Mkutano wa CCM Jangwani: CCM yafa Rasmi

SEBM

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
495
195
UTANGULIZI

Wote tulisikia kwenye vyombo mbalimbali vya habari juu ya uwepo wa mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwaniulioitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ukiwa na maudhui ya Kutoa Msimamo Wake Juu ya Masuala Yanayogusa Mustakabali wa Taifa hususan katika maeneo makubwa matatu:

(a) Hatma ya Maisha ya Watanzania Katika ajira, miundombinu, Reli, Barabara, umeme, bei ya bidhaa, raslimali n.k)
(b) Mchakato wa Katiba na
(c) Vurugu za Zanzibar

Mkutano huu uliotegemewa kuwa na watu wengi; kwa kweli ulihudhuriwa na maelfu ya wanachamana wafuasi wa CCM ambao wengi wao waliletwa na mabasi, malori n.k. MWANZO WA MKUTANO Kabla ya kufunguliwa mkutano rasmi, kulikuwepo na utambulisho wa viongozi mbali mbali waCCM ambao walitoa salamu zao.

Awali walielezea kwamba ule haukuwa mkutano wa mipasho, bali ulilenga kuwaambia wananchi wa CCM nini kimefanywa na Serikali ya CCM katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Miongoni mwa kauli tata zilizojitokeza ni;-

- CCM kusifiwa kwa kuwa na wanachama wa aina mbali mbali ya watu (makundi yote) tofauti ya vyama vingine vinavyowagawa watu kidini na kikabila (Kaongea mama mmoja nimesahau jina lake)
- Wananchi kuwaogopa wapinzani wanaozunguka nchi nzima kueneza sera zao kwa kuwa haowamefadhiliwa na wazungu/wabebari ambao wana nia ya kuja kuchukua rasilimalizetu (Mwingulu Nchemba).
- Mbunge mmoja alisema wanataka Jamhuri ya Kaskazini na baada ya muda Mbowe akasema alikosea kusema hiyo kauli. Lakini sisi tunasema kuwa mtoto akikosea au akisema jambo basi katumwa na Baba yake na hivyo Mbunge huyo alitumwa na Baba yake – Mbowe (John Guninita)

HOJA ZA MAWAZIRI
Waliandaliwa mawaziri mbalimbali ambao uwepo wao ulilenga kuhakikisha wanatoa majibu kwa wananchi ya nini kimefanywa na serikali ya CCM kwa 2010 – 2015.

Mawaziri hawa ni wasomi wenye sifa za Uprofesa (Tibaijuka, Maghembe) na Madaktari (Mwakyembe na Magufuli) na mwingine sijui elimu yale ( Wassira).

(1) Prof. Jumanne Maghembe
Ni Waziri mwenye dhamana ya Maji.

- Hakuna la maana alilozungumza hususan utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa 2010 – 2015 zaidi ya kutoa maelezo ya ‘mipango' ya serikali na wizara yake katika kuleta maji Dar Es Salaam. Muda mwingi aliutumia kuzungumza ‘cubic meter' za maji zitakazofika Kimara, visima anavyodhamiria kufungua 15/07/2012, na kwamba katika bajeti ya 2012/2013 kutengwa kwa hela (hajazitaja, maana bajeti haijapita, anyway) ka ajili ya kuimarisha upatikanaji wa maji.

(2) Steven Masatu Wassira
Ni waziri mwenye dhamana ya Uratibu na Mahusiano.

- Alianza mkutano wake kwa kuwafahamisha wananchi kuwa alikuwa anamwakilisha Rais Masetu, Lesotho na baadaye kupanda ndege Johanesburg na kuwahi mkutano Jangwani.

- Baadaye akazungumzia juu ya sababu mbali mbali zinazoleta ugumu wa maisha kwa wananchi:

- Uchumi; hali inasababishwa na kuyumba kwa hali ya uchumi duniani.

