sukari ; unasababishwana kuwepo kwa viwanda vichache vya sukari (alimaanisha TPC, Kagera, Mtibwa, Kilombero)na hivyo serikali inajenga viwanda vitano zaidi (hakusema kama 100% vitamilikiwa na serikali au vitakuwa tena vya makaburu, wa-madagascar n.k)

- Umeme; hali ya matatizo ya mvua na hivyo mpango unafanyika kujenga mitambo ya gesi asilia kutoka Mtwara –Dar.

Alimalizia wasilisho lake kwakusema kuwa kuna shule nyingi sana na ukilinganisha zamani na sasa; kuna vyuo vikuu vingi na kulikuwa na chuo kikuu chenye wanafunzi 14 wa Sheria pale Lumumba. [ukweli ni kuwa, University of East Africa (Makerere) katika kuhakikisha inapanuka, ilianzisha tawi Tanzania na wanafunzi walikuwa pale Ushirika na walikuwa wanalala Kigamboni wakati kunajengwa UDSM]

(3) Profesa Tibaijuka: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

- Kimsingi sikujua hata alichokuwa anakielezea pale jukwaani zaidi ya kuzungumza kuwa alifika Dar 1970 na yeye ni Mwalimu wa UDSM (Economics) na kuwa alikuwa NJE ambako baada ya kuchuma (alimaanisha mali, ila akaja na kusema kuchuma Ujuzi) alirudi Tanzania.

- Alisema tu kuwa kero za Ardhi Kigamboni na Kurasini zinafahamika na watazifanyia kazi; na kwenye bajeti ya 2012/2013 wametenga fedha kwa ajili ya mipango mingi ya maendeleo.

- Zaidi pia alisema juu ya ujio wa Mji wa Kisasa wa Kigamboni utakaofanana na Dubai na Bahrain na kwamba wananchi waendelee kumpatia kero zao na kuwa kulipa pango kwamiezi 12 ni batili na uhalali ni kulipa kwa miezi 3 tu.

(4) Dr. Harisson Mwakyembe: Waziri wa Uchukuzi.

- Nadhani hakuwa anajua Ilani ya CCM inasemaje au pia hakujua yuko mkutanoni pale kufanya nini, maana alianza kuzungumzia kuhusu Wapinzani kuelezea MADUDU YALIYOBAINIWA NA CAG na kwamba Mamlaka makubwa kapewa CAG na Rais (sikuelewa uhusiano!).

- Zaidi ya kuzungumza juu ya kutozwa nauli ya 1,500 Tegeta; na nauli za Kimara na kutoa namba yake ya simu (0782 24 25 26) ili tumpigie na kumpa kero kwakuwa ‘ana simu kubwa’ hakuna la maana alilozungumza.

- Kauli zake nyingi ni zilezile za ‘mipango’ ya kufanya hiki na kile: kuwa na treni Ubungo Maziwa mpaka Stesheni; kufufua TAZARA, kusafisha Bandari. Alimalizia kwa kusema ‘ TUPENI MUDA TUNAYAFANYIA KAZI MATATIZO YENU’

(5) Dr. John Magufuli: Waziriwa Miundo Mbinu.

- Pamoja na kwamba tangu awali nilitegema kusikia idadi yakilometa za lami zinazojengwa na majina ya makampuni, sikutegemea kufahamu kuwa kipaji chake kingine ni kufahamu lugha mbali mbali za Kitanzania.

- Aliendelea tu kutaja kilometa za Lami zinazowekwa huku akitoa ulinganisho wa kilometer za lami tangu uhuru (6,500) hadi sasa (11,154) tofauti la kauli ya awali ya Wassira kuwa uhuru kulikuwa na barabara 3 tu (Dar – Moro. Hii naijua ina kama 200kms; Tanga - Korogwe ; kama 101kms na Arusha – Moshi; kama 90kms.)

