Mkurugenzi wa Makampuni ya Vanilla Matatani kwa utapeli, RC Makonda aagiza awekwe chini ya ulinzi hadi alipe mamilioni aliyotapeli

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
750
1,800
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya amejikuta Mikononi mwa Polisi Mara baada ya kutajwa kutapeli wakulima wa Vanila mamilioni ya fedha na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paulo Makonda kuagiza akamatwe na alipe madai yao chini ya ulinzi mkali wa polisi Arusha.

Mnkondya alikamatwa mapema jana ofisini kwake katika jengo la Ngorongoro jijini Arusha na kupigwa pingu hadi katika viwanja vya ofisi za mkuu wa Mkoa Arusha , ambapo Makonda alikuwa akisikiliza malalamiko ya wananchi waliokuwa wamejikusanya katika viwanja hivyo wakiwa na madai mbalimbali.

Mnkondya anadaiwa kuwatapeli wananchi wawili aliowarubuni kuwekeza mamilioni ya fedha katika mradi wake wa kilimo cha Vanila lakini baada ya kupokea fedha hizo aliingia mitini na kutelekeza mashamba aliyokuwa ameingia mkataba na wananchi hao.

Mmoja ya wananchi hao akiongea kwa uchungu ambele ya RC Makonda akiwakilisha wenzake, alidai kudhulumiwa na Mkurugenzi huyo wa Vanila akiwalaghai kwamba watoe pesa na yeye huwapatia shamba la kulipa kilimo cha vanila na pindi zao hilo linapoiva atanunua mwenyewe kwa bei nzuri inayofikia sh,1,000,000 kwa kilo moja jambo ambalo sio kweli .

Hata hivyo baada ya maelezo hayo ya wananchi hao ,Makonda alimwagiza mkuu wa polisi wa wilaya (OCD )kumsaka popote alipo Mnkondya popote alipo aje kujibu hoja hizo na ndipo alipokamatwa ofisini kwake alikokuwa amejifungia na kuletwa akiwa chini ya ulinzi na pingu mkononi.

RC Makonda baada ya kumhoji mbele ya umati mkubwa wa wananchi waliokuwa wamefurika katika viwanja vya ofisi yake maelezo ya Mnkondya yalionekana kuwa na mkanganyiko unaoashiria kuwepo vitendo vya kitapeli licha ya kujipambanua kwamba yeye ni mwekezaji mwenye mashamba bora Afrika lakini mbele ya makonda hakufua dafu badala yake alijikuta mikononi mwa OCD baada ya RC Makonda kuagiza akae chini ya ulinzi mpaka atakapolipa fedha za wadai wake.
 
Ampeleke mahakamani kWa jinaüyo ya kujipatia fed kwa nia za udanganyifu, kisha awapatie waathirika msaada wa kisheria kwenye kesi ya maddi....
 
Hao waliyotapeliwa ni wajinga tu
Makonda angeachana nao

Ova
 
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya amejikuta Mikononi mwa Polisi Mara baada ya kutajwa kutapeli wakulima wa Vanila mamilioni ya fedha na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paulo Makonda kuagiza akamatwe na alipe madai yao chini ya ulinzi mkali wa polisi Arusha.

Mnkondya alikamatwa mapema jana ofisini kwake katika jengo la Ngorongoro jijini Arusha na kupigwa pingu hadi katika viwanja vya ofisi za mkuu wa Mkoa Arusha , ambapo Makonda alikuwa akisikiliza malalamiko ya wananchi waliokuwa wamejikusanya katika viwanja hivyo wakiwa na madai mbalimbali.

Mnkondya anadaiwa kuwatapeli wananchi wawili aliowarubuni kuwekeza mamilioni ya fedha katika mradi wake wa kilimo cha Vanila lakini baada ya kupokea fedha hizo aliingia mitini na kutelekeza mashamba aliyokuwa ameingia mkataba na wananchi hao.

Mmoja ya wananchi hao akiongea kwa uchungu ambele ya RC Makonda akiwakilisha wenzake, alidai kudhulumiwa na Mkurugenzi huyo wa Vanila akiwalaghai kwamba watoe pesa na yeye huwapatia shamba la kulipa kilimo cha vanila na pindi zao hilo linapoiva atanunua mwenyewe kwa bei nzuri inayofikia sh,1,000,000 kwa kilo moja jambo ambalo sio kweli .

Hata hivyo baada ya maelezo hayo ya wananchi hao ,Makonda alimwagiza mkuu wa polisi wa wilaya (OCD )kumsaka popote alipo Mnkondya popote alipo aje kujibu hoja hizo na ndipo alipokamatwa ofisini kwake alikokuwa amejifungia na kuletwa akiwa chini ya ulinzi na pingu mkononi.

RC Makonda baada ya kumhoji mbele ya umati mkubwa wa wananchi waliokuwa wamefurika katika viwanja vya ofisi yake maelezo ya Mnkondya yalionekana kuwa na mkanganyiko unaoashiria kuwepo vitendo vya kitapeli licha ya kujipambanua kwamba yeye ni mwekezaji mwenye mashamba bora Afrika lakini mbele ya makonda hakufua dafu badala yake alijikuta mikononi mwa OCD baada ya RC Makonda kuagiza akae chini ya ulinzi mpaka atakapolipa fedha za wadai wake.
CCM wajanja Sana wamemuweka hamnazo Ili watu wajadili vitiko vyake wasiohoji kuhusu umeme,maji
 
Back
Top Bottom