- Chakula; kwamba Tanzania kama nchi inalima sana na eneo lake kubwa (56%) linatumika kwa kilimo na hivyo nchi majirani za Kenya, Uganda, South Sudan huja Tanzania kubeba chakula karibu chote na hivyo Tanzania kutokuwa na chakula.

- Kupanda kwa bidhaa za mafuta kunatokana na vita inayoendelea huko Iran na Mataifa ya Magharibi.

- Uhaba/gharama ya sukari ; unasababishwana kuwepo kwa viwanda vichache vya sukari (alimaanisha TPC, Kagera, Mtibwa, Kilombero)na hivyo serikali inajenga viwanda vitano zaidi (hakusema kama 100% vitamilikiwa na serikali au vitakuwa tena vya makaburu, wa-madagascar n.k)

- Umeme; hali ya matatizo ya mvua na hivyo mpango unafanyika kujenga mitambo ya gesi asilia kutoka Mtwara –Dar.

Alimalizia wasilisho lake kwakusema kuwa kuna shule nyingi sana na ukilinganisha zamani na sasa; kuna vyuo vikuu vingi na kulikuwa na chuo kikuu chenye wanafunzi 14 wa Sheria pale Lumumba. [ukweli ni kuwa, University of East Africa (Makerere) katika kuhakikisha inapanuka, ilianzisha tawi Tanzania na wanafunzi walikuwa pale Ushirika na walikuwa wanalala Kigamboni wakati kunajengwa UDSM]

(3) Profesa Tibaijuka: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

- Kimsingi sikujua hata alichokuwa anakielezea pale jukwaani zaidi ya kuzungumza kuwa alifika Dar 1970 na yeye ni Mwalimu wa UDSM (Economics) na kuwa alikuwa NJE ambako baada ya kuchuma (alimaanisha mali, ila akaja na kusema kuchuma Ujuzi) alirudi Tanzania.

- Alisema tu kuwa kero za Ardhi Kigamboni na Kurasini zinafahamika na watazifanyia kazi; na kwenye bajeti ya 2012/2013 wametenga fedha kwa ajili ya mipango mingi ya maendeleo.

- Zaidi pia alisema juu ya ujio wa Mji wa Kisasa wa Kigamboni utakaofanana na Dubai na Bahrain na kwamba wananchi waendelee kumpatia kero zao na kuwa kulipa pango kwamiezi 12 ni batili na uhalali ni kulipa kwa miezi 3 tu.

(4) Dr. Harisson Mwakyembe: Waziri wa Uchukuzi.

- Nadhani hakuwa anajua Ilani ya CCM inasemaje au pia hakujua yuko mkutanoni pale kufanya nini, maana alianza kuzungumzia kuhusu Wapinzani kuelezea MADUDU YALIYOBAINIWA NA CAG na kwamba Mamlaka makubwa kapewa CAG na Rais (sikuelewa uhusiano!).

- Zaidi ya kuzungumza juu ya kutozwa nauli ya 1,500 Tegeta; na nauli za Kimara na kutoa namba yake ya simu (0782 24 25 26) ili tumpigie na kumpa kero kwakuwa ‘ana simu kubwa' hakuna la maana alilozungumza.

- Kauli zake nyingi ni zilezile za ‘mipango' ya kufanya hiki na kile: kuwa na treni Ubungo Maziwa mpaka Stesheni; kufufua TAZARA, kusafisha Bandari. Alimalizia kwa kusema ' TUPENI MUDA TUNAYAFANYIA KAZI MATATIZO YENU'

(5) Dr. John Magufuli: Waziriwa Miundo Mbinu.

- Pamoja na kwamba tangu awali nilitegema kusikia idadi yakilometa za lami zinazojengwa na majina ya makampuni, sikutegemea kufahamu kuwa kipaji chake kingine ni kufahamu lugha mbali mbali za Kitanzania.