- Alizungumza pia kuwa bajeti hii ya 2012/2013 imepanga kutekeleza miradi mingi ya maendeleo ya barabara. Labda tukio la kusisimua ni kuwa, wakati akiwa anaendelea kuongea (huku ikijionyesha dhahiri kuna kitu anakisubiria), Magufuli alitangaza kuwa ameongea kwa muda mrefu na amemaliza muda wake lakini anatambua kuwa kuna watu wanataka kurudisha kadi za CCM (akabadili ghafla na kusema za vyama vingine) waziwasilishe.

Katika hali ya kushangaza, waliibuka watu wa umri mmoja (vijana wa kike na kiume wa umri wa miaka 28 – 33), na ambao walionekana wakiwa wanafahamiana kabla (au kukaa pamoja kabla), na waliokuwa wakicheza wimbo mmojakwa umahiri walirudisha kadi. Kadi hazikuonekana na wala hawakujitokeza katika kuzungumza kwa nini ‘walihama huko walikotoka’ na kujiunga na CCM.

HITIMISHO

- Lazima nikiri, kwa kusikia na kutazama yaliyosemwa na CCM katika mkutano wao leo, ni dhahiri kuwa CCM imefikia mwisho wake kwa kuwa imeshindwa kuwapa majibu sahihi watanzania juu ya shida zao na namna serikali ya CCM ilivyoweza kuwakwamua wananchi na mipango yake thabiti ijayo katika kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa.

- Pamoja na kuwa Kinana alikuja kuelezea kuwa mada nyingine mbili (Katiba na Zanzibar) zitawasilishwa na Kamati/Halmashauri kuu kwaKamati ya Warioba, lakini ukweli ni kuwa walikosa majibu ya kuridhisha.

- Mwanzoni walisema hawako pale kujibu hoja za vyama vingine au kuweka mipasho, lakini kauli zao zilijidhihirisha kuwa hawakuwa na la maana la kusema/kuwaambia wananchi (mfano, salamu ya ‘vyama vingine vidogo’ hoyee, ya Magufuli, Mbowe arudi kuuza Pombe, CCM wataweka lami na CHADEMA waandamane kwenye hizo lami n.k)

- Kimsingi ni kama vile tulikuwa kwenye mkutano wa kampeni, kusikiliza ahadi za nini chama kitafanya na wala si nini kimefanywa na serikali ndani ya 2010 – 2015.

- Walichokifanya mawaziri hawa, wasomi, ni upotezaji wa muda wa wananchi na upotevu wa rasilimali za Taifa kwani wangeweza kuongea waliyoongoea kwa kuwaambia tu manaibu waziri wao wazungumze na wahariri au wazee wa Dar Es Salaam na si kama walivyofanya.

CCM Imejivua nguo rasmi leo; CCM Imekufa Rasmi

He heeeeee Leo cdm mmeshikwa pabaya sana, kila mtu anaweweseka na ofisi Leo makao makuu hamkufungua, hakuna la maana hapo kwenye thread zaidi ya craaaaap kajisaidie ulale mkuu
 
Pale palikuwa na tafrija ya kumpokea Wassira eti katokea South. Ama kweli wao wana Hela sisi tuna Mungu.
 
Kwa Idadi ya Mawaziri waliokuwepo pale uwanjani nilitaraji muda usingetosha lakini cha ajabu chama changu hakina hoja ya kuwaeleza wananchi muda ukatosha mpaka Chege akapata nafasi ya kumtambulisha Kikwete kwa vijana, naamini ulikuwa wimbo sahihi kwa kuwa vijana wengi hawa mjui kikwete kwa sasa wengi wana wajua Mbowe, Slaa, Zitto, Lema na Mnyika kwa kuwa wanawasemea kila uchwao

Nilisikitika kuona chama changu kinatoa ahadi kana kwamba kiko katika kampeni kumbe ilikuwa wakati muafaka wa kuwaeleza wananchi wametekelezaje mkataba wao na wananchi, nimesikitika kuona hazina ya chama zimeshindwa tumika ipasavyo.

