LHRC yamuonya Makonda kwa kumdhalilisha Mtumishi wa Kike mbele ya Umati wa Wananchi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,517
8,451
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa taarifa ya Onyo kwa Mkuu wa Mkoa Arusha, Paul Makonda baada ya kuonekana kwenye Video akitoa kauli za udhalilishaji dhidi Mtumishi wa Kike kutoka Longido

Akitoa taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dkt. Anna Henga, amesema ""Tumepokea kwa masikito Video inayomuonesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha akimdhalilisha Mtumishi wa jinsia ya Kike kule Longido. Tunakemea vikali kauli hizo hasa kwa Mtu kama yeye Mkuu wa Mkoa"

Aidha, LHRC imemtaka Makonda kuomba radhi na kuacha tabia hiyo kwasababu inatweza Utu wa Mwanamke na kushusha juhudi za kutetea Haki za Wanawake huku Viongozi kama yeye wakitoa kauli zinatoa mifano mibaya kwa watu wengine

Kupitia Video hiyo, RC Makonda anasikika akimtaka Mtumishi huyo kuzungumza vizuri na si kama anaongea na mtu anayetaka kumposa au yuko kwenye Kitchen Party na pia yeye (RC) ana Mke mzuri.

Pia soma:
- Makonda ashtakiwe kwa udhalilishaji alioufanya kwa mwanakamati huyu

- Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa walaani matamshi ya Paul Makonda

- Paul Makonda: Kwa umri huu nitishike na kauli za Watu? Mtapata watu wengine watakaowapetipeti
 
Link
Video
Waraka
Barua
Onyo
Viko wapi?
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa taarifa ya Onyo kwa Mkuu wa Mkoa Arusha, Paul Makonda baada ya kuonekana kwenye Video akitoa kauli za udhalilishaji dhidi Mtumishi wa Kike kutoka Longido

Akitoa taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dkt. Anna Henga, amesema ""Tumepokea kwa masikito Video inayomuonesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha akimdhalilisha Mtumishi wa jinsia ya Kike kule Longido. Tunakemea vikali kauli hizo hasa kwa Mtu kama yeye Mkuu wa Mkoa"

Aidha, LHRC imemtaka Makonda kuomba radhi na kuacha tabia hiyo kwasababu inatweza Utu wa Mwanamke na kushusha juhudi za kutetea Haki za Wanawake huku Viongozi kama yeye wakitoa kauli zinatoa mifano mibaya kwa watu wengine

Kupitia Video hiyo, RC Makonda anasikika akimtaka Mtumishi huyo kuzungumza vizuri na si kama anaongea na mtu anayetaka kumposa au yuko kwenye Kitchen Party na pia yeye (RC) ana Mke mzuri
 
Makonda awe makini. Kwa mtindo wake wa kazi Anatengeneza maadui wengi sasa kuna saa atajaa kwenye 18 anayemlinda atashindwa kumlinda.
 
Back
Top Bottom