- Aliendelea tu kutaja kilometa za Lami zinazowekwa huku akitoa ulinganisho wa kilometer za lami tangu uhuru (6,500) hadi sasa (11,154) tofauti la kauli ya awali ya Wassira kuwa uhuru kulikuwa na barabara 3 tu (Dar – Moro. Hii naijua ina kama 200kms; Tanga - Korogwe ; kama 101kms na Arusha – Moshi; kama 90kms.)

- Alizungumza pia kuwa bajeti hii ya 2012/2013 imepanga kutekeleza miradi mingi ya maendeleo ya barabara. Labda tukio la kusisimua ni kuwa, wakati akiwa anaendelea kuongea (huku ikijionyesha dhahiri kuna kitu anakisubiria), Magufuli alitangaza kuwa ameongea kwa muda mrefu na amemaliza muda wake lakini anatambua kuwa kuna watu wanataka kurudisha kadi za CCM (akabadili ghafla na kusema za vyama vingine) waziwasilishe.

Katika hali ya kushangaza, waliibuka watu wa umri mmoja (vijana wa kike na kiume wa umri wa miaka 28 – 33), na ambao walionekana wakiwa wanafahamiana kabla (au kukaa pamoja kabla), na waliokuwa wakicheza wimbo mmojakwa umahiri walirudisha kadi. Kadi hazikuonekana na wala hawakujitokeza katika kuzungumza kwa nini ‘walihama huko walikotoka' na kujiunga na CCM.

HITIMISHO

- Lazima nikiri, kwa kusikia na kutazama yaliyosemwa na CCM katika mkutano wao leo, ni dhahiri kuwa CCM imefikia mwisho wake kwa kuwa imeshindwa kuwapa majibu sahihi watanzania juu ya shida zao na namna serikali ya CCM ilivyoweza kuwakwamua wananchi na mipango yake thabiti ijayo katika kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa.

- Pamoja na kuwa Kinana alikuja kuelezea kuwa mada nyingine mbili (Katiba na Zanzibar) zitawasilishwa na Kamati/Halmashauri kuu kwaKamati ya Warioba, lakini ukweli ni kuwa walikosa majibu ya kuridhisha.

- Mwanzoni walisema hawako pale kujibu hoja za vyama vingine au kuweka mipasho, lakini kauli zao zilijidhihirisha kuwa hawakuwa na la maana la kusema/kuwaambia wananchi (mfano, salamu ya ‘vyama vingine vidogo' hoyee, ya Magufuli, Mbowe arudi kuuza Pombe, CCM wataweka lami na CHADEMA waandamane kwenye hizo lami n.k)

- Kimsingi ni kama vile tulikuwa kwenye mkutano wa kampeni, kusikiliza ahadi za nini chama kitafanya na wala si nini kimefanywa na serikali ndani ya 2010 – 2015.

- Walichokifanya mawaziri hawa, wasomi, ni upotezaji wa muda wa wananchi na upotevu wa rasilimali za Taifa kwani wangeweza kuongea waliyoongoea kwa kuwaambia tu manaibu waziri wao wazungumze na wahariri au wazee wa Dar Es Salaam na si kama walivyofanya.

CCM Imejivua nguo rasmi leo; CCM Imekufa Rasmi
 

Communist

JF-Expert Member
Jun 1, 2012
5,398
2,000
Wasira hajui kama kuna viti vinaitwa index. Yeye alikuwa anasoma tarakimu tu. Nyingine zilionyesha kushuka kwa ratio kati yake na ongezeko la idadi ya watu. CCM inakufa.
 

AlamaZA NYAKATI

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
274
0
Nimesikiliza mwanzo mpaka mwisho HAKUNA lolote la maana lililozungumzwa.
Magamba kwisney...........PIPOZ.......................................................POWER
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,961
2,000
Huyu jamaa wa Bunda anatupa takwimu za 1961 anazilinganisha na za 2012?? Ukichukua kwa idadi ya population tuliyo nayo sasa hivi tuko nyuma kwa zaidi ya 35% kwa hiyo miaka yao ya utawala. Mambo ya aibu haya.

