Mkulo anatuongopea?

Achaneni na Mkulo huyo. Anatumiwa tu kama vibaraka wengine!

Mishahara wanalipa kwa kubangaiza. Mwezi wa kwanza mwaka huu katika Wilaya niliyoko walileta mshahara ukiwa na nakisi ya Shs.28 Mil!!! Halmashauri ikabidi ijazie kutoka deposite!! Bajeti za mwaka ujao za DADPs zimekatwa kwa asilimia 50%!!! Kipengele cha ugani wamekata kabisa!!! (Kilimo kwanza oyee!!!). Halafu anasema Serikali ina hela za kutosha!!!!

Mr. Mkulo tell it to the mountains!!!!

Taabu ya watu kama akina Mkulo na mawaziri wengi tu wanafikiri matumizi na mapato ya serikali ni siri za serikali!
 
Alichokisema Mh. Zitto kina ukweli kwanza yeye ni waziri kivuli wa fedha na uchumi,lkn kama kweli serikali haijafilisika kwa nn mishahara kwenye tasisi za ummma ilipwe tar 34 ya mwezi, nikimaanisha tarehe 3?

Serikali imefulia kweli, Zitto akijibu, Mkulo ataumbuka hana lolote Mkulo.
 
Hivi huyu waziri si ndio mlisema elimu yake duni?


anyway nadhani anatekeleza maagizo ya mkuu kwamba waongee wasikae kimya
 
Selikari yetu hiyo jamani, mie hata sipotezi muda kukokotoa hayo mahesabu yao.
1. Kwanza Rais mwenyewe hajui idadi kamili ya wafanyakazi wake(mtakumbuka sakata la Mgaya) sasa atajuaje hiyo mishahara, kwahiyo Mkulo kaweka namba tu mchezo uishe.
2. Uongo ukirudiwarudiwa mara nyingi huwa Ukweli Raisi kasema hayo jana kwenye semina Elekezi

akhaaaaaaaa....mie hata siendelei nasikia hasira tu!
 
Budget ya 2010-2011 inaonyesha kuwa recurrent expenditure ambayo inainclude mishahara ni bn 7790, sawa na asilimia 67% ya budget yote ya serekali ya trilioni 11610 tzs. Makusanyo ya ndani ni bn 6003 tzs. Katika recurrent expenditure kuna mambo mengi sana, lakini mishahara inaweza kuwa ni moja ya sehemu nene nene. Sikuweza kupata mchanganuo wa mishahara ya wafanyakazi katika bajeti hiyo ni asilimia ngapi-- kama kuna mwenye nayo aiweke hapa tuichambue. Kama serekali inakusanya wastani wa bilioni 450 kwa mwezi, kwa mwaka itakusanya 5400bn, sawa na tofauti ya bn 603 pungufu ya budget ya makusanyo ya ndani

Mkulo kwa unafiki mkubwa ameshidwa kutaja ziada/nakisi ya mapato na matumizi baada ya kuchojoa mishahara. Ina maana ukishalipa mishahara kinachobaki ni ziada na ni akiba, je kuhusu usafiri, hospitali, ruzuku za vyama vya siasa, safari za JK, vitafunwa vya ofisi, mafuta ya magari ya serekali, viongozi wastaafu etc. Ukishalipa vyote hivyo ziada au pungufu ni kiasi gani-- hilo ndilo alitakiwa asema na hakusema na ndio hapo Zito anapokuwa shujaa kwani ndipo haswa alipopasema

Ni kweli serekali inaweza kuwa na uwezo wa kulipa mishahara kufuatia makusanyo yake, kama mishahara ingekuwa first priority, but je ni kipi kinaanza kulipwa, kama vitafunwa vya wakubwa vinaanza kulipwa kabla ya mshahara wa kalumakenge, ni wazi kuwa kinachobaki baada ya kuondoa matumizi hayo ya wakubwa ni kidogo kuweza kuwalipa kina kalumakenge kima cha chini.

Ninachotaka kusema hapa ni kuwa kuna pengo la mapato na matumizi, matumizi ni makubwa kuliko mapato, na Mkulo hilo hakulionyesha, yeye kaonyesha tu matumizi ya serekali kwa upande wa mishahara, hakusema mengine. So ukishatoa hayo mengine, kinachobaki ni kidogo kuweza kulipa wafanyakazi- ukizingatia kuwa mishahara iko ranked low kwenye order ya matumizi ya serekali na ndio maana serekali inakopa. Zito is absolutely right, Mkulo umezidi kuiumbua serekali ya JK

Na hawa waandishi wa habari uchwara wasioweza kuuliza maswali ya kiuchmabuzi zaidi wananiudhi kama nini
 
Jamani hawa watu wanajikaanga kwa mafuta yao wenyewe. Sasa wanatuonyesha kwamba zaidi ya 50% ya makusanyo ya selikali ni kulipa mishahara, hapo bado uendeshaji mwingine wa selikali kama posho, mafuta, stationary etc etc, hii ina maana kwamba hela tunayokusanya haiwezi kabisa kuendesha selikali sasa miradi ya maendeleo inaghalimiwa vipi jamani?