Naamini haukuwa wakati muafaka kwetu kufanya mkutano ule, ni weweseko wa M4C na Umati uliokusanywa pale na CDM ki ukweli CCM wameshindwa kujibu mapigo.

Mniambie gwanda ni shillingi ngapi na ninatakiwa kufanya nini nami nijiunge na timu ya wakombozi nimegundua CCM hakuna jipya, hatuna uwezo wa kujibu hoja za CDM waliojaa matumaini ya watanzania
 
Kumbe mbwembwe zote ilikuwa kuigopa cdm maana hakuna chama kingine cha upinzani kilichotajwa zaidi ya cdm na vp khs katiba mbona hawajazungumzia
 
Tutawaadhibu muda si mrefu, kila chenye mwanzo kina mwisho wake na huu ndiyo mwisho wao. Unajua hata mtu akikwambia unakufa hautakubali kirahisi mpaka umauti ukukute' so nyinyiemu subirini mtaona hiki tunachowaambia kama ni kweli au si kweli.
 
Kwa Idadi ya Mawaziri waliokuwepo pale uwanjani nilitaraji muda usingetosha lakini cha ajabu chama changu hakina hoja ya kuwaeleza wananchi muda ukatosha mpaka Chege akapata nafasi ya kumtambulisha Kikwete kwa vijana, naamini ulikuwa wimbo sahihi kwa kuwa vijana wengi hawa mjui kikwete kwa sasa wengi wana wajua Mbowe, Slaa, Zitto, Lema na Mnyika kwa kuwa wanawasemea kila uchwao

Nilisikitika kuona chama changu kinatoa ahadi kana kwamba kiko katika kampeni kumbe ilikuwa wakati muafaka wa kuwaeleza wananchi wametekelezaje mkataba wao na wananchi, nimesikitika kuona hazina ya chama zimeshindwa tumika ipasavyo.

Naamini haukuwa wakati muafaka kwetu kufanya mkutano ule, ni weweseko wa M4C na Umati uliokusanywa pale na CDM ki ukweli CCM wameshindwa kujibu mapigo.

Mniambie gwanda ni shillingi ngapi na ninatakiwa kufanya nini nami nijiunge na timu ya wakombozi nimegundua CCM hakuna jipya, hatuna uwezo wa kujibu hoja za CDM waliojaa matumaini ya watanzania

Kweli Leo na wasiwasi lazima nguo za ndani haziko sawasawa, poleee mkuu ndio demokrasia ccm hawatawafanya vibaya tena km leo, na hapo ni nape tu against all cdm bado mnalalamika
 
Comrade usitegemee chochote cha maana toka CCM labda kama uko tayari kuusikia ujinga Lakini naimani wamepata jibu la swali lao kwa nini pale pameitwa CDM Square
 
Dr mwakyembe kasema kazi ni KULINDANA 2, Unahitaji akili ya kiwenda wazimu kuzungumzia utekelezaji wa sera za ccm, ambako kila FISADI analindwa, Majizi yana nguvu ya kuangusha serikali.
 
Kweli Leo na wasiwasi lazima nguo za ndani haziko sawasawa, poleee mkuu ndio demokrasia ccm hawatawafanya vibaya tena km leo, na hapo ni nape tu against all cdm bado mnalalamika
We ni mwanaume bwana kama Nape anakufurumusha ni huko huko hatuwezi kukubaliana na ujinga wa Na
attachment.php
pe na CCM,njaa mbya zawadi yako hiyo
 
