Mkurugenzi mkuu SSRA: Kiuhalisia michango yote ya mstaafu ni 20% ya mshahara wake so 25% inampa ziada ya 5%

Wewe uwe unaelewa, kama ulichangie sh 50 mil maana yake ni kuwa hiyo ni 20% sasa wewe unalipwa 25% kwa mkupuo sawa na sh 62.5 milioni.
Kama Hisabati hujui hata QM inakushinda mkuu?!
tatizo wengine ni wanafunzi wanachangia tu hawako bado kwenye ajir
 
Simple! Kama hajui aende bank akakope hata milioni 20 tu kwa miaka 5, baada ya miaka 5 awarudishie bank milioni 20 yao tu, aone kama Majembe hawajatua kuuza Nyumba yake.

Aende HESLB(loan board ya wanafunzi) akawaulize japo hawafanyi biashara kwanini wahitimu hawarudishi pesa ile ile waliyokopeshwa. Wakati serikali haifanyi biashara kwenye elimu kwa watu wake.

Huyu mama nadhani kakamata cheo bahati mbaya au anashinikizo kuu kutoka juu.
 
Bado nasema kama kuna mashirika nchini yanaendeshwa na viazi kama ninyi ni hasara kubwa kwa Taifa.

Kwanza mi si mwana chadema ni kada pyua.

Pili mahesabu kwangu ndo mchezo wa kila siku.

Tatu mtu kama ninyi kutetea ujinga aliosema huyo mama wa SSRA, ambaye eti ana Phd , ndo unaelewa kuwa malalamiko ya degree zinazopatikana isivyo halali kama alivyodai Dr Viscensia Shule, zina matatizo makubwa katika uchumi wa Taifa.

Usijifiche ati mambo ya finance, hizo ni simple arithmetics.
Kama katika hii mada huelewi basis ya calculations za percentages za 20% ya michango inayokatwa kuwa ni TOFAUTI KABISA na percentage ya 25% ya jumla ya makato kama alivyo fanya huyo mama, basi wote mna degree za vyupi.
Achana na huyo kiazi mfiringo, yaan 25% ya malipo ya mkupuko uliyochangia kwa miaka mfano 30 ni sawa na mchango wako wa 20 au 25% ya mchango wako kwa mwezi?? Ivi ni hesabu za wapi hizi, kwanza ingefaa apewe yote 100% na aendelee kupata kiasi fulan kila mwez kutokana na future value ya hyo pesa uliyochangia miaka yote na faida iliyotengeneza kwa mirad iliyoekezwa
 
unajua ni kwa nini wanamuongezea?kwa nini wasiwape watu wasiokuwa na kazi yaani wa mitaani?
Mwenyewe anahisi mchango wa mwajiri ni hisani, anasahau kuwa ile ni makubaliano ya mwajiri na jasho la mwajiriwa.Ingekuwa hisani mwajiri angetoa huo mchango kwa wasiokuwa na ajira.Mifuko isikimbie ukweli.
 
