Mkurugenzi mkuu SSRA: Kiuhalisia michango yote ya mstaafu ni 20% ya mshahara wake so 25% inampa ziada ya 5%

Sio lazima kila kitu utetee Mkuu.. Haya mengine yanakugusa mpaka wewe mwenyewe na jamaa zako.. Hesabu ziko wazi, wewe unakazana kuzi-distort.. Kama 20% yako kwa miaka 30 imekutengenezea milioni 100, 25% ya milioni 100 ni kiasi gani..?
Usibishane na mtu ambaye analipwa kwa number of posts in the thread.

Hajui mshahara wala mifuko ya jamii haimhusu.
 
Mwambie watoe na hiyo 5% ibaki 20% kama ambavyo anadai ndiyo stahiki ya watumishi,nyau kabisa!

Yaani mfano nichangie 20% kila mwezi,tuseme hiyo 20% ni sawa na 150,000/- kwa mwezi, nifikishe jumla ya mil 50 kwa kipindi chote cha utumishi!

Halafu uje unipe 25%, sawa na mil 12.5 ya mil 50 niliyochangia!

Halafu useme hata hiyo umenifanyia hisani wakati ni wizi wa mchana kweupe?Pumbav kabisa!
Tena Jinga kabisa
 
Umesikia watumishi wa serikali na taasisi zake wanalalamikia mafao au hicho kikokotoo?

Alaa, kumbe kwako wewe hiki kinachoendelea hata kwenye mjadala huu uliouanzisha kufuatia kauli ya PhD holder wa SSRA mwanamama yule ni kitu gani bwana?

Wanapongeza siyo? Wanagongeana glass za champagne siyo kushangilia kikokotoo dhalimu?

Kwa taarifa yako mimi hapa tunayechat nawe ni mtumishi wa umma tena ktk taasisi nyeti kabisa ya serikali.

I am complaining. I am absolutely against this stupid decision!!
 
Alaa, kumbe kwako wewe hiki kinachoendelea hata kwenye mjadala huu uliouanzisha kufuatia kauli ya PhD holder wa SSRA mwanamama yule ni kitu gani bwana?

Wanapongeza siyo? Wanagongeana glass za champagne siyo kushangilia kikokotoo dhalimu?

Kwa taarifa yako mimi hapa tunayechat nawe ni mtumishi wa umma tena ktk taasisi nyeti kabisa ya serikali.

I am complaining. I am absolutely against this stupid decision!!
Mkuu mjadala uko mubashara muda huu ITV, karibu tuelimishane!
 
Mkuu mjadala uko mubashara muda huu ITV, karibu tuelimishane!

Nafuatilia vizuri sana...

Unfortunately serikali kupitia SSRA ama mfuko wowote wa hifadhi ya jamii wameingia mitini, hawajaonekana kwenye mjadala kujibu hoja...

Hii ni ishara na ushahidi wa wazi kuwa huu ni mpango muovu mahususi uliopangwa na serikali kuumiza wafanyakazi....

Inatisha kweli kama serikali inatafuta mapato ya ku - finance huduma za jamii na miradi ya maendeleo hata mahali ambapo si sustainable....
 
===
Kama kweli hawajamlisha maneno huyo Mama:
Yawezekana na mimi ni kilaza, ebu tutumie hesabu za MAGAZIJUTO kujadili hili.
====
1. Tufikirie amefanya kazi serikali miaka 20 ; mwanzo alikuwa analipwa 400,000/= kwa mwezi ilipofika miaka 10 akapandishwa mshahara mpaka 600,000/- ; baadaya miaka 15 akapandishwa mpaka 800,000/= mpaka anastaafu; .
2.Tufikiria yeye alikuwa anachanga 5% na serikali/mwajiri 15%. Jumla michango 20%;
3.Tufikirie fomula iliyotumika kukokotoa kiinua mgongo ilitumia mshahara wa 600,000/=;
4. Tufikirie kutotambua 'factors' nyingine zaidi ya hii ya makato tu ya pension.
=====
5. Idadi ya miezi ya kuchangia pension ni 20 X 12 = miezi 240
6. Kiasi halisi kilichochangwa na mfanyakazi huyo kwa mwezi kutoka kwenye mshahara wake wa, tuseme 600,000/=, ni (5/100) x 600,000 = 30,000/=
7. Jumla ya kiasi alichochanga kwa miezi 240 ni 30,000 x 240 =7,200,000/=
8. Kwa kutumia namba 5, 6 na namba 7 hapo juu, mwajiri alichangia (tukitumia 15% iliyosemwa namba 2 hapo juu) kiasi cha 21,600,000/=
9 Jumla ya kiinua mgongo chote kwa mstaafu tukitumia namba 7 na 8 hapo juu ni 28,800,000/=
10. Asilimia 25 ya kiinua mgongo chote ni 7,200,000/=.
=====
Hesabu zangu, za kutumia mambo ya wastani na kiwango sawa, zinaniambia, hiyo 25% ni ela ya mstaafu aliyochangia mwenyewe. Ile aliyochangiwa na mwajiri inabaki kwenye mfuko. Hakuna ziada kwenye malipo ya 25% kutoka kwa ela iliyochangwa na serikali/mwajiri.
(ONYO:Hizi hesabu zangu ni kwa minajiri ya kuboresha mjadala hapa jukwaani na zinaweza kuwa na makosa uzitumie kwa uangalifu, mimi kama TUJITEGEMEE wala JF hatutahusika kwa lolote ukizitumia na baadaye zikakuletea matatizo).
====
11. Swali: Mfanyakazi aliyestaafu kwa kulipwa 800,000/= kwa mwezi, je. pensheni yake ya kila mwezi analipwa shilingi ngapi?
12. Tukipata majibu ya swali lilipo namba 11 hapo juu tutajua kiasi alichochangiwa na mwajiri atalipwa chote kwa muda wa miezi mingapi, kabla ya Serikali/mfuko kuanza kumlipa ela za bure mpaka 'umauti' unapomfika kama huyo Mkurugenzi wa SSRA anavyofafanua.
-------------
Yangu ni hayo. Zingatia onyo kwenye post hii.
Huo ni mfano mzuri sana, kingine cha kuongezea ni kwamba huyu mwanachama bado atalipwa pension up to 80% ya 600,000.00 ambayo ni sawa na 480,000.00 kwa mwezi, kwa hiyo atakuwa kama bado yuko kazini.