Ahsante mleta mada maana wengine hata huo muda wa kuangalia chama cha kisanii hatukuwa nao leo, nami nasema wananchi hatutaki porojo za majukwaani ,tunataka bajeti ijayo ishushe gharama za mafuta,vyakula,nauli,umeme,maji,mawasiliano,elimu,afya ,uchumi wa mtanzania upande,kima cha chini mshahara kitosheleze mahitaji na mengine.Mambo ya kipuuzi tumechoka watu badala ya kuongelea maisha yetu mnaongelea chadema basi ipisheni chadema iongoze.Tunashuhudia namna ccm inavyouza nchi eti watanzania wanahitaji lishe bora itakayozalishwa na makabaila ni ujinga mtupu.Tumechoka kuonewa ,kunyanyaswa na kupuuzwa na watawala tunataka haki,madini yetu,maliasili yetu vyote mmegawa kwa interest zenu,subirini yaliyyotokea zimbamwe muone sio kazi kuuza nchi.DaWA YENU CCM IPO JIKONI mnafulahi watu wanauana kwa kukosa maeneo ya mifugo na kilimo,mnawaondoa watu kwenye ardhi nzuri ili muwape wawezekaji wezi,hatutakubali! Tunaipenda Tanzania yetu,ni bora kuendelea kuwa maskini kuliko kuruhusu nchi yetu kuuzwa,CCM BE CAREFUL WANANCHI TUMECHOKAAAAAAAAA!
 
Barabara ya jangwani inajengwa ili uandamane kwenye lami, upo hapo !
Munaiba mpaka midomo munaweweseka duuh CCM kwishiney Kodi zetu munajidai fedha za baba yenu ,wezi wakubwa
attachment.php
mpaka kadi za kufoji mukishindwa kuishi mjini rudini vijiji munaweza kufungwa kwa ushahidi huu hapa
 
UTANGULIZI

Wote tulisikia kwenye vyombo mbalimbali vya habari juu ya uwepo wa mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwaniulioitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ukiwa na maudhui ya Kutoa Msimamo Wake Juu ya Masuala Yanayogusa Mustakabali wa Taifa hususan katika maeneo makubwa matatu:

(a) Hatma ya Maisha ya Watanzania Katika ajira, miundombinu, Reli, Barabara, umeme, bei ya bidhaa, raslimali n.k)
(b) Mchakato wa Katiba na
(c) Vurugu za Zanzibar

Mkutano huu uliotegemewa kuwa na watu wengi; kwa kweli ulihudhuriwa na maelfu ya wanachamana wafuasi wa CCM ambao wengi wao waliletwa na mabasi, malori n.k. MWANZO WA MKUTANO Kabla ya kufunguliwa mkutano rasmi, kulikuwepo na utambulisho wa viongozi mbali mbali waCCM ambao walitoa salamu zao.

Awali walielezea kwamba ule haukuwa mkutano wa mipasho, bali ulilenga kuwaambia wananchi wa CCM nini kimefanywa na Serikali ya CCM katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Miongoni mwa kauli tata zilizojitokeza ni;-

- CCM kusifiwa kwa kuwa na wanachama wa aina mbali mbali ya watu (makundi yote) tofauti ya vyama vingine vinavyowagawa watu kidini na kikabila (Kaongea mama mmoja nimesahau jina lake)
- Wananchi kuwaogopa wapinzani wanaozunguka nchi nzima kueneza sera zao kwa kuwa haowamefadhiliwa na wazungu/wabebari ambao wana nia ya kuja kuchukua rasilimalizetu (Mwingulu Nchemba).
- Mbunge mmoja alisema wanataka Jamhuri ya Kaskazini na baada ya muda Mbowe akasema alikosea kusema hiyo kauli. Lakini sisi tunasema kuwa mtoto akikosea au akisema jambo basi katumwa na Baba yake na hivyo Mbunge huyo alitumwa na Baba yake – Mbowe (John Guninita)

HOJA ZA MAWAZIRI
Waliandaliwa mawaziri mbalimbali ambao uwepo wao ulilenga kuhakikisha wanatoa majibu kwa wananchi ya nini kimefanywa na serikali ya CCM kwa 2010 – 2015.

Mawaziri hawa ni wasomi wenye sifa za Uprofesa (Tibaijuka, Maghembe) na Madaktari (Mwakyembe na Magufuli) na mwingine sijui elimu yale ( Wassira).

