Mkurugenzi aponea chupuchupu kuungua moto; gari la mamilioni lateketea

mediaman

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
451
687
Baadhi ya wateja wangu hupenda kuniita Mkurugenzi ingawa sina sifa za kuitwa hivyo. Nafurahia zaidi kuitwa Mkulima. Haya, fuatilia sasa kwa makini ujue mazito niliyokutana nayo safarini. Hii ni habari ya kweli kabisa, ila kama wewe ni mwepesi wa kulia na kutoa machozi, usiendelee kusoma habari hii, tafadhali.

Siku moja nilienda katika jiji moja lililopo kando kando ya Bahari ya Hindi. Nilienda huko kuwatembelea jamaa zangu. Nilifika mchana, jamaa wakanipokea kwa furaha sana baadaye kidogo wakaanza kunitembeza huku na kule kunionesha maendeleo ya vitu na ya watu katika jiji hilo. Kwa ujumla maisha huko ni mazuri. Watu wanaponda raha zao.

Usiku ukafika, jamaa zangu wakaona vema wanitafutie chumba cha kulala katika hoteli moja inayosifika katika jiji hilo. Kabla ya kulala tulikuwa na muda mrefu wa kupashana mambo kadha wa kadha kuhusu maisha. Tuliongea mengi na baadaye nikawaambia jamaa zangu hao kuwa nimepanga kurudi kwetu asubuhi ya siku inayofuata. Hatimaye tukaagana, wakaondoka na mimi nikalala usingizi mwanana.

Kesho yake niliamka mapema sana na kujiandaa na safari ya kurudi kwetu. Kama kawaida yangu kabla ya kusafiri huwa ninamuomba sana Mungu anilinde safarini maana safari zina mengi. Baada ya maombi nikaweka kila kitu vizuri kwenye begi langu tayari kuondoka ili niwahi gari la abiria la kwanza.

Magari ya abiria yanayotoka katika jiji hilo kuja kwetu, yote ni mapya mapya na ya kisasa sana. Yanajulikana kama Toyota Hiace(Luxury). Yanabeba abiria wanane tu kwa wakati mmoja. Na kila abiria anakaa kwenye "siti" nzuri iliyojaa sponji utafikiri ni kiti cha Mkurugenzi wa Shirika fulani kubwa. Kwakuwa abiria ni wanane tu na gari ni pana, hakuna kubanana. Magari hayo yana "Wide Angle TV Screen" kubwa sana. Hivyo wapenzi wa muziki na video wanasafiri kwa furaha sana wakitazama "muvi". Pamoja na TV, magari hayo yanatoa pia huduma ya intaneti(WiFi) bure!

Saa mbili asubuhi nilikuwa bado niko chumbani katika hoteli ile. Niliendelea tu kupumzika kwenye kochi mpaka saa tatu. Baadaye nikaanza kujishangaa na kujiuliza: mbona siondoki hapo hotelini wakati nilikuwa nimepanga niondoke mapema asubuhi, ili niwahi gari la kwanza? Sikupata jibu kwanini nilikuwa nachelewa kuondoka pale hotelini.

Ilipofika kama saa 4 asubuhi ndio nikachukua begi langu na kuondoka pale. Lakini nikasema kabla sijaenda kituo cha magari ngoja kwanza nikawaage wale jamaa zangu, ingawa tulikuwa tumeishaagana jana yake usiku! Duh, Waafrika tunapendana!

Baada ya kuagana nao hatimaye nikaelekea kituo cha magari yale ya abiria -Toyota Hiace(Luxury). Nilipofika tu nikaona gari linaondoka kituoni. Nikajilaumu kwanini nimechelewa kufika kituoni, ningeondoka na gari hilo ili niwahi kurudi kwetu. Majuto ni mjukuu, ikabidi tu nipande gari la pili lililokuwa linafuata kwenye foleni. Abiria hawakuwa wengi hivyo ilichukua muda kupata abiria wanane wa kujaza hiyo Toyota Hiace. Baada ya saa kama moja hivi gari ilijaa, tukaanza kuondoka. Barabara ni ya lami safi, hivyo mwendo ulikuwa wa kasi sana.

