Mkulo anatuongopea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkulo anatuongopea?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyambala, May 10, 2011.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkulo: Serikali haijafilisika

  na Mwandishi wetu, Dodoma
  Source: Hapa

  WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, amesema serikali haijafilisika na haijawahi kukopa fedha kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi wake.

  Mkulo alisema hayo mjini Dodoma jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari akijibu tuhuma za Naibu Katibu Mkuu wa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kabwe Zitto, aliyesema kuwa serikali imefilisika kiasi cha kukopa kwenye mabenki ya ndani kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi wake na wabunge.

  "Napenda kutumia fursa hii kukanusha vikali madai hayo kuwa ni uongo mtupu na upotishaji unaofanywa kwa maksudi kwa lengo la kujitafutia umaarufu wa kisiasa… napenda kuwaeleza wananchi kuwa taarifa hizo si sahihi. Serikali inalipa watumishi wake mishahara kwa kutumia mapato yake ya ndani pia ina uwezo wa kugharamia shughuli zake nyingine ikiwemo kuendesha Bunge," alisema Mkulo.

  Alisema mishahara ya watumishi wa serikali katika kipindi cha kuanzia Desemba hadi Aprili mwaka huu, makusanyo na mapato ya ndani ni malipo ya mishahara ya watumishi wa serikali.

  Akifafanua hilo Mkulo alieleza kwamba Desemba mwaka jana serikali ilikusanya sh bilioni 594 ambapo kiasi cha sh bilioni 243.80 kilitumika kulipa mishahara na ziada ya sh bilioni 350.20 ilipatikana wakati Januari mwaka huu makusanyo yalikuwa sh bilioni 433.50 na mishahara iliyolipwa ni sh bilioni 240 huku ziada ya sh bilioni 193 ikiendelea kuwepo.

  Mkulo aliendelea kufafanua kuwa Februari mwaka huu walikusanya sh bilioni 430 na ikalipa mishahara sh bilioni 266 na ikabaki na ziada ya sh bilioni 163.70 huku Machi serikali ikikusanya sh bilioni 567 na ikalipa mishahara sh bilioni 249 na kubaki na ziada ya sh bil. 317 wakati Aprili walikusanya