(1) Prof. Jumanne Maghembe
Ni Waziri mwenye dhamana ya Maji.

- Hakuna la maana alilozungumza hususan utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa 2010 – 2015 zaidi ya kutoa maelezo ya ‘mipango’ ya serikali na wizara yake katika kuleta maji Dar Es Salaam. Muda mwingi aliutumia kuzungumza ‘cubic meter’ za maji zitakazofika Kimara, visima anavyodhamiria kufungua 15/07/2012, na kwamba katika bajeti ya 2012/2013 kutengwa kwa hela (hajazitaja, maana bajeti haijapita, anyway) ka ajili ya kuimarisha upatikanaji wa maji.

(2) Steven Masatu Wassira
Ni waziri mwenye dhamana ya Uratibu na Mahusiano.

- Alianza mkutano wake kwa kuwafahamisha wananchi kuwa alikuwa anamwakilisha Rais Masetu, Lesotho na baadaye kupanda ndege Johanesburg na kuwahi mkutano Jangwani.

- Baadaye akazungumzia juu ya sababu mbali mbali zinazoleta ugumu wa maisha kwa wananchi:

- Uchumi; hali inasababishwa na kuyumba kwa hali ya uchumi duniani.

- Chakula; kwamba Tanzania kama nchi inalima sana na eneo lake kubwa (56%) linatumika kwa kilimo na hivyo nchi majirani za Kenya, Uganda, South Sudan huja Tanzania kubeba chakula karibu chote na hivyo Tanzania kutokuwa na chakula.

- Kupanda kwa bidhaa za mafuta kunatokana na vita inayoendelea huko Iran na Mataifa ya Magharibi.

- Uhaba/gharama ya sukari ; unasababishwana kuwepo kwa viwanda vichache vya sukari (alimaanisha TPC, Kagera, Mtibwa, Kilombero)na hivyo serikali inajenga viwanda vitano zaidi (hakusema kama 100% vitamilikiwa na serikali au vitakuwa tena vya makaburu, wa-madagascar n.k)

- Umeme; hali ya matatizo ya mvua na hivyo mpango unafanyika kujenga mitambo ya gesi asilia kutoka Mtwara –Dar.

Alimalizia wasilisho lake kwakusema kuwa kuna shule nyingi sana na ukilinganisha zamani na sasa; kuna vyuo vikuu vingi na kulikuwa na chuo kikuu chenye wanafunzi 14 wa Sheria pale Lumumba. [ukweli ni kuwa, University of East Africa (Makerere) katika kuhakikisha inapanuka, ilianzisha tawi Tanzania na wanafunzi walikuwa pale Ushirika na walikuwa wanalala Kigamboni wakati kunajengwa UDSM]

(3) Profesa Tibaijuka: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

- Kimsingi sikujua hata alichokuwa anakielezea pale jukwaani zaidi ya kuzungumza kuwa alifika Dar 1970 na yeye ni Mwalimu wa UDSM (Economics) na kuwa alikuwa NJE ambako baada ya kuchuma (alimaanisha mali, ila akaja na kusema kuchuma Ujuzi) alirudi Tanzania.

- Alisema tu kuwa kero za Ardhi Kigamboni na Kurasini zinafahamika na watazifanyia kazi; na kwenye bajeti ya 2012/2013 wametenga fedha kwa ajili ya mipango mingi ya maendeleo.

- Zaidi pia alisema juu ya ujio wa Mji wa Kisasa wa Kigamboni utakaofanana na Dubai na Bahrain na kwamba wananchi waendelee kumpatia kero zao na kuwa kulipa pango kwamiezi 12 ni batili na uhalali ni kulipa kwa miezi 3 tu.

(4) Dr. Harisson Mwakyembe: Waziri wa Uchukuzi.

- Nadhani hakuwa anajua Ilani ya CCM inasemaje au pia hakujua yuko mkutanoni pale kufanya nini, maana alianza kuzungumzia kuhusu Wapinzani kuelezea MADUDU YALIYOBAINIWA NA CAG na kwamba Mamlaka makubwa kapewa CAG na Rais (sikuelewa uhusiano!).