Baada ya kusafiri takriban saa moja na nusu, tukaikuta njiani ile Toyota Hiace(Luxury) iliyoondoka kabla yetu. Ooh maskini, ilikuwa inaungua moto mkali sana. Dereva wa Hiace yetu akasimamisha gari, mimi na abiria wenzangu tukashuka na kwenda kuitazama hiyo Hiace iliyokuwa inaungua. Viti vyote vya kifahari vya gari hilo na TV Screen, vilikuwa tayari vimeishateketea kwa moto. Rangi ya gari ilikuwa imeishapotea; utafikiri ni gari la mwaka 47 gereji. Moto ulikuwa mkali sana hivyo hatukuweza kusogea karibu na gari hilo. Matairi ya gari hilo yalikuwa yameanza kushika moto.

Eneo lile halikuwa na nyumba yoyote karibu. Ni pori tu hivyo hapakuwa na mtu yeyote wa kutoa msaada. Kitu cha ajabu sana hatukumuona abiria hata mmoja wa Hiace hiyo wala dereva wake! Hayo magari huwa hayana "konda". Dereva ndio konda. Abiria akitaka kushuka, ni lazima dereva atoke nje aje afungue mlango wa abiria! Hivyo sijui abiria waliokuwemo kwenye Hiace hiyo kama walipona huo moto au la.

Muda huo ndio nikatambua waziwazi kwanini nilikuwa nachelewa chelewa kuondoka hotelini. Kumbe Mungu aliishaiona hiyo ajali, na kwa uweza wake(bila mimi kujua) alinizuia nisiwahi kupanda gari lile.

Yale maombi niliyoomba asubuhi sana baada ya kuamka, Mungu aliyasikia na kuniokoa na ajali hiyo. Vinginevyo nafikiri ule moto ulioiteketeza hiyo Hiace yenye thamani ya mamilioni ya pesa, ungeniteketeza pia na mimi au begi langu, kama ningewahi na kupanda Hiace hiyo. Katika kitabu cha Mwanzo 28:15 Mungu ameahidi kutulinda popote tuendapo. Hata hivyo ni muhimu sana kabla ya kusafiri tumuombe Mungu, katika Jina la Yesu, aitimize ahadi hiyo.

Yesu anatuambia: "Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni..." (Marko 14:38).
 
Ni

Baada ya kuagana nao hatimaye nikaelekea kituo cha magari yale ya abiria -Toyota Hiace(Luxury). Nilipofika tu nikaona gari linaondoka kituoni. Nikajilaumu kwanini nimechelewa kufika kituoni, ningeondoka na gari hilo ili niwahi kurudi kwetu. Majuto ni mjukuu, Ikabidi nipande tu gari la pili lililokuwa linafuata kwenye foleni. Abiria hawakuwa wengi hivyo ilichukua muda kupata abiria wanane wa kujaza hiyo Toyota Hiace. Baada ya saa kama moja hivi gari ilijaa, tukaanza kuondoka. Barabara ni ya lami safi, hivyo mwendo ulikuwa wa kasi sana.

Baada ya kusafiri takriban saa moja na nusu, tukaikuta njiani ile Toyota Hiace(Luxury) iliyoondoka kabla yetu. Ooh maskini, ilikuwa inaungua moto mkali sana. Dereva wa Hiace yetu akasimamisha gari, mimi na abiria wenzangu tukashuka na kwenda kuitazama hiyo Hiace iliyokuwa inaungua. Viti vyote vya kifahari vya gari hilo na TV Screen, vilikuwa tayari vimeishateketea kwa moto. Rangi ya gari ilikuwa imeishapotea; utafikiri ni gari la mwaka 47 gereji. Moto ulikuwa mkali sana hivyo hatukuweza kusogea karibu na gari hilo. Matairi ya gari hilo yalikuwa yameanza kushika moto.

Eneo lile halikuwa na nyumba yoyote karibu. Ni pori tu hivyo hapakuwa na mtu yeyote wa kutoa msaada. Kitu cha ajabu sana hatukumuona abiria hata mmoja wa Hiace hiyo wala dereva wake! Hayo magari huwa hayana "konda". Dereva ndio konda. Abiria akitaka kushuka, ni lazima dereva atoke nje aje afungue mlango wa abiria! Hivyo sijui abiria waliokuwemo kwenye Hiace hiyo kama walipona huo moto au la.

Muda huo ndio nikatambua waziwazi kwanini nilikuwa nachelewa chelewa kuondoka hotelini. Kumbe Mungu aliishaiona hiyo ajali, na kwa uweza wake(bila mimi kujua) alinizuia nisiwahi kupanda gari lile.