===
Kama kweli hawajamlisha maneno huyo Mama:
Yawezekana na mimi ni kilaza, ebu tutumie hesabu za MAGAZIJUTO kujadili hili.
====
1. Tufikirie amefanya kazi serikali miaka 20 ; mwanzo alikuwa analipwa 400,000/= kwa mwezi ilipofika miaka 10 akapandishwa mshahara mpaka 600,000/- ; baadaya miaka 15 akapandishwa mpaka 800,000/= mpaka anastaafu; .
2.Tufikiria yeye alikuwa anachanga 5% na serikali/mwajiri 15%. Jumla michango 20%;
3.Tufikirie fomula iliyotumika kukokotoa kiinua mgongo ilitumia mshahara wa 600,000/=;
4. Tufikirie kutotambua 'factors' nyingine zaidi ya hii ya makato tu ya pension.
=====
5. Idadi ya miezi ya kuchangia pension ni 20 X 12 = miezi 240
6. Kiasi halisi kilichochangwa na mfanyakazi huyo kwa mwezi kutoka kwenye mshahara wake wa, tuseme 600,000/=, ni (5/100) x 600,000 = 30,000/=
7. Jumla ya kiasi alichochanga kwa miezi 240 ni 30,000 x 240 =7,200,000/=
8. Kwa kutumia namba 5, 6 na namba 7 hapo juu, mwajiri alichangia (tukitumia 15% iliyosemwa namba 2 hapo juu) kiasi cha 21,600,000/=
9 Jumla ya kiinua mgongo chote kwa mstaafu tukitumia namba 7 na 8 hapo juu ni 28,800,000/=
10. Asilimia 25 ya kiinua mgongo chote ni 7,200,000/=.
=====
Hesabu zangu, za kutumia mambo ya wastani na kiwango sawa, zinaniambia, hiyo 25% ni ela ya mstaafu aliyochangia mwenyewe. Ile aliyochangiwa na mwajiri inabaki kwenye mfuko. Hakuna ziada kwenye malipo ya 25% kutoka kwa ela iliyochangwa na serikali/mwajiri.
(ONYO:Hizi hesabu zangu ni kwa minajiri ya kuboresha mjadala hapa jukwaani na zinaweza kuwa na makosa uzitumie kwa uangalifu, mimi kama TUJITEGEMEE wala JF hatutahusika kwa lolote ukizitumia na baadaye zikakuletea matatizo).
====
11. Swali: Mfanyakazi aliyestaafu kwa kulipwa 800,000/= kwa mwezi, je. pensheni yake ya kila mwezi analipwa shilingi ngapi?
12. Tukipata majibu ya swali lilipo namba 11 hapo juu tutajua kiasi alichochangiwa na mwajiri atalipwa chote kwa muda wa miezi mingapi, kabla ya Serikali/mfuko kuanza kumlipa ela za bure mpaka 'umauti' unapomfika kama huyo Mkurugenzi wa SSRA anavyofafanua.
-------------
Yangu ni hayo. Zingatia onyo kwenye post hii.

Hapo 10. pana makosa ya tafsiri. Inaonekana pia dhana ya hifadhi ya jamii haijaeleweka vizuri. Rejea Nataka Pesa Zangu Zote wakati wa kustaafu - JamiiForums


Irudi sheria na kikokotoo cha awali,

Kikokotoo cha sasa hivi kilianza kutumika mwaka 2014. 1:1. Rejea Ukweli Kuhusu Mafao ya PSSSF Sheria Mpya ya Kustaafu - JamiiForums

Huyu mama ni mtaaluma PHD holder wa Econometrics. Nilifuatilia wakati anaongea siku ile alitolea mfano wa kuongeza mke wa pili akimaanisha kwamba maisha ya mwanadamu hayaridhishi wakati wote, kila akipata hiki atataka na kile (rejea Maslow's hierachy of need). Katika mazingira hayo utakuta mstaafu akipata pesa mingi anajikuta mahitaji yake "yanashift upward" na anaweza kujiingiza hata kwenye mahitaji yasiyo ya lazima.

Pili: tunakubaliana kwamba "mtihani mkubwa kwa wastaafu wote huwa ni jinsi ya kutunza ile mafao ili yasiishe haraka, yamsaidie. Katka hili, wastaafu wengi hujikuta wakichekwa au wastaafu wenyewe kwa wenyewe wanachekana kwa kumaliza hela bila kuwa wamefanya jambo lolote la msingi. Mintarafu, ni hekma kubwa kwa serikali kuamua kuwapunguzia "mtihani huu" wazee wetu ili waishi hadi wafe na pesa zao. Wasife masikini.

Nadharia ya ulipaji mafao inakubaliana na wanachosema hawa SSRA kwa niaba ya serikali kwamba; mafao ni haki yake mstaafu akiwa hadi umauti unapomkuta. Mstaafu hawezi kufa akaacha mafao. Anayekufa mwaka wa kwanza amekweda na stahili yake imeishia pale na atakaye kufa na miaka 150 naye atakula pensheni mpaka mwisho wake, wala hatakuwa amekula zaidi. Kwa kifupi, pensheni inakua due pale inapokuwa claimed, pensheni ya mwezi ujao SIO haki ya mstaafu ya mwezi huu, ni mpaka afike mwezi ujao!

QFT. Ukweli Kuhusu Mafao ya PSSSF Sheria Mpya ya Kustaafu - JamiiForums

Hesabu zake bado haziniingii akilini. Labda niulize, alimaanisha mtumishi akistaafu ANALIPWA 25% YA MSHAHARA WAKE AU 25% YA PENSHENI YAKE!!? JE NINI TOFAUTI YA ULIPWAJI MAFAO KABLA YA SHERIA KUPITISHWA NA BAADA YA SHERIA HIYO KUPIGISHWA!!? JE WASTAAFU WA SASA WANAFURAHIA ONGEZEKO HILO LA 5%%
Kanuni ya kikokotozi wa mafao ya wastaafu iliyokuwa inatumika kabla ya hii mpya haikuwa na malalamiko makubwa kama hii....

Labda nikuulize swali moja na kisha na wewe ukipata nafasi ukamuulize Dr General wa SSRA atujibu wafanyakazi...

Kwamba, kwani kikokotozi cha mwanzo kilikuwa na shida gani hata wanatuletea hiki cha kinyonyaji na cha ajabu kabisa?

Formula ni ileile iliyokuwepo toka Julai 2014. Nataka Pesa Zangu Zote wakati wa kustaafu - JamiiForums

jambo hili wakitaka kuondoa malambano ni kutulipa chetu chote tulichochangia pamoja na kilichototolewa na serikali kwani serikali si ndivvyo tulivyojipangi,mbona msiwachangie wasio kuwa na kazi?
Huo ni mfano mzuri sana, kingine cha kuongezea ni kwamba huyu mwanachama bado atalipwa pension up to 80% ya 600,000.00 ambayo ni sawa na 480,000.00 kwa mwezi, kwa hiyo atakuwa kama bado yuko kazini.

Haswaa. Hifadhi ya jamii vs Amana za Benki ni vitu vinavyochanganywa kwenye mjadala. Ukweli Kuhusu Mafao ya PSSSF Sheria Mpya ya Kustaafu - JamiiForums
Nataka Pesa Zangu Zote wakati wa kustaafu - JamiiForums
 
Alaa, kumbe kwako wewe hiki kinachoendelea hata kwenye mjadala huu uliouanzisha kufuatia kauli ya PhD holder wa SSRA mwanamama yule ni kitu gani bwana?

Wanapongeza siyo? Wanagongeana glass za champagne siyo kushangilia kikokotoo dhalimu?

Kwa taarifa yako mimi hapa tunayechat nawe ni mtumishi wa umma tena ktk taasisi nyeti kabisa ya serikali.

I am complaining. I am absolutely against this stupid decision!!
Anasahau wengi walalamikaji Ni wa mifuko wanachama waliokuwa mifuko ya LAPF na PSPF ambao wengi ni waajiriwa wa Serikali.Hii mifuko warudishe kama zamani kwenye hiyo mifuko.
 
Huo ni mfano mzuri sana, kingine cha kuongezea ni kwamba huyu mwanachama bado atalipwa pension up to 80% ya 600,000.00 ambayo ni sawa na 480,000.00 kwa mwezi, kwa hiyo atakuwa kama bado yuko kazini.

Cha kuzingatia formula za pension hazizingatii accumulated amount, isipokuwa idadi ya miezi aliyochangia na average salary, nazani itakuwa ya miaka mitano au mitatu kama sikosei.
Ikumbuke siku nayo mchangiaji atakapo taka itungwe kanuni ya michango ilipwe na riba hapo ndio akili zitawashika hao wanyonyaji.
 
Bado nasema kama kuna mashirika nchini yanaendeshwa na viazi kama ninyi ni hasara kubwa kwa Taifa.

Kwanza mi si mwana chadema ni kada pyua.

Pili mahesabu kwangu ndo mchezo wa kila siku.

Tatu mtu kama ninyi kutetea ujinga aliosema huyo mama wa SSRA, ambaye eti ana Phd , ndo unaelewa kuwa malalamiko ya degree zinazopatikana isivyo halali kama alivyodai Dr Viscensia Shule, zina matatizo makubwa katika uchumi wa Taifa.

Usijifiche ati mambo ya finance, hizo ni simple arithmetics.
Kama katika hii mada huelewi basis ya calculations za percentages za 20% ya michango inayokatwa kuwa ni TOFAUTI KABISA na percentage ya 25% ya jumla ya makato kama alivyo fanya huyo mama, basi wote mna degree za vyupi.
Lakini degree yake ya kyupi inampa mpunga kuliko wako na mkeo mkijumlisha na ma ex wenu wote tangu mvunje ungo or sorry we kidume kumbe!
 
Hapo 10. pana makosa ya tafsiri. Inaonekana pia dhana ya hifadhi ya jamii haijaeleweka vizuri. Rejea Nataka Pesa Zangu Zote wakati wa kustaafu - JamiiForums




Kikokotoo cha sasa hivi kilianza kutumika mwaka 2014. 1:1. Rejea Ukweli Kuhusu Mafao ya PSSSF Sheria Mpya ya Kustaafu - JamiiForums



QFT. Ukweli Kuhusu Mafao ya PSSSF Sheria Mpya ya Kustaafu - JamiiForums




Formula ni ileile iliyokuwepo toka Julai 2014. Nataka Pesa Zangu Zote wakati wa kustaafu - JamiiForums

Mlenge,
Kikwetu "Mlenge", maana yake ni "chumvi".....

Kwetu ni wapi? Ukiniuliza kwa wakati wako na tukiwa wawili tu nitakueleza....

Anyway, lililo muhimu kwa sasa ni mjadala ulio mezani....

Lakini kipekee kabisa, niseme toka ndani ya nafsi yangu kuwa asante sana kwa kunifungua nilipokuwa sielewi.....

Honestly, nimejifunza na kuelewa mengi kuhusu sheria iliyounda mfuko mpya wa PSSSF na kanuni za kuitekeleza sheria yenyewe ambamo ndani yake kipengere cha kikokotoo kimeleta sintofahamu kubwa miongoni mwa wafanyakazi.....

Nakubaliana na wewe kabisa kuwa, kimsingi sheria ni nzuri tu na pengine imeboresha kwa wengi kama ulivyoeleza....

Aidha hata kanuni zenyewe zinazoongoza kuitekeleza sheria kimsingi hazina tatizo kubwa kwa kiwango cha watu wanavyofikiri.....

Tatizo lipo kwenye kipengere kidogo tu cha kanuni ya kukokotoa mafao ya mkupuo mmoja ya mfanyakazi mstaafu huyu....

Aidha nimesoma pia maoni ya chama cha wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu (THIUT).

Wamesema jambo zuri sana kwa kushauri wadau wote wanaohusika kurudi mezani na kuitatua sintofahamu......

Wadau hawa ni wafanyakazi wenyewe (ambao kimsingi ndiyo wadau wakuu ktk hili), mifuko ya hifadhi ya jamii upande mmoja na serikali upande mwingine pamoja na vyama vya wafanyakazi kupitia shirikisho lao (TUCTA).....

Narudia tena kusema, kwa maoni yangu sheria siyo mbaya....

Shida iko kwenye kanuni tena kipengere kidogo tu ambacho kikirekebishwa na elimu kutolewa kwa wafanyakazi, nina hakika hakutakuwa tena na msuguano unaendelea sasa.....

Kiukweli malalamiko ni makubwa sana na yanaweza kuathiri ufanisi wa utendaji kazi ktk maeneo ya kazi......

