Wanajidai hawajui ili hali mkopo wa wanafunzi tu watu wanarudisha na Kariba kadogo.Acheni akili za kibata, hiyo hela muda wote iliokaa huko ingekua na compound interest ingezaa kiasi gani? Yani mnadhani social security ni linear kiasi hicho kua utasema tu umepata faida ya 5% ?? Kama akili za phd ndio hizi bora kuishia cheti!
Ndugu Mlenge,
Umeniuliza 25% au 1/4 ni ya kitu gani, si ndiyo eeh?
Nilivyokuelewa = ni ya jumla ya michango ya mstaafu ktk muda wake wote wa utumishi + mchango wa mwajiri kwa kuzingatia kanuni ya kukokotoa mafao hayo.....
Kama nimekosea/sijaelewa, niko tayari kueleweshwa zaidi na zaidi.....
Wewe ndo umeona wakulima siku zote sio waelewa....acha kutoa maneno usiyoyajua!Huyu bibie asitufanye wajinga wa mahesabu.
20% ya mshahara ni kitu tofauti kabisa na 25% ya makusanyo yote ya makato ya pensheni!
Ajifunze kuwa haongei na wakulima wasiojua kitu.
Mbaya zaidi huyu ama na atueleze ni kwa nini usinirudishie 100% kwa mkupuo mmoja fedha niliyokatwa kwa miaka mingi.
Hivi hadi phd zipo za Picchu?Mkurugenzi mkuu wa SSRA bi Irene amesema mfanyakazi anachangia mifuko ya jamii kwa utaratibu wa 10% na mwajiri 10% au 5% na mwajiri 15% na kwa utaratibu wowote ule mchango wake ni jumla ya 20% ya mshahara wake.
Unapostaafu unalipwa kwa mkupuo 25 % ya mshahara wako je huoni kama tayari una faida ya 5% na bado utaendelea kupokea pension yako ya mwezi hadi ufe?
Irene amewaomba radhi wale wenye matatizo ya lugha kwani wakati ule wa semina elimishi kwa wastaafu alitumia lugha ya kitaalamu zaidi huenda ndio sababu hata Bulaya hakumuelewa.
Chanzo: Clouds 360!
Kalime korosho usikie muziki wake.Wewe ndo umeona wakulima siku zote sio waelewa....acha kutoa maneno usiyoyajua!
Hesabu anazielewa vizuri sema wewe ndio huku muelewa kwakuwa ulikuwa na jibu lako kichwani.Tatizo hapo nikwanini alipwe hiyo 62.5 na siyo 150.Wewe uwe unaelewa, kama ulichangie sh 50 mil maana yake ni kuwa hiyo ni 20% sasa wewe unalipwa 25% kwa mkupuo sawa na sh 62.5 milioni.
Kama Hisabati hujui hata QM inakushinda mkuu?!
Ni ndiyo, ndugu Kitaturu.
Jumla ya michango (ya mtumishi + ya mwajiri) haina uhusika wowote katika kuamua mafao ya mtu aliyechangia kuanzia miaka 15. Mafao ya pensheni ni kama bima ya kumsaidia mtu asiadhirike (fainali) uzeeni. Mafao ya pensheni si kama akaunti ya benki. Mafao yanaangalia vitu viwili tu:
1. Amechangia kwa muda gani? [Idadi ya Michango]
2. Mshahara wake wa mwisho ulikuwaje? [Wastani wa Jumla ya Mishahara ya Mwaka Mzima, (ukiangalia mishahara mikubwa aliyowahi kuipata kwa miaka mitatu, katika kipindi cha miaka kumi ya mwisho kabla kustaafu)].
Lengo ni kumfanya mstaafu apate angalau mshahara angalau unafanana na mshahara wake wa mwisho kila mwezi mpaka atakapofariki.
Ukitaka kupata amani moyoni, chukulia michango unayopelekewa kwenye mifuko ya pensheni ni sawa tu na michango yako unayopelekewa kwenye mfuko wa bima ya afya: ni kama ada ya uanachama na siyo amana kama za kwenye SACCOS au benki.
Mwisho wa mwaka huendi NHIF kusema, mmekata mshahara wangu mwaka mzima, na mimi sijaumwa. Nirudishieni hela zangu! Kwenye mafao ni hivyohivyo. Cha kuzungumzia ni muda wa kuchangia, na ukubwa wa mshahara wako wa mwisho. Na pensheni utakayolipwa kila mwezi. Chukulia malipo ya mkupuo kama "retro-rockets" za kukuwezesha kupata "soft-landing" kuingia kwenye kustaafu.
Je, kipi unapenda:
A. Mafao ya mkupuo makubwa, pensheni ya kila mwezi iwe ni kama utani (nauli ya kwenda kuyachukua toka kijijini kwenda wilayani ni kubwa kuliko mafao)
B. Pensheni ya kila mwezi ni kubwa (si haba, yanakuwezesha kupata rizki ya kila siku), mafao ya mkupuo kama haya?
Kama wewe tayari umeshastaafu, bila shaka jibu lako ni B. Kama bado kustaafu jibu la wengi ni A.
Hapa tunafikia kwenye maamuzi ya kifalsafa:
1. Je, mstaafu apewe hela zake zote, kwa mkupuo, na halafu apambane na hali yake akizitumbua vibaya? Ni mtu mzima mwenye akili timamu. Hela zake, kwa nini mtu aanze kumpangia matumizi? Mpe chake, asepe! Mbele ya safari kelele zote za kusema pensheni ya kila mwezi ni ndogo mno, haiendani na uhalisia, nk. ZIPUUZWE.
2. Je, kujiunga kwenye mifuko ya pensheni kuwe ni hiari au lazima?,
Kwa hiyo, 25% ni ya kwa kile ambacho mfuko unakadiria kuwa ni gharama itakazotumia kumpa hifadhi ya jamii mwanachama wa mfuko. Hiyo 25% siyo ya robo kwa yale mafao ya mkupuo.
Kama ulimsikia mwenzio alipata 100m wakati anastaafu, ina maana bado na wewe utapata hizohizo, kama sifa zenu zinafanana. Kwa vile mifuko mingi ilikuwa inatumia 25% kwa miaka mingi.
Huyu mama kanichanganya, nasoma koments ndo nachanganyikiwa zaidi.
Kwaniiiiiiii, haya mafao ya Wastaafu ni Stahiki zao au ni Favour? Ninachoamini ni kuwa zile ni Stahiki za wastaafu hawa, sasa kama ni stahiki zao, iweje waje kuwapangia namna ya matumizi? Mtu kamaliza kazi kwa muda uliopangwa apewe chake. Akienda kuzihonga atajua yeye, lile ni jasho lake.
Ama vipi hiyo mifuko iwe hiyari kujiunga. Kila mmoja achague anachoona kuwa sahihi fulu stopu
we nae tutokee hapa unajifanya kujua kumbe mbulura mmoja tu.100% ndio hiyo hiyo 20% usichoelewa ni nini?!
Mkuu kwa mantiki hiyo huoni mfanyakaziNadhani utakuwa umenielewa. Na kama ndiyo, basi ndo kusema michango hiyo inaweza kuingizwa tu kwenye bidhaa Kama kodi ili ukinunua chochote ndiyo unakuwa umechangia hivyo!!
Hahahaa...... Umeshapanic!we nae tutokee hapa unajifanya kujua kumbe mbulura mmoja tu.
Mbona huyu mama ni kilaza sana. Halafu ni PhD holder!