Magufuli anatupa kilomita za lami hela ni za mikopo ambozo Ccm inawaachia watoto na wajukuu wetu madeni ya kulipa huki wakitoa zawadi ya madini na wanyama pori wetu ughaibuni. Halafu wanaenda kuwaomba mikopo, jamani??

CCM mnaongea na watu wenye akili sio wagagagigikoko!
 

Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
1,195
Waliotarajia mazuri leo ndio wa kuhurumiwa.

CCM hawawezi kubadilika.
 

Ngarenaro

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
308
225
Acha upotoshaji wakati mwingine si lazima sana kuchambua mambo ya CCM, ambayo ni dhahiri yapo nje ya uwezo wako, ukweli ni kwamba umeupindisha ukweli na umepotosha kwa kiasi kikubwa yale yaliyozungumza kwenye Mkutano wa leo.
 

Honolulu

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
5,648
1,225
Acha upotoshaji wakati mwingine si lazima sana kuchambua mambo ya CCM, ambayo ni dhahiri yapo nje ya uwezo wako, ukweli ni kwamba umeupindisha ukweli na umepotosha kwa kiasi kikubwa yale yaliyozungumza kwenye Mkutano wa leo.
Hizi ndizo kauli za wasichana wanaobishana sokoni kuhusu mvulana yupi ni mzuri. Na ccm imeishaujua ujinga wa watanzania na ndio maana inawatongoza na inapowapata inawatumia ipasavyo.

Ccm inawahadaa watu kama wewe mithili ya mvulana anayemtafuta msichana!!! Inawatongoza kwa vitisheti vya njano na vikofia vya kijani; Inawapa lifti; inawalisha wali kuku; inawatumbuiza kwa taarabu; inawaahidi maisha bora na kisha inawahonga elfu tano!! Kwa ulaini wananchi wanakubali kufanya mapenzi na ccm. Wanapewa mimba, wanazaa ufukara na kisha wanatelekezwa kwa maisha duni!

Nionavyo mimi:
Watanzania wakiteseka na mazingaombwe ya ugumu wa maisha ni sawa tu!! Ni haki yao!! Waendelee tu kutaabika kwa kuwa dhiki, mahangaiko na ufukara wanavitaka wenyewe!!
 

Osaka

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
1,762
1,225
...Lazima nikiri, kwa kusikia na kutazama yaliyosemwa na CCM katika mkutano wao leo, ni dhahiri kuwa CCM imefikia mwisho wake kwa kuwa imeshindwa kuwapa majibu sahihi watanzania juu ya shida zao na namna serikali ya CCM ilivyoweza kuwakwamua wananchi na mipango yake thabiti ijayo katika kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa.
Wewe umenena!

 

Honolulu

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
5,648
1,225
CCM imeishaujua ujinga wa watanzania na ndio maana inawatongoza na inapowapata inawatumia ipasavyo.

Inawahadaa watanzania mithili ya mvulana anayemtafuta msichana!!! Inawatongoza kwa vitisheti vya njano na vikofia vya kijani; Inawapa lifti; inawalisha wali kuku; inawatumbuiza kwa taarabu; inawaahidi maisha bora na kisha inawahonga elfu tano!! Kwa ulaini wananchi wanakubali kufanya mapenzi na CCM. Wanapewa mimba. Wanazaa ufukara na kisha CCM inawatelekeza kwa maisha duni!

Nionavyo mimi:

Watanzania wakiteseka na mazingaombwe ya ugumu wa maisha ni sawa tu!! Ni haki yao!! Waendelee tu kutaabika kwa kuwa dhiki, mahangaiko na ufukara wanavitaka wenyewe!!
 

Edson

JF-Expert Member
Mar 7, 2009
9,496
2,000
Acha upotoshaji wakati mwingine si lazima sana kuchambua mambo ya CCM, ambayo ni dhahiri yapo nje ya uwezo wako, ukweli ni kwamba umeupindisha ukweli na umepotosha kwa kiasi kikubwa yale yaliyozungumza kwenye Mkutano wa leo.
kama hukupata bahati ya kusikiliza na kutazama mkutano wa majizi leo usingesema ulichosema..........kama kweli umetazama niambe ni wapi mleta thread amepotosha
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,865
1,225
Wako wapi wale waliozusha SHIBUDA atarudisha kadi ya CHADEMA leo? MBELE YA UMATI?

Shibuda kaishiwa kisiasa, na hao wazushi wameishiwa mara mbili wanampa Umaarufu wa Jikoni...
 

Bob G

JF-Expert Member
Oct 5, 2011
2,352
1,500
Taarabu zimeendelea kutawala mikutano ya ccm, hivi kwanini wanaccm hushangilia sana mambo yasiyo na maana na ya msingi hawapendi kuyasikia?
 

DOWN SYNDROME

Member
Jun 8, 2012
18
0
Acha upotoshaji wakati mwingine si lazima sana kuchambua mambo ya CCM, ambayo ni dhahiri yapo nje ya uwezo wako, ukweli ni kwamba umeupindisha ukweli na umepotosha kwa kiasi kikubwa yale yaliyozungumza kwenye Mkutano wa leo.

Wewe jamaa ni muongo sana! Nyie ndio wasaliti wakubwa wa watanzania wote masikini,nenda kafie huko KUZIMU na CCM yako!
 

nundaz

JF-Expert Member
Jun 8, 2012
259
250
watu wenyewe walikuwa hawapo pale mentallity.wengi wamezolewa mitaan kuja kula ubwabwa wao.m4C INAWATIA WAZIMU
 

Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
12,155
2,000
Kama kuna mtu haja notice hili atakuwa na Matatizo.

1. Kasimama Magembe
---- Huyu akaishia kutoa ahadi mpya Lukuki kama vile ndo anaomba kura, Yan huu ugonjwa hata Mwenyekiti wao anaugua, kila atakaposimama atatumia platform hiyo Kutoa ahadi Mpya.
2. Wasira,
Huyu ndo kabisa, yani ameonesha ni kuwa kila akilala akiamka Jinamizi la CHADEMA na M4C Linamtesa mno,Mbaya zaid akafanya kitu inaitwa Personal attack kwa Mbowe, CDM wakiendeleza hii Movement Wasira ata colapse Mazima
3.Mwakyembe,
Huyu naye yuko Vuguvugu Mno, haeleweki though unaweza kusema kuwa ndiye Magamba pekee aliyejaribu kuongea Point leo, nae pia aliishia kuonesha hofu kwa CDM though hakutaja direct, lakini Utu uzima Dawa, Old is Gold, sie Watu wazima tukamuelewa.
4. Magufuli.
Naye akajikita zaid katika Agenda Kuu ya Leo yani CHADEMA, huyu amejitahid mno kutokutoka Nje ya Mada kuu ya leo ambayo Magamba wameandaa Mkutano wao Purposely Kuijadili CHADEMA jinsi inavyowanyima Usingizi

My take:
CCM wanacheza Ngoma ya CDM, wanazidi kuonesha ni jinsi gani CDM ni tishio kwao, CDM tuendelezenI hii M4C,
CCM ni wepesi Mnoooooooooooo
Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeesssssssssssssssssssssssssssss
 

Mlingwa

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
381
170
ASANTE SEBM,
Hakika umetuhabarisha kinagaubaga kuhusu yaliyojiri huko, nimekusoma sawia katika hitimisho lako, Hongera kwa kuwa umekuwa wazi ku-nukuu angalabu kila msemaji hata kama sio wote. Asante sana.
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom