Mkulo hili lako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkulo hili lako

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by nard, Dec 24, 2011.

 1. n

  nard Member

  #1
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 15
  Ndugu zangu watanzania mara nyingi nimekuwa nikifuatilia habari za uchumi wa nchi yetu kwa karibu sana. Mengi nimeyasikia, nimeyasoma na mengine yanajithibitisha yenyewe! Kwa mfano mwezi Mei mwaka huu mh. Zitto alisema serikali imefilisika na haina fedha ya kutekeleza mambo mengine muhimu yaliyo kwenye bajeti waziri wa fedha akakanusha habari hizo. Nimethibitisha mwenyewe kwani ajira na madai ya walimu ni sehemu mojawapo ya mambo ambayo hayajatekelezeka! Tofauti na mawaziri na viongozi wengine wanaohusika kusema uongo kwa watanzania kuwa ajira "mwezi ujao" malipo ya madai "mwezi ujao " na mwezi unapofika msemaji anaingia mitini! Hivi sasa najiuliza mh Mkulo anasubiri mpaka Zitto au wanasiasa wengine wasimame jukwaani na kusema SERIKALI IMEFILISIKA ndiyo yeye akanushe au athibitishe? kwa nini asituambie hali halisi ya nchi? kuna haja gani ya yeye kuwa waziri kama anashindwa kutekeleza majukumu yake? Lakini kwa kukaa kwake kimya nimeamini "serikali imefilisika" na yeye anaona haya kusema ukweli kwani alishakana mwanzoni.
   
 2. A

  Arkad Member

  #2
  Dec 24, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  wananchi hawawezi ku-handle ukweli..hivyo njia rahisi ni kudanganywa..wananchi wakiambiwa ukweli patakuwa hapatoshi . Watu wanapenda ahadi ndicho serikali inachofanya..Kuna vitu vingine wanakwambia hupaswi kujua kw amani yako..wanasema wanaku ''protect''.
   
 3. M

  Malila JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kwa sasa kabakiwa na njia hiyo basi.
   
 4. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Mkulo ni msanii na muongo; hastahili kuwa waziri wa fedha kwenye serikali yeyote makini!
   
Loading...