Yale maombi niliyoomba asubuhi sana baada ya kuamka, Mungu aliyasikia na kuniokoa na ajali hiyo. Vinginevyo nafikiri ule moto ulioiteketeza hiyo Hiace yenye thamani ya mamilioni ya pesa, ungeniteketeza pia na mimi au begi langu, kama ningewahi na kupanda Hiace hiyo. Katika kitabu cha Mwanzo 28:15 Mungu ameahidi kutulinda popote tuendapo. Hata hivyo ni muhimu sana kabla ya kusafiri tumuombe Mungu, katika Jina la Yesu, aitimize ahadi hiyo.

Yesu anatuambia: "Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni..." (Marko 14:38).
Kweli tunatakiwa kuomba kwa kila jambo ila na wewe kaa ukijua kwamba haikuwa siku yako ya kufa maana hata kama ungeomba ungejikuta tu unasafiri na hiyo gari,lakin pia kama umepangiwa kufa kwa moto utakufa kwa moto tu hata ule uwakao jikoni,kwa hiyo kunusulika kwako sio kwa sabab ya kuomba ila siku yako bado ila tunaomba kwa mungu kusudi hata kama yakitukuta mauti awe tayari ameturidhia kwa sabab mauti yanakuja ghafla.
 
Ungeamka hapohapo na kukianda mbona ungepanda Gari la kwanza kabla ya hilo la mamilioni lililoungua.
 
Baadhi ya wateja wangu hupenda kuniita Mkurugenzi ingawa sina sifa za kuitwa hivyo. Nafurahia zaidi kuitwa Mkulima. Haya, fuatilia sasa kwa makini ujue mazito niliyokutana nayo safarini. Hii ni habari ya kweli kabisa, ila kama wewe ni mwepesi wa kulia na kutoa machozi, usiendelee kusoma habari hii, tafadhali.

Siku moja nilienda katika jiji moja lililopo kando kando ya Bahari ya Hindi. Nilienda huko kuwatembelea jamaa zangu. Nilifika mchana, jamaa wakanipokea kwa furaha sana baadaye kidogo wakaanza kunitembeza huku na kule kunionesha maendeleo ya vitu na ya watu katika jiji hilo. Kwa ujumla maisha huko ni mazuri. Watu wanaponda raha zao.

Usiku ukafika, jamaa zangu wakaona vema wanitafutie chumba cha kulala katika hoteli moja inayosifika katika jiji hilo. Kabla ya kulala tulikuwa na muda mrefu wa kupashana mambo kadha wa kadha kuhusu maisha. Tuliongea mengi na baadaye nikawaambia jamaa zangu hao kuwa nimepanga kurudi kwetu asubuhi ya siku inayofuata. Hatimaye tukaagana, wakaondoka na mimi nikalala usingizi mwanana.

Kesho yake niliamka mapema sana na kujiandaa na safari ya kurudi kwetu. Kama kawaida yangu kabla ya kusafiri huwa ninamuomba sana Mungu anilinde safarini maana safari zina mengi. Baada ya maombi nikaweka kila kitu vizuri kwenye begi langu tayari kuondoka ili niwahi gari la abiria la kwanza.

Magari ya abiria yanayotoka katika jiji hilo kuja kwetu, yote ni mapya mapya na ya kisasa sana. Yanajulikana kama Toyota Hiace(Luxury). Yanabeba abiria wanane tu kwa wakati mmoja. Na kila abiria anakaa kwenye "siti" nzuri iliyojaa sponji utafikiri ni kiti cha Mkurugenzi wa Shirika fulani kubwa. Kwakuwa abiria ni wanane tu na gari ni pana, hakuna kubanana. Magari hayo yana "Wide Angle TV Screen" kubwa sana. Hivyo wapenzi wa muziki na video wanasafiri kwa furaha sana wakitazama "muvi". Pamoja na TV, magari hayo yanatoa pia huduma ya intaneti(WiFi) bure!

Saa mbili asubuhi nilikuwa bado niko chumbani katika hoteli ile. Niliendelea tu kupumzika kwenye kochi mpaka saa tatu. Baadaye nikaanza kujishangaa na kujiuliza: mbona siondoki hapo hotelini wakati nilikuwa nimepanga niondoke mapema asubuhi, ili niwahi gari la kwanza? Sikupata jibu kwanini nilikuwa nachelewa kuondoka pale hotelini.

