Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke amtangaza Mtolea kuwa mshindi wa Kiti cha Ubunge

True; upande huo wa gharama unaweza kuwa mzuri lakini sidhani kama tunaweza tukakubali chaguzi zote watu wapite bila kupinga ili kusifanyike uchaguzi... Ndio maana akiwepo mgombea mmoja wa Urais, hapiti bila kupingwa...
Msaada kwenye tuta, hivi akiwa mgombea Uraisi mmoja na akapata kura elfu 1,ambazo ni kura nyingi kuliko za mgombea mwingine ambaye hayupo, hajashinda uchaguzi?
 
Haiwezekani kuzima sauti za watu kipuuzi namna hii. mnaharibu umoja na ustawi wa taifa letu.
 
Huyu Mwakibibi dawa yake inachemka, atanyweshwa muda sio mrefu. Aliharibu uchaguzi kwenye lile jimbo akapewa Eng Chiza, wakati alishindwa. Akahamishiwa Temeke. Leo anakuambia wagombea wa vyama vyote, hawawezi kujaza fomu, sasa sijui zimeandikwa Kinyakyusa? Au!! Maana yeye tu ndie anajua kuzijaza na anawajazia wagombea wa CCM. Jamani watanzani tuamke na kuikataa hii Tume ya uchaguzi ya CCM.

Kuna muda nashangaaga na kucheka, hiv kwa sheria hyo mbona haitokei mgombea wa ccm ndio akakosea kujaza form.
 
Afadhali turudi kwenye chama kimoja ambacho kitaongoza na Jiwe lisilooneshwa njia, hapo ndio namba tutazisoma kisawasawa hadi tutakumbuka tulikotoka.
 
Sasa alitakiwa kufanya nini kama sheria inamtaka afanye hivyo? ndio maana miye nilipingaga ubunge wa kupita bila kuchaguliwa...
Mimi naunga mkono tumeokowa pesa za walipa kodi, hata ungefanyika uchaguzi maagizo yanafahamika ni lazima atangazwe Mtolea.

Chadema kujitowa kwenye hizi chaguzi za marudio za maigizo ni uamuzi wa busara sana.
 
2020 Wabunge wengi wa CCM watapita bila kupigwa zaidi ya 150 watapitishwa kwa hiyo njia.....
 
Kuitoa CCM kwa kura ni ngumu kama ngamia kupita kwenye mlango wa kirikuu

CCM itatolewa kwa vita tuuu.

Wameshika kila sehemu Muhimu kuanzia juu hadi chini
 
Dar es Salaam. Abdallah Mtolea, aliyepitishwa na CCM kuwania Ubunge wa Temeke, leo Alhamisi Desemba 20, 2018 amepita bila kupingwa baada ya wagombea waliokuwa wamechukua fomu kuwania nafasi hiyo kukosa sifa.

Mtolea aliyekuwa mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF hadi Novemba 2018 alipojiunga na CCM na kupitishwa kuwania ubunge, leo Alhamisi Desemba 20, 2018 ametangazwa na msimamizi wa uchaguzi, Lusubilo Mwakabibi kuwa mshindi.

Akizungumza na Mwananchi leo Mtolea amekiri kupita bila kupingwa.

Katika hati ya kuchaguliwa kuwa mbunge ambayo Mwananchi imeiona inaeleza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 81 (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, Mtolea amechaguliwa kuwa mbunge wa Temeke katika uchaguzi uliofanyika leo.

Kifungu cha 45 (2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, na kile cha 44 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, vinasema endapo mgombea aliyeteuliwa katika uchaguzi ni mmoja tu, mgombea huyo atahesabika amechaguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Soma pia > Mkurugenzi aliyesimamia uchaguzi wa marudio Buyungu ahamishiwa Dar es salaam manispaa ya Temeke - JamiiForums
Ni vema 2020 tukafanya hivyo kuanzia juu mpk chini ili tusipoteze muda, fedha na damu za ndugu zetu.
 
Kwa hii inayoitwa 'tume ya uchaguzi' kama kuna chama chochote kitakachoshiriki kwenye uchaguzi unaoandaliwa nayo, basi hicho chama lazima kitakuwa ni "Chama Pandikizi tu". Nothing Else.
 
hiyo barua ya kumtangaza ina makosa huwezi kusema uchaguzi umefanyika wakati unajua hakuna uchaguzi uliofanyika na ikibaki hivyo vizazi vijavyo vitaamini kuna uchugazi ulifanyika wakati siyo ni lazima wahusika waone namna ya kuandika ukweli wa kilic
 
Ni demokrasia ya kujiamulia kila mmoja awe upande gani wa kushindwa au kushinda!
Yaa nakubaliana nawe kuwa hata kumuacha mtu afanye mambo yake kutokana na ujinga wake nayo ni demokrasia. Ingawa kumfahamisha ni wajibu wa kibinadamu. Nakufahamisha tuu kutimiza wajibu huo
 
Back
Top Bottom