- Zaidi ya kuzungumza juu ya kutozwa nauli ya 1,500 Tegeta; na nauli za Kimara na kutoa namba yake ya simu (0782 24 25 26) ili tumpigie na kumpa kero kwakuwa ‘ana simu kubwa’ hakuna la maana alilozungumza.

- Kauli zake nyingi ni zilezile za ‘mipango’ ya kufanya hiki na kile: kuwa na treni Ubungo Maziwa mpaka Stesheni; kufufua TAZARA, kusafisha Bandari. Alimalizia kwa kusema ‘ TUPENI MUDA TUNAYAFANYIA KAZI MATATIZO YENU’

(5) Dr. John Magufuli: Waziriwa Miundo Mbinu.

- Pamoja na kwamba tangu awali nilitegema kusikia idadi yakilometa za lami zinazojengwa na majina ya makampuni, sikutegemea kufahamu kuwa kipaji chake kingine ni kufahamu lugha mbali mbali za Kitanzania.

- Aliendelea tu kutaja kilometa za Lami zinazowekwa huku akitoa ulinganisho wa kilometer za lami tangu uhuru (6,500) hadi sasa (11,154) tofauti la kauli ya awali ya Wassira kuwa uhuru kulikuwa na barabara 3 tu (Dar – Moro. Hii naijua ina kama 200kms; Tanga - Korogwe ; kama 101kms na Arusha – Moshi; kama 90kms.)

- Alizungumza pia kuwa bajeti hii ya 2012/2013 imepanga kutekeleza miradi mingi ya maendeleo ya barabara. Labda tukio la kusisimua ni kuwa, wakati akiwa anaendelea kuongea (huku ikijionyesha dhahiri kuna kitu anakisubiria), Magufuli alitangaza kuwa ameongea kwa muda mrefu na amemaliza muda wake lakini anatambua kuwa kuna watu wanataka kurudisha kadi za CCM (akabadili ghafla na kusema za vyama vingine) waziwasilishe.

Katika hali ya kushangaza, waliibuka watu wa umri mmoja (vijana wa kike na kiume wa umri wa miaka 28 – 33), na ambao walionekana wakiwa wanafahamiana kabla (au kukaa pamoja kabla), na waliokuwa wakicheza wimbo mmojakwa umahiri walirudisha kadi. Kadi hazikuonekana na wala hawakujitokeza katika kuzungumza kwa nini ‘walihama huko walikotoka’ na kujiunga na CCM.

HITIMISHO

- Lazima nikiri, kwa kusikia na kutazama yaliyosemwa na CCM katika mkutano wao leo, ni dhahiri kuwa CCM imefikia mwisho wake kwa kuwa imeshindwa kuwapa majibu sahihi watanzania juu ya shida zao na namna serikali ya CCM ilivyoweza kuwakwamua wananchi na mipango yake thabiti ijayo katika kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa.

- Pamoja na kuwa Kinana alikuja kuelezea kuwa mada nyingine mbili (Katiba na Zanzibar) zitawasilishwa na Kamati/Halmashauri kuu kwaKamati ya Warioba, lakini ukweli ni kuwa walikosa majibu ya kuridhisha.

- Mwanzoni walisema hawako pale kujibu hoja za vyama vingine au kuweka mipasho, lakini kauli zao zilijidhihirisha kuwa hawakuwa na la maana la kusema/kuwaambia wananchi (mfano, salamu ya ‘vyama vingine vidogo’ hoyee, ya Magufuli, Mbowe arudi kuuza Pombe, CCM wataweka lami na CHADEMA waandamane kwenye hizo lami n.k)

- Kimsingi ni kama vile tulikuwa kwenye mkutano wa kampeni, kusikiliza ahadi za nini chama kitafanya na wala si nini kimefanywa na serikali ndani ya 2010 – 2015.

- Walichokifanya mawaziri hawa, wasomi, ni upotezaji wa muda wa wananchi na upotevu wa rasilimali za Taifa kwani wangeweza kuongea waliyoongoea kwa kuwaambia tu manaibu waziri wao wazungumze na wahariri au wazee wa Dar Es Salaam na si kama walivyofanya.

CCM Imejivua nguo rasmi leo; CCM Imekufa Rasmi

Mkuu pole na kazi kubwa lakini nakupongeza sana maana umeifanya kwa muda mfupi na kwa umakini sana. Asante kwa kujali wana jf
 
Watanzania tunahitaji zaidi matendo kuliko siasa.Ahadi tumezisikia tangu uhuru!
 
Munaiba mpaka midomo munaweweseka duuh CCM kwishiney Kodi zetu munajidai fedha za baba yenu ,wezi wakubwa
attachment.php
mpaka kadi za kufoji mukishindwa kuishi mjini rudini vijiji munaweza kufungwa kwa ushahidi huu hapa

Ha ha haaaa mkuu umeandika lugha gani hapo? Hujaeleweka hata Chembe Rudi kwenu rwanda
 
Acha upotoshaji wakati mwingine si lazima sana kuchambua mambo ya CCM, ambayo ni dhahiri yapo nje ya uwezo wako, ukweli ni kwamba umeupindisha ukweli na umepotosha kwa kiasi kikubwa yale yaliyozungumza kwenye Mkutano wa leo.

Njoo na kilichozungumzwa ku-counter hiki kilichowekwa! Tunakufuatilia utujulishe ukweli
 
We ni mwanaume bwana kama Nape anakufurumusha ni huko huko hatuwezi kukubaliana na ujinga wa Na
attachment.php
pe na CCM,njaa mbya zawadi yako hiyo

Hizo kadi zote faki. Kadi gani ya mwanachama isiyokuwa na picha ya mwanachama wala Muhuri wa Chama? zingine sijui waliziokota! jinsi zilivyochanika haioneshi kama hata zimewahi kuwa za mwanachama wa chama alie hai maana hata hivyo hazina picha wala muhuri.
 
Du! Dactari wa sheria mh. Mw..ky..ebe kaingia wizarani kwa kasi na hata kwenye mkutano wa leo tumemwona na kumsikia lakini akumbuke kwa kasi hiyo ndani ya nyinyiem hatafika mbali.Wangapi wamekwama? Kama hajui akamwulize Lyt..nga. Labda aje huku CDM.
 
Leo magamba walikuwa na mkutano jangwani baadhi ya mambo yaliyojiri:
-Watu kusombwa na mafuso pamoja na mabus kama kawaida
-Nilishuhudia vijana waliokuwa waliokuwa wanazichapa kwa kugombania pesa waliopewa
-Walikuwa wanauza Tshirt zilizoandikwa `CHANA GWANDA NA GAMBA , VAA UZALENDO`
 
Mkuu SEBM,

Umesahau ishu moja ya msingi kabla ya kutangaza kifo cha CCM.

- Leo wamejitokeza wanawake wengi kuliko ule mkutano wa CHADEMA. In fact CHADEMA wanawake walikuwa ni kama hawapo kabisa. Hii ni nguzo muhimu sana ya uhai wa chama.

- Na kwenye taarifa ya mtandao wa chama wanasema wana matawi kama 600 Dar es Salaam, na wanachama/wakereketwa 400,000. Sina uhakika na numbers, lakini ni kweli kuwa CCM bado wana mtandao mkubwa wa matawi.

Nilidhani madhumuni ya mkutano ule ni kueleza nini wamefanya, kumbe ilikuwa kuonesha uhai wa matawi ya wanawake! Sioni uhusiano wa hilo na kilichotarajiwa kwa mujibu wa matangazo. Tambueni wengine humu tunafuatilia issues sio ushabiki wa kisiasa
 
Back
Top Bottom