Mi nadhani hawa jamaa wangekaa kimya tu kuliko kujivua nguo hadharani kila kukicha, haiwezekani 50% tulipie mishahara tu halafu tutengemee kama kwenye situation hiyo maendeleo yatapatikana tutangoja sana ila hapa maendeleo hakuna.

NB: Zitto na wengine wenye majukwaa ya kuzungumza, please keep on the pressure mpaka waone nchi chungu hii tumechoka watu wanaiba madini yetu kila siku sisi tunakusanya peanuts ambayo yote inachukuliwa na matumizi ya selikali
 
Hao ni wababaishaji,mimi ninaushahidi kwani mishahara hailipwi kwa wakati,ina maana mpka wachakachue kwanza,na yupo ndugu yangu ambaye anafundisha chuo cha ualimu huu ni mwezi wa tatu hajalipwa,huyo Mkulo aacha blaa blaa
 
Nyambala nimerudia hizo hesabu na kujiuliza:

Mwezi Disemba mishahara 243.80 bilioni
Mwezi Januari mishahara
240 bilioni (punguzo la bilioni 3)
Mwezi Machi Mishahara
249 bilioni (ongezeko la bilioni 9)
Mwezi Aprili Mishahara
246.70 (punguzo la bilioni 3 hivi)

Najiuliza kulikuwa na tatizo gani la Ajira huko serikalini? wanaajiri sana au wanatimuana sana? Au mishahara inabadilika mara kwa mara? au hii inajumlisha na posho zote n.k? Vyovyote vile ilivyo sijui kama hesabu hizi zinaakisi ajira halisi iliyopo serikalini.

Mzee Mwanakijiji heshima yako. Kuhusiana na hilo hata mie naweza kukusaidia mkuu kutoka na trend zilivyo . Kwa kawaida kwenye mwisho wa kila quarter yaani Machi, June, September na Desemba wafanyakazi wengi hulipwa sana malimbiko ya posho zao yale yanayotokana na mishahara. Na hili hufanyika kwa sababu katika kila mwisho wa hizi quarters ndipo vile vile mapato huwa mengi kwani watu wengi na makampuni mengi hulipa zile provisional tax return. Na anapo sema mishahara ina include vitu vingi mkuu, basic salaries, overtime, house allowance nk
 
Hao ni wababaishaji,mimi ninaushahidi kwani mishahara hailipwi kwa wakati,ina maana mpka wachakachue kwanza,na yupo ndugu yangu ambaye anafundisha chuo cha ualimu huu ni mwezi wa tatu hajalipwa,huyo Mkulo aacha blaa blaa

Huyo ndugu yako lazima atakuwa na matatizo
 
Jamani hawa watu wanajikaanga kwa mafuta yao wenyewe. Sasa wanatuonyesha kwamba zaidi ya 50% ya makusanyo ya selikali ni kulipa mishahara, hapo bado uendeshaji mwingine wa selikali kama posho, mafuta, stationary etc etc, hii ina maana kwamba hela tunayokusanya haiwezi kabisa kuendesha selikali sasa miradi ya maendeleo inaghalimiwa vipi jamani?

Mi nadhani hawa jamaa wangekaa kimya tu kuliko kujivua nguo hadharani kila kukicha, haiwezekani 50% tulipie mishahara tu halafu tutengemee kama kwenye situation hiyo maendeleo yatapatikana tutangoja sana ila hapa maendeleo hakuna.

NB: Zitto na wengine wenye majukwaa ya kuzungumza, please keep on the pressure mpaka waone nchi chungu hii tumechoka watu wanaiba madini yetu kila siku sisi tunakusanya peanuts ambayo yote inachukuliwa na matumizi ya selikali

Mkuu soma bajeti 2010/2011 utayajua hayo yote. Kwani serikali iliisha sema itakopa kwa ajili ya pesa za maendeleo (development expenditures) na hilo ndilo wanalo fanya
 
Hawa watawala wanatufanyia masihara! Kwani hawajui kuwa hawa akina zitto nao ni wafanyakazi wa serikali kisiasa?kuwa nao wanapata mshahara?iweje akae aongee utumbo? Na apa ameharibu kabisa kwa kuwa wafanyakazi walitegemea apology badala ya siasa upupu! Mkullo kama mtaalam wa fedha angeweza kupata sababu nyingine za kiuchumi zinazoridhisha watu badala ya kuleta upuuzi. Acheni majibu ya kitoto viongozi,hatutaki majibu kama ya TRA walivomjibu dr Slaa,ni ujinga,ni ujinga ni ujinga.
 
Serikali imefulia ukweli,hawawezi kulipa mishahara tarehe 34 ya mwezi ndio useme ina akiba wakati hazina kila siku wanawarudisha watu na kuwaambia fedha hakuna,nn kimebaki halafu mkulo asimtishe mh.zitto kwa sababu ni bora wahisani wakapata taarifa serikali ya chama cha magamba imefulia,ili wasitishe hiyo misaada kwa sababu inanufaisha magamba kutoka chama cha magamba.
 
Tukubali kwamba mishahara haijalipwa. Hali sio hiyo kwa watumishi wa serikali. Magari yao ya mikopo na ya wizi yako barabarani. Maisha yanakwenda kama kawaida kwenye familia zao. Wakubwa wao watakuwa St. Gasper kwa siku nne mfululizo. Wabunge na kamati zao wanaendelea kama kawaida. Ruzuku za vyama zinalipwa ndio maana CHADEMA wako huko waliko. Mambo yote haya yanakwenda kwa ndoto na miujiza kama ile ya Samunge?
 
Hahahahahahahahaha, naanza kwa kicheko kwa sababu, kuna waalimu wapya ambao mpaka sasa wanpewa mishahara nusu, huu sio uongo wa Mkullo? Na Vipi kuhusu mishahara wa watumishi waliopanda vyeo katika taasisi mablimbali za serikali? Mbona mishahara hiyo mipya haijatoka tangu July 2010 walipopanda vyeo? Je, wanataka kutuambia kuwa hiyo ziada, ambayo kwa mujibu wa mkullo, ipo tu inasubiri shughuli haifai kulipa hayo malimbikizo na mishahara mipya ya hao watumishi?

Bado napata shida kuelewa utetezi wa Mkullo, lakini shida zaidi inakuja pale aliposema tusieneze uongo dhidi ya serikali kwani tunaweza kukosa missada kutoka kwa wafadhili. JK fanya reshuffle, mawaziri wako hawawezi kuisemea serikali na wankuangusha mno.
 
Nyambala nimerudia hizo hesabu na kujiuliza:

Mwezi Disemba mishahara 243.80 bilioni
Mwezi Januari mishahara
240 bilioni (punguzo la bilioni 3)
Mwezi Machi Mishahara
249 bilioni (ongezeko la bilioni 9)
Mwezi Aprili Mishahara
246.70 (punguzo la bilioni 3 hivi)

Najiuliza kulikuwa na tatizo gani la Ajira huko serikalini? wanaajiri sana au wanatimuana sana? Au mishahara inabadilika mara kwa mara? au hii inajumlisha na posho zote n.k? Vyovyote vile ilivyo sijui kama hesabu hizi zinaakisi ajira halisi iliyopo serikalini.

Sasa hapa inakuaje?:A S cry:
 
Kwa kauli ya Mkulo, ni kwamba hamna vipaumbele vingine serikalini baada ya makusanyo isipokuwa mishahara tu. Je, hapo tutegemee maendeleo? Shule zetu za kujifunza SIPIYU kinadharia zitauona mwanga wa ukweli wa elimu? Je, siku mapato yakishuka chini ya 250bn itakuwaje? nchi itaenda? (Bado madeni lukuki ya serikali, DOWANS, IPTL, Kesi mbalimbali za madai dhidi ya serikali, kupunguza deni la taifa, n.k.) Sina hamu na Mkuu-Loo!!
 
Sisi tumesema sana basi tuyaache ili Mungu ayashughulikie maana yanajua kujitetea hayo,yetu macho na masikio
 
Mkuu soma bajeti 2010/2011 utayajua hayo yote. Kwani serikali iliisha sema itakopa kwa ajili ya pesa za maendeleo (development expenditures) na hilo ndilo wanalo fanya

kaka na wewe unakubaliana nao kwamba hela ya maendeleo tukaombe misaada,hela ya kuendesha selikali ndo tujitafutie wenyewe wakati kuna watu wanachimba madini na kuiba rasilimali nyingine sie tunaomba hela kwao kwajili ya maendelo
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom