Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke amtangaza Mtolea kuwa mshindi wa Kiti cha Ubunge

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
IMG-20181220-WA0045.jpg
Dar es Salaam. Abdallah Mtolea, aliyepitishwa na CCM kuwania Ubunge wa Temeke, leo Alhamisi Desemba 20, 2018 amepita bila kupingwa baada ya wagombea waliokuwa wamechukua fomu kuwania nafasi hiyo kukosa sifa.

Mtolea aliyekuwa mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF hadi Novemba 2018 alipojiunga na CCM na kupitishwa kuwania ubunge, leo Alhamisi Desemba 20, 2018 ametangazwa na msimamizi wa uchaguzi, Lusubilo Mwakabibi kuwa mshindi.

Akizungumza na Mwananchi leo Mtolea amekiri kupita bila kupingwa.

Katika hati ya kuchaguliwa kuwa mbunge ambayo Mwananchi imeiona inaeleza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 81 (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, Mtolea amechaguliwa kuwa mbunge wa Temeke katika uchaguzi uliofanyika leo.

Kifungu cha 45 (2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, na kile cha 44 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, vinasema endapo mgombea aliyeteuliwa katika uchaguzi ni mmoja tu, mgombea huyo atahesabika amechaguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Soma pia > Mkurugenzi aliyesimamia uchaguzi wa marudio Buyungu ahamishiwa Dar es salaam manispaa ya Temeke - JamiiForums
 
Huyu Mwakibibi dawa yake inachemka, atanyweshwa muda sio mrefu. Aliharibu uchaguzi kwenye lile jimbo akapewa Eng Chiza, wakati alishindwa. Akahamishiwa Temeke. Leo anakuambia wagombea wa vyama vyote, hawawezi kujaza fomu, sasa sijui zimeandikwa Kinyakyusa? Au!! Maana yeye tu ndie anajua kuzijaza na anawajazia wagombea wa CCM. Jamani watanzani tuamke na kuikataa hii Tume ya uchaguzi ya CCM.
 
Kijana wa Kijitonyama....mzee wa nyama laini....
 
Huyu Mwakibibi dawa yake inachemka, atanyweshwa muda sio mrefu. Aliharibu uchaguzi kwenye lile jimbo akapewa Eng Chiza, wakati alishindwa. Akahamishiwa Temeke. Leo anakuambia wagombea wa vyama vyote, hawawezi kujaza fomu, sasa sijui zimeandikwa Kinyakyusa? Au!! Maana yeye tu ndie anajua kuzijaza na anawajazia wagombea wa CCM. Jamani watanzani tuamke na kuikataa hii Tume ya uchaguzi ya CCM.
Ni jirani yetu ntamtegea bomu la nyukilia
 
Back
Top Bottom