Na ilifikia watu sasa kufika mbali sana hata kuanza kuhoji mpaka mafao ya wabunge, wakuu wa mikoa, mawaziri, wakurugenzi mbalimbali wa taasisi na mashirika ya umma, waziri mkuu, majaji na mpaka Rais kutoguswa na sheria ama kanuni hii.....

Kwamba kwa nini wao sheria na kanuni hii hawagusi na badala yake iwe kwa wafanyakazi wa kada za chini tu ambao kimsingi ndiyo wazalishaji na watendaji kazi wakuu??
 
Mlenge,
Kikwetu "Mlenge", maana yake ni "chumvi".....

Kwetu ni wapi? Ukiniuliza kwa wakati wako na tukiwa wawili tu nitakueleza....

Anyway, lililo muhimu kwa sasa ni mjadala ulio mezani....

....

Narudia tena kusema, kwa maoni yangu sheria siyo mbaya....

Shida iko kwenye kanuni tena kipengere kidogo tu ambacho kikirekebishwa na elimu kutolewa kwa wafanyakazi, nina hakika hakutakuwa tena na msuguano unaendelea sasa.....

....
QUOTE]

Na miye kikwetu maana ni hiyohiyo "chumvi". Labda kwetu kumoja...

25% ni 1/4 ya kitu gani?
 
Mkurugenzi mkuu wa SSRA bi Irene amesema mfanyakazi anachangia mifuko ya jamii kwa utaratibu wa 10% na mwajiri 10% au 5% na mwajiri 15% na kwa utaratibu wowote ule mchango wake ni jumla ya 20% ya mshahara wake.

Unapostaafu unalipwa kwa mkupuo 25 % ya mshahara wako je huoni kama tayari una faida ya 5% na bado utaendelea kupokea pension yako ya mwezi hadi ufe?

Irene amewaomba radhi wale wenye matatizo ya lugha kwani wakati ule wa semina elimishi kwa wastaafu alitumia lugha ya kitaalamu zaidi huenda ndio sababu hata Bulaya hakumuelewa.

Chanzo: Clouds 360!

Huyu mama ni MCHAWI anayestahili kupigwa mawe mpaka afe..!!
Yeye hawezi kuwa ni MDHIBITI WA MAFAO YA WATUMISHI kwa KUTUNGA KANUNI ZA KINYONYAJI kwa wanapostahafu kana kwamba hiyo fedha inatoka mfukoni mwake.
Hiyo fedha ni fedha ya Watumishi waliyokatwa wakti wote walipokuwa kazini.....!!Hili halikubaliki na litapingwa mpaka siku ya kiyama..!!
 
Mwambie watoe na hiyo 5% ibaki 20% kama ambavyo anadai ndiyo stahiki ya watumishi,nyau kabisa!

Yaani mfano nichangie 20% kila mwezi,tuseme hiyo 20% ni sawa na 150,000/- kwa mwezi, nifikishe jumla ya mil 50 kwa kipindi chote cha utumishi!

Halafu uje unipe 25%, sawa na mil 12.5 ya mil 50 niliyochangia!

Halafu useme hata hiyo umenifanyia hisani wakati ni wizi wa mchana kweupe?Pumbav kabisa!


Nilichelewa kuiona hii thread...nimesikitishwa sana na alichosema huyo mama...mi kwa vile tu nilishaapa kutokumtukana mwanamke maana wanawake wote nawaona kama mama zangu...ningemshushia matusi ya haja...Aisee huyu mama sijui anadhani watu wote hawana akili????au labda ndo ufahamu wake umeishia hapo.
 
Mama Irene umeleweka endelea na kazi......upo vizuri. Tatazo la wa tz....hawajui maana ya akiba ya uzeeni...wnataka ndo wakaanze maisha upya....
 
Acheni akili za kibata, hiyo hela muda wote iliokaa huko ingekua na compound interest ingezaa kiasi gani? Yani mnadhani social security ni linear kiasi hicho kua utasema tu umepata faida ya 5% ?? Kama akili za phd ndio hizi bora kuishia cheti!
 
Back
Top Bottom