Cha kuzingatia formula za pension hazizingatii accumulated amount, isipokuwa idadi ya miezi aliyochangia na average salary, nazani itakuwa ya miaka mitano au mitatu kama sikosei.
 
Mkurugenzi mkuu wa SSRA bi Irene amesema mfanyakazi anachangia mifuko ya jamii kwa utaratibu wa 10% na mwajiri 10% au 5% na mwajiri 15% na kwa utaratibu wowote ule mchango wake ni jumla ya 20% ya mshahara wake.

Unapostaafu unalipwa kwa mkupuo 25 % ya mshahara wako je huoni kama tayari una faida ya 5% na bado utaendelea kupokea pension yako ya mwezi hadi ufe?

Irene amewaomba radhi wale wenye matatizo ya lugha kwani wakati ule wa semina elimishi kwa wastaafu alitumia lugha ya kitaalamu zaidi huenda ndio sababu hata Bulaya hakumuelewa.

Chanzo: Clouds 360!
yaani huyu mama nini, au ni THAT TIME OF THE MONTH FOR HER, anafikiri sisi ni wajinga,
 
Kosa tunalofanya watanzania ni kumlaumu huyu mama! Wa kulaumiwa ni JPM na ndiye anayeweza kubadili mambo
 
Mkurugenzi mkuu wa SSRA bi Irene amesema mfanyakazi anachangia mifuko ya jamii kwa utaratibu wa 10% na mwajiri 10% au 5% na mwajiri 15% na kwa utaratibu wowote ule mchango wake ni jumla ya 20% ya mshahara wake.

Unapostaafu unalipwa kwa mkupuo 25 % ya mshahara wako je huoni kama tayari una faida ya 5% na bado utaendelea kupokea pension yako ya mwezi hadi ufe?

Irene amewaomba radhi wale wenye matatizo ya lugha kwani wakati ule wa semina elimishi kwa wastaafu alitumia lugha ya kitaalamu zaidi huenda ndio sababu hata Bulaya hakumuelewa.

Chanzo: Clouds 360!
She has made herself a monster
 
Swala hapa siyo kulipa asilimia 20 au kuongezewa 5 hapa ni mtumishi kulipwa hela yake yote.
Pia Kusema aliongea kitaamu hakuna utaalamu wowote kwenye mafao ya mtu
 
Utaendelea kulipwa pensheni kila mwezi hadi utakapotwaliwa usisahau hilo!
Kumbuka hiyo itawahusu waliofikisha kuanzia miaka 15 kazini. Vipi kama hukufikisha atanufaika vipi?
Usimlazimishe mtu kumchagulia penye faida
Ikiwa mfumo wako ni mzuri wafanyakazi wanaouchagua ni mbovu ya nini kutumia nguvu kuunadi?
Je wewe una nia njema kweli?
 
Wewe fanya siasa mambo ya finance waachie wataalamu, nyie ndomama Mbowe anawapiga ruzuku kwa mikopo feki mnabaki mnashangilia kama mazuzu!.....Yaani Bavicha wote mnashindwa kuelewa tofauti ya mshahara na mchango wa mfuko wa jamii? Umeambiwa malipo ya mkupuo ni 25 ya mishahara yako yote uliyolipwa hadi unastaafu wewe umeng'ang'ana na contribution ya mfuko wa jamii..... Ufipa ni bure kabisa.
Huyo Bulaya ameshaelewa na hoja yake imefia hapo hapo!
Bado nasema kama kuna mashirika nchini yanaendeshwa na viazi kama ninyi ni hasara kubwa kwa Taifa.

Kwanza mi si mwana chadema ni kada pyua.

Pili mahesabu kwangu ndo mchezo wa kila siku.

Tatu mtu kama ninyi kutetea ujinga aliosema huyo mama wa SSRA, ambaye eti ana Phd , ndo unaelewa kuwa malalamiko ya degree zinazopatikana isivyo halali kama alivyodai Dr Viscensia Shule, zina matatizo makubwa katika uchumi wa Taifa.

Usijifiche ati mambo ya finance, hizo ni simple arithmetics.
Kama katika hii mada huelewi basis ya calculations za percentages za 20% ya michango inayokatwa kuwa ni TOFAUTI KABISA na percentage ya 25% ya jumla ya makato kama alivyo fanya huyo mama, basi wote mna degree za vyupi.
 
Back
Top Bottom