Mkurugenzi mkuu SSRA: Kiuhalisia michango yote ya mstaafu ni 20% ya mshahara wake so 25% inampa ziada ya 5%

Acheni akili za kibata, hiyo hela muda wote iliokaa huko ingekua na compound interest ingezaa kiasi gani? Yani mnadhani social security ni linear kiasi hicho kua utasema tu umepata faida ya 5% ?? Kama akili za phd ndio hizi bora kuishia cheti!
Wanajidai hawajui ili hali mkopo wa wanafunzi tu watu wanarudisha na Kariba kadogo.
 
Ndugu Mlenge,

Umeniuliza 25% au 1/4 ni ya kitu gani, si ndiyo eeh?

Nilivyokuelewa = ni ya jumla ya michango ya mstaafu ktk muda wake wote wa utumishi + mchango wa mwajiri kwa kuzingatia kanuni ya kukokotoa mafao hayo.....

Kama nimekosea/sijaelewa, niko tayari kueleweshwa zaidi na zaidi.....
 
Ni ndiyo, ndugu Kitaturu.

Jumla ya michango (ya mtumishi + ya mwajiri) haina uhusika wowote katika kuamua mafao ya mtu aliyechangia kuanzia miaka 15. Mafao ya pensheni ni kama bima ya kumsaidia mtu asiadhirike (fainali) uzeeni. Mafao ya pensheni si kama akaunti ya benki. Mafao yanaangalia vitu viwili tu:

1. Amechangia kwa muda gani? [Idadi ya Michango]
2. Mshahara wake wa mwisho ulikuwaje? [Wastani wa Jumla ya Mishahara ya Mwaka Mzima, (ukiangalia mishahara mikubwa aliyowahi kuipata kwa miaka mitatu, katika kipindi cha miaka kumi ya mwisho kabla kustaafu)].

Lengo ni kumfanya mstaafu apate angalau mshahara angalau unafanana na mshahara wake wa mwisho kila mwezi mpaka atakapofariki.

Ukitaka kupata amani moyoni, chukulia michango unayopelekewa kwenye mifuko ya pensheni ni sawa tu na michango yako unayopelekewa kwenye mfuko wa bima ya afya: ni kama ada ya uanachama na siyo amana kama za kwenye SACCOS au benki.

Mwisho wa mwaka huendi NHIF kusema, mmekata mshahara wangu mwaka mzima, na mimi sijaumwa. Nirudishieni hela zangu! Kwenye mafao ni hivyohivyo. Cha kuzungumzia ni muda wa kuchangia, na ukubwa wa mshahara wako wa mwisho. Na pensheni utakayolipwa kila mwezi. Chukulia malipo ya mkupuo kama "retro-rockets" za kukuwezesha kupata "soft-landing" kuingia kwenye kustaafu.

Je, kipi unapenda:

A. Mafao ya mkupuo makubwa, pensheni ya kila mwezi iwe ni kama utani (nauli ya kwenda kuyachukua toka kijijini kwenda wilayani ni kubwa kuliko mafao)

B. Pensheni ya kila mwezi ni kubwa (si haba, yanakuwezesha kupata rizki ya kila siku), mafao ya mkupuo kama haya?

Kama wewe tayari umeshastaafu, bila shaka jibu lako ni B. Kama bado kustaafu jibu la wengi ni A.

Hapa tunafikia kwenye maamuzi ya kifalsafa:

1. Je, mstaafu apewe hela zake zote, kwa mkupuo, na halafu apambane na hali yake akizitumbua vibaya? Ni mtu mzima mwenye akili timamu. Hela zake, kwa nini mtu aanze kumpangia matumizi? Mpe chake, asepe! Mbele ya safari kelele zote za kusema pensheni ya kila mwezi ni ndogo mno, haiendani na uhalisia, nk. ZIPUUZWE.

2. Je, kujiunga kwenye mifuko ya pensheni kuwe ni hiari au lazima?,

Kwa hiyo, 25% ni ya kwa kile ambacho mfuko unakadiria kuwa ni gharama itakazotumia kumpa hifadhi ya jamii mwanachama wa mfuko. Hiyo 25% siyo ya robo kwa yale mafao ya mkupuo.

Kama ulimsikia mwenzio alipata 100m wakati anastaafu, ina maana bado na wewe utapata hizohizo, kama sifa zenu zinafanana. Kwa vile mifuko mingi ilikuwa inatumia 25% kwa miaka mingi.
 
