Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
Mtolea aliyekuwa mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF hadi Novemba 2018 alipojiunga na CCM na kupitishwa kuwania ubunge, leo Alhamisi Desemba 20, 2018 ametangazwa na msimamizi wa uchaguzi, Lusubilo Mwakabibi kuwa mshindi.
Akizungumza na Mwananchi leo Mtolea amekiri kupita bila kupingwa.
Katika hati ya kuchaguliwa kuwa mbunge ambayo Mwananchi imeiona inaeleza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 81 (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, Mtolea amechaguliwa kuwa mbunge wa Temeke katika uchaguzi uliofanyika leo.
Kifungu cha 45 (2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, na kile cha 44 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, vinasema endapo mgombea aliyeteuliwa katika uchaguzi ni mmoja tu, mgombea huyo atahesabika amechaguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Soma pia > Mkurugenzi aliyesimamia uchaguzi wa marudio Buyungu ahamishiwa Dar es salaam manispaa ya Temeke - JamiiForums