Ilipofika kama saa 4 asubuhi ndio nikachukua begi langu na kuondoka pale. Lakini nikasema kabla sijaenda kituo cha magari ngoja kwanza nikawaage wale jamaa zangu, ingawa tulikuwa tumeishaagana jana yake usiku! Duh, Waafrika tunapendana!

Baada ya kuagana nao hatimaye nikaelekea kituo cha magari yale ya abiria -Toyota Hiace(Luxury). Nilipofika tu nikaona gari linaondoka kituoni. Nikajilaumu kwanini nimechelewa kufika kituoni, ningeondoka na gari hilo ili niwahi kurudi kwetu. Majuto ni mjukuu, ikabidi tu nipande gari la pili lililokuwa linafuata kwenye foleni. Abiria hawakuwa wengi hivyo ilichukua muda kupata abiria wanane wa kujaza hiyo Toyota Hiace. Baada ya saa kama moja hivi gari ilijaa, tukaanza kuondoka. Barabara ni ya lami safi, hivyo mwendo ulikuwa wa kasi sana.

Baada ya kusafiri takriban saa moja na nusu, tukaikuta njiani ile Toyota Hiace(Luxury) iliyoondoka kabla yetu. Ooh maskini, ilikuwa inaungua moto mkali sana. Dereva wa Hiace yetu akasimamisha gari, mimi na abiria wenzangu tukashuka na kwenda kuitazama hiyo Hiace iliyokuwa inaungua. Viti vyote vya kifahari vya gari hilo na TV Screen, vilikuwa tayari vimeishateketea kwa moto. Rangi ya gari ilikuwa imeishapotea; utafikiri ni gari la mwaka 47 gereji. Moto ulikuwa mkali sana hivyo hatukuweza kusogea karibu na gari hilo. Matairi ya gari hilo yalikuwa yameanza kushika moto.

Eneo lile halikuwa na nyumba yoyote karibu. Ni pori tu hivyo hapakuwa na mtu yeyote wa kutoa msaada. Kitu cha ajabu sana hatukumuona abiria hata mmoja wa Hiace hiyo wala dereva wake! Hayo magari huwa hayana "konda". Dereva ndio konda. Abiria akitaka kushuka, ni lazima dereva atoke nje aje afungue mlango wa abiria! Hivyo sijui abiria waliokuwemo kwenye Hiace hiyo kama walipona huo moto au la.

Muda huo ndio nikatambua waziwazi kwanini nilikuwa nachelewa chelewa kuondoka hotelini. Kumbe Mungu aliishaiona hiyo ajali, na kwa uweza wake(bila mimi kujua) alinizuia nisiwahi kupanda gari lile.

Yale maombi niliyoomba asubuhi sana baada ya kuamka, Mungu aliyasikia na kuniokoa na ajali hiyo. Vinginevyo nafikiri ule moto ulioiteketeza hiyo Hiace yenye thamani ya mamilioni ya pesa, ungeniteketeza pia na mimi au begi langu, kama ningewahi na kupanda Hiace hiyo. Katika kitabu cha Mwanzo 28:15 Mungu ameahidi kutulinda popote tuendapo. Hata hivyo ni muhimu sana kabla ya kusafiri tumuombe Mungu, katika Jina la Yesu, aitimize ahadi hiyo.

Yesu anatuambia: "Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni..." (Marko 14:38).
Imeisha au itaendelea.
 
Siku yako ilikuwa haijafika...hata hao waliopona au la kuna walioomba kabla ya hiyo safari....Dah inaonekana uliisikitika sana hiyo gari kuungua na kuteketea kuliko roho za hao abiria........
 
Nimefarijika tu hapo mwishoni hukutuwekea namba yako ya simu ili tukuchangie sadaka!
 
Mimi sipendi pesa, Mkuu.
Soma: 1 Timotheo 6:6-10
[6]Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.
[7]Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu;
[8]ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo.
[9]Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.
[10]Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
 
Huyu ni yule Mwamba aliyekanyagwa na Tembo? vilevile nahisi ndio huyu pia Alikutana na Majambazi zaidi ya kumi usiku?
Mmmmmmh Nikavute zangu Bangi mie
 
Kwani Wakulugenzi wenyewe Og..

Wanasemaje ...juu ya hii habari:
 
Back
Top Bottom