Huyu bibie asitufanye wajinga wa mahesabu.

20% ya mshahara ni kitu tofauti kabisa na 25% ya makusanyo yote ya makato ya pensheni!

Ajifunze kuwa haongei na wakulima wasiojua kitu.

Mbaya zaidi huyu ama na atueleze ni kwa nini usinirudishie 100% kwa mkupuo mmoja fedha niliyokatwa kwa miaka mingi.
Wewe ndo umeona wakulima siku zote sio waelewa....acha kutoa maneno usiyoyajua!
 
Mkurugenzi mkuu wa SSRA bi Irene amesema mfanyakazi anachangia mifuko ya jamii kwa utaratibu wa 10% na mwajiri 10% au 5% na mwajiri 15% na kwa utaratibu wowote ule mchango wake ni jumla ya 20% ya mshahara wake.

Unapostaafu unalipwa kwa mkupuo 25 % ya mshahara wako je huoni kama tayari una faida ya 5% na bado utaendelea kupokea pension yako ya mwezi hadi ufe?

Irene amewaomba radhi wale wenye matatizo ya lugha kwani wakati ule wa semina elimishi kwa wastaafu alitumia lugha ya kitaalamu zaidi huenda ndio sababu hata Bulaya hakumuelewa.

Chanzo: Clouds 360!
Hivi hadi phd zipo za Picchu?
 
Wewe uwe unaelewa, kama ulichangie sh 50 mil maana yake ni kuwa hiyo ni 20% sasa wewe unalipwa 25% kwa mkupuo sawa na sh 62.5 milioni.
Kama Hisabati hujui hata QM inakushinda mkuu?!
Hesabu anazielewa vizuri sema wewe ndio huku muelewa kwakuwa ulikuwa na jibu lako kichwani.Tatizo hapo nikwanini alipwe hiyo 62.5 na siyo 150.
 
Huyu mama kanichanganya, nasoma koments ndo nachanganyikiwa zaidi.

Kwaniiiiiiii, haya mafao ya Wastaafu ni Stahiki zao au ni Favour? Ninachoamini ni kuwa zile ni Stahiki za wastaafu hawa, sasa kama ni stahiki zao, iweje waje kuwapangia namna ya matumizi? Mtu kamaliza kazi kwa muda uliopangwa apewe chake. Akienda kuzihonga atajua yeye, lile ni jasho lake.

Ama vipi hiyo mifuko iwe hiyari kujiunga. Kila mmoja achague anachoona kuwa sahihi fulu stopu
 
Kwenye finance kuna kanuni ya "Time Value of Money". Kimsingi inachosema kanuni hii ni kuwa pesa inapoteza thamani kadiri muda unavyoongezeka. Hivyo ukitunza pesa bila kuiwekeza baada ya muda thamani yake itapungua. Hivyo pesa aliyochangia mstaafu miaka zaidi ya 20 au 30 iliyopita haiwezi kuwa na thamani sawa na pesa hiyo hivi sasa.
 
Ni ndiyo, ndugu Kitaturu.

Jumla ya michango (ya mtumishi + ya mwajiri) haina uhusika wowote katika kuamua mafao ya mtu aliyechangia kuanzia miaka 15. Mafao ya pensheni ni kama bima ya kumsaidia mtu asiadhirike (fainali) uzeeni. Mafao ya pensheni si kama akaunti ya benki. Mafao yanaangalia vitu viwili tu:

1. Amechangia kwa muda gani? [Idadi ya Michango]
2. Mshahara wake wa mwisho ulikuwaje? [Wastani wa Jumla ya Mishahara ya Mwaka Mzima, (ukiangalia mishahara mikubwa aliyowahi kuipata kwa miaka mitatu, katika kipindi cha miaka kumi ya mwisho kabla kustaafu)].

Lengo ni kumfanya mstaafu apate angalau mshahara angalau unafanana na mshahara wake wa mwisho kila mwezi mpaka atakapofariki.

Ukitaka kupata amani moyoni, chukulia michango unayopelekewa kwenye mifuko ya pensheni ni sawa tu na michango yako unayopelekewa kwenye mfuko wa bima ya afya: ni kama ada ya uanachama na siyo amana kama za kwenye SACCOS au benki.

Mwisho wa mwaka huendi NHIF kusema, mmekata mshahara wangu mwaka mzima, na mimi sijaumwa. Nirudishieni hela zangu! Kwenye mafao ni hivyohivyo. Cha kuzungumzia ni muda wa kuchangia, na ukubwa wa mshahara wako wa mwisho. Na pensheni utakayolipwa kila mwezi. Chukulia malipo ya mkupuo kama "retro-rockets" za kukuwezesha kupata "soft-landing" kuingia kwenye kustaafu.

Je, kipi unapenda:

A. Mafao ya mkupuo makubwa, pensheni ya kila mwezi iwe ni kama utani (nauli ya kwenda kuyachukua toka kijijini kwenda wilayani ni kubwa kuliko mafao)

B. Pensheni ya kila mwezi ni kubwa (si haba, yanakuwezesha kupata rizki ya kila siku), mafao ya mkupuo kama haya?

Kama wewe tayari umeshastaafu, bila shaka jibu lako ni B. Kama bado kustaafu jibu la wengi ni A.

Hapa tunafikia kwenye maamuzi ya kifalsafa:

1. Je, mstaafu apewe hela zake zote, kwa mkupuo, na halafu apambane na hali yake akizitumbua vibaya? Ni mtu mzima mwenye akili timamu. Hela zake, kwa nini mtu aanze kumpangia matumizi? Mpe chake, asepe! Mbele ya safari kelele zote za kusema pensheni ya kila mwezi ni ndogo mno, haiendani na uhalisia, nk. ZIPUUZWE.

2. Je, kujiunga kwenye mifuko ya pensheni kuwe ni hiari au lazima?,

Kwa hiyo, 25% ni ya kwa kile ambacho mfuko unakadiria kuwa ni gharama itakazotumia kumpa hifadhi ya jamii mwanachama wa mfuko. Hiyo 25% siyo ya robo kwa yale mafao ya mkupuo.

Kama ulimsikia mwenzio alipata 100m wakati anastaafu, ina maana bado na wewe utapata hizohizo, kama sifa zenu zinafanana. Kwa vile mifuko mingi ilikuwa inatumia 25% kwa miaka mingi.

Aisee, vizuri Sana.

Sasa hebu tuelimishane kidogo basi.

Kwani kelele hizi zinazopigwa kwa sasa zinatokana na nini hasa?

Ni kipi ambacho kimeleta tofauti kwa sababu nikinukuu maelezo yako hapo juu, ni kwamba hakuna tofauti yoyote ya kiwango walichopata wa kabla ya sheria na kanuni hizi mpya na watakachopata wale watakaostaafu na waliostaafu kuanzia tarh 1/8/2018...

Kama hakuna tofauti what reason makes them cry and complain to that extent? Haelewi, wanahisi tu au kuna nini hasa?

Na kwani kuna ubaya gani kama sheria na kanuni ya zamani ya kukokotolea mafao ya wastaafu ikiendelea kutumika so long as haina malalamiko makubwa kiasi cha hii inavyolalamikiwa?

Na kingine cha mwisho nilichoelewa na kwa kufuatilia mjadala ulivyo na unavyoendelea, ni kuwa kumbe shida ilikuwa kwenye baadhi ya mifuko tu ndiyo kikokotoo chao kilikuwa na shida ....

Sasa kwa malalamiko ya hao na ktk kutaka kurekebisha kasoro hiyo, likely sheria na kanuni hizi mpya (umesema za 2014) zimeleta unafuu kwa Wale wa mifuko ile mingine waliokuwa wanalalamika na kuamusha kilio kwa hii mingine ambayo wanachama wake wala hawakuwa wanalalamika!!

Kwa hiyo tatizo limetatuliwa upande huu, lakini unazua tatizo upande mwingine
 
Huyu mama kanichanganya, nasoma koments ndo nachanganyikiwa zaidi.

Kwaniiiiiiii, haya mafao ya Wastaafu ni Stahiki zao au ni Favour? Ninachoamini ni kuwa zile ni Stahiki za wastaafu hawa, sasa kama ni stahiki zao, iweje waje kuwapangia namna ya matumizi? Mtu kamaliza kazi kwa muda uliopangwa apewe chake. Akienda kuzihonga atajua yeye, lile ni jasho lake.

Ama vipi hiyo mifuko iwe hiyari kujiunga. Kila mmoja achague anachoona kuwa sahihi fulu stopu

Nsanzu,

Uko sahihi sana kuwaza na kufikiri hivyo...

Lakini unasahau jambo moja kuwa, serikali ni dude fulani kubwa ambalo ndani yake lina vyake linavyomiliki....

Kwamba, kiuhalisia "watu" ni miliki ya serikali. Ukimilikwa huna maamuzi. Anayekumiliki ndiye mwenye maamuzi ule nini, uende wapi, ufanye nini na usifanye nini, upate nini na usipate nini....

Umesahau kuwa tunaambiwa kuwa "social security " ni sera na mpango wa ya dunia yote?

Ndo kusema kuwa, hiari haipo na haitakuja kuwepo!!

Na kwa taarifa tu ni kuwa, tunakoelekea itakuwa ni lazima kila mtu kujiunga na hizi schemes na kuchangia vivyo hivyo itakuwa ni lazima...!!

Unaweza ukaniuliza ulazima wa kuchangia utatoka wapi wakati kuna watu watakuwa hawana ajira, hawajaajiriwa popote wala kuwa na shughuli maalumu zao binafsi za kuwaingizia kipato ili wawe na uwezo wa kuchangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii?

Jibu la hoja hii liko wazi mno.

Kwa sababu unaweza ukaulizwa pia kuwa, kwani kuna mtu asiyelipa kodi duniani achilia mbali hapa kwetu Tanzania?

Jibu ni hakuna, hayupo!!

Kama yupo asiyelipa kodi, basi huyo hajawahi kununua hata pipi dukani!!

Nadhani utakuwa umenielewa. Na kama ndiyo, basi ndo kusema michango hiyo inaweza kuingizwa tu kwenye bidhaa Kama kodi ili ukinunua chochote ndiyo unakuwa umechangia hivyo!!

Baadhi ya nchi duniani zinalipa watu wao mafao ya uzeeni na pensheni juu japo hajawahi kuajiriwa popote wala kuchangia direct yeye mwenyewe...

Mfumo unaotumiwa ni kama huo niliojaribu kueleza hapo juu
 
Hivi huyo mwajiri anaweza kumchangia mtu 10%
bila kumfanyia kazi? na kodi yetu tunayokatwa
mbona hatupewi TIN na badala yake inatumika
namba ya mwajiri au na kodi hatukatwi anakatwa mwajiri?
Mmeishaamua kutudhurumu hata msipotoa maelezo
tutalazimika kuwaelewa msipateshida kujikanyaga
na hapa raia wajiandae sana kutoa fedha ya kubrashi viatu
maana hata kile kilichokuwapa matumaini waajiriwa kimeporwa.
 
Nadhani utakuwa umenielewa. Na kama ndiyo, basi ndo kusema michango hiyo inaweza kuingizwa tu kwenye bidhaa Kama kodi ili ukinunua chochote ndiyo unakuwa umechangia hivyo!!
Mkuu kwa mantiki hiyo huoni mfanyakazi
analipa kodi mara mbili? au kuna maduka maalum
ya waliokatwa kodi kwenye mishahara yao ili wasilipie kodi
hizo bidhaa wanazonunua?
 
Kinachonifurahisha ni kwamba hiyo post ya ukurugenzi
ni ya kuteuliwa,soon wote tutaimba wimbo mmoja
pale mteuaji atakapoamua kumteua mwingine.
Ninamkumbuka mheshimiwa fulani
aliyekuwa anasimama kidete kupitisha
sharia kandamizi za habari,baada ya kurudishwa
kwenye kundi la waliowengi ninamuoni
kwenye machapisho mbali mbali akilaani
kilichokuwa kinalaaniwa akiwa mheshimiwa.
muda utaamua nani yupo sahihi na ni nani
ana makosa.Tusubili tu.
 
Naomba kuuliza swali kama huyo mkurugenzi anapitia comments hizi anisaidie.
Hivi kama tunalipwa kwa kufuata kile tulichochanga wenyewe kwenye mifuko hiyo
na si pamajo na tulichochangiwa na mwajiri,je anasemaje juu
ya mfuko wa fidia pindi mfanyakazi anapoumia kazini(WCF)
Huu mfuko mfanya kazi hachangii bali mwajiri peke yake,
inamaana mfanyakazi akiumia kazini halipwi chochote,
kwa madai hayo ya kutochangia chochote?
 
Mimi napendekeza hicho kikokotoo kitumike kwa kada zote, siasa n.k., wabunge, mawaziri na hata wakuu wetu wa nchi ili kupromote umoja wa kitaifa. Hata wabunge walipwe tu 25% ya gratuity zao na Fedha nyingine walipwe kidogokidogo mpaka marupurupu yaishe.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom