Mkutano wa CCM Jangwani: CCM yafa Rasmi

Ccm wafe au wasife hawani impact yoyote katika maisha yangu na ya watanzania wengi.
The unseen is illustrated by the seen.
 
Acha upotoshaji wakati mwingine si lazima sana kuchambua mambo ya CCM, ambayo ni dhahiri yapo nje ya uwezo wako, ukweli ni kwamba umeupindisha ukweli na umepotosha kwa kiasi kikubwa yale yaliyozungumza kwenye Mkutano wa leo.
Watu wazima wakiongea uwe unanyamaza kimya!!ngarenaro na jangwani wapi na wapi? Au ni wivu wa kutosombwa na malori kwenda karatu kula ubwabwa kama ilivyokuwa kipindi cha kampeni, tatizo lenu warangi wengi wa ngarenaro ni uvivu, na ujinga!

Kwenda zako huko.
 
Acha upotoshaji wakati mwingine si lazima sana kuchambua mambo ya CCM, ambayo ni dhahiri yapo nje ya uwezo wako, ukweli ni kwamba umeupindisha ukweli na umepotosha kwa kiasi kikubwa yale yaliyozungumza kwenye Mkutano wa leo.
acha ushamba wewe siku hizi dunia ni kijiji kimoja kila mtu ameona na kusikia kwangu mimi mtoa mada hakuwa biased amesema kilichojiri wewe kwa ugonjwa wa kupenda hujaona hata pumba moja ya mkutano ule gamba mkubwa wewe
 
Msishangae,hata mwanza walipokuja kujilopokea watu walibebwa kwenye malori na mabasi.Walipewa wali nyama,walickiliza maneno ya kwenye khanga ya Vicky Kamata na Suma Lee.Lakini ulipofika uchaguzi wa kata ya Kirumba tukawafundisha demokrasia hadi wakachukia na kuwakata mapanga wabunge wetu.Hawa magamba wamekengeuka kwa asilimia kubwa ndo maana wanahangaika majukwaani.Mi naamini sera zikitekelezwa wananchi wataona wenyewe siyo kuonyeshwa kwenye majukwaa.Ama kweli,mbio za panya huishia sakafuni.
 
wapendwa,

kwanza nakushukuru sana mleta mada ( SEBM) kwa kutuchambulia na kutuletea kwa muhtasari yote yaliyojiri. ubarikiwe sana mpendwa

matumizi ya pesa kwenye siasa ni kitu kibaya sana. kila anayeng'ara katika ccm alitumia pesa kuwa hapo alipo. matokeo yake wanasiasa wa kweli wamefunikwa na hawachomozi kwa kukosa pesa ama kwa kulinda maadili wakajizuia kutoa rushwa.

hao waliozungumza wote, hakuna hata mmoja aliyepiga siasa pekee kupata nafasi aliyonayo. naweza kuhitimisha kuwa hao wote si mifano ya kuigwa kisiasa na kimaadili na hata siasa yenyewe hawaijui! hivyo haishangazi kuona wakizungumza kama wapinzani wakati chama chao kiko madarakani kwa nusu karne sasa!

hawa ndio magamba halisi waoapaswa kujipima na ujiondoa chamani ama waondolewe! kwa kweli wamenisikitisha sana

mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God!
 
Wadau Habari?
Leo sikupata muda wa kusikiliza viongozi wakihutubia katika mkutano wa CCM viwanja vya Jangwani naskia kunaitwa siku hizi CHADEMA SQUARE naomba kwa aliesikiliza asinambie wamezungumzia nini? Naomba kama kuna mzungumzaji yeyote kati yao amegusia jambo lolote kati ya mambo yafuatayo, na labda atanisaidia kama ataniambia wamelizungumziaje?
1. Wizi wa kagoda Agriculture, Deep Green, Buhemba EPA, je wamedokeza chochote kuhusu wizi huu?

2. Vipi jamani wamegusia kuhusu Uuzwaji wa nyumba za serikali? Vipi wamesema lini watazirudisha? Au wanadhani hatuzihitaji?

3. Vipi kuhusu Mikataba mibovu ya madini tayari wameirekebisha?

4. Kuhusu huduma mbovu za jamii wamezungumzia mipango yeyote ya kuiboresha?

5. Twiga vipi waliosafirishwa kuna yeyote aliyefikishwa mahakamani?

Ni hayo tu kwa sasa, nasubiri majibu wadau
 
CCM imeishaujua ujinga wa watanzania na ndio maana inawatongoza na inapowapata inawatumia ipasavyo.

Inawahadaa watanzania mithili ya mvulana anayemtafuta msichana!!! Inawatongoza kwa vitisheti vya njano na vikofia vya kijani; Inawapa lifti; inawalisha wali kuku; inawatumbuiza kwa taarabu; inawaahidi maisha bora na kisha inawahonga elfu tano!! Kwa ulaini wananchi wanakubali kufanya mapenzi na CCM. Wanapewa mimba. Wanazaa ufukara na kisha CCM inawatelekeza kwa maisha duni!

Nionavyo mimi:

Watanzania wakiteseka na mazingaombwe ya ugumu wa maisha ni sawa tu!! Ni haki yao!! Waendelee tu kutaabika kwa kuwa dhiki, mahangaiko na ufukara wanavitaka wenyewe!!
Tafadhali bana...kabla ya kila neno 'watanzania' anza na 'baadhi ya'...unakuwa unatutusi sana ukitujumuisha sote na takataka za CCM...!
 
Ni aibu kwa chama kikongwe kama CCM kufanya mkutano wa kisanii kabisa kama huu.
Hii ni mbinu ya secretarieti ya Mukama kujifanya inafanyakazi kukwepa lawama,mambo kama haya alifanya sana Makamba senior chama kikapoteza mwelekeo naona wakina Nape wanarudia usanii uleule ili chama kife kabisa.
 
utasubiri jibu mpaka yesu atarudi, hatamimi sijasikiliza lakini wote waliokuwepo hakuna mwenye uthubutu wa kuyaongelea...
 
CCM kushindana na chadema wanajitia aibu mkutano haukuwa na hamasa yeyote wale wa mama na mikorogo yao unawaona walivyochoka ,Mawaziri hawana hata mfupa wa kujiamini walikuwa wanaonyesha uoga,Vitisho Mwakyembe analalamika eti atatimua wapi hivi nani amewambiya kutisha wafanya kazi kutaongeza tija,wakati chama chao ndio msuka raketi ya wizi
Kinana Msomali mwizi wa pembe za ndovu,msafirisha wanyama hai,mleta wasomali nchini alshabaab eti ana nguvu hata ya kusema wapinzani hawana safu ya kuongoza CCM wamelala usingizi kweli ,wanadhani wataendelea kuiba kura tunawaambia safari hii tutapiga kura na kuilinda hawakujiandaa kabisa
 
ccm walidhani hukumu itatolewa kwa kuangalia namba ya wahudhuriaji kumbe ni ujumbe kwa waliofika na wasiofika.ni fedheha ya hali ya juu.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Nape amegusia kuhusu kufungua band na lusinde. Na mipasho ili tawala pamoja na mwanachama mmoja kusisitiza hawataki mipasho,lakini nape hakumuelewa.

Wassira alisema alikuwa south kwenye sherehe.
 
Mkuu SEBM,

Umesahau ishu moja ya msingi kabla ya kutangaza kifo cha CCM.

- Leo wamejitokeza wanawake wengi kuliko ule mkutano wa CHADEMA. In fact CHADEMA wanawake walikuwa ni kama hawapo kabisa. Hii ni nguzo muhimu sana ya uhai wa chama.

- Na kwenye taarifa ya mtandao wa chama wanasema wana matawi kama 600 Dar es Salaam, na wanachama/wakereketwa 400,000. Sina uhakika na numbers, lakini ni kweli kuwa CCM bado wana mtandao mkubwa wa matawi.
 
Acha upotoshaji wakati mwingine si lazima sana kuchambua mambo ya CCM, ambayo ni dhahiri yapo nje ya uwezo wako, ukweli ni kwamba umeupindisha ukweli na umepotosha kwa kiasi kikubwa yale yaliyozungumza kwenye Mkutano wa leo.

Tuandikie yaliyo sahihi basi, sio kupinga tu.

Kwa taarifa yako watu tumefuatilia kwa makini, hicho anachosema huyo mdau ni sawa kabisa. CCM has very limited ruling time. hayo tulisikia na kuyaona leo ni dalili tosha kuwa kifo chao kimekaribia kabisa.

Wameshindwa kuelewa Siasa na Muziki sio mbinu tena kwa sasa. wanamuziki wenyewe wanakuja na playback kuashiria huwa hata hawana maandalizi.

CCM your Days for rulling this TZ are numbered.
 
Ukipewa nauli unaweza uliza?watu walikuwa picnic usiwaze sana hawawezi kuongelea mambo hayo
 
naombea mtizamo wa kiccm uendelee, yaani wizi wao na ufujaji ili walio wavivu wa kufikiri wajue wajibu wao kama waTZ!
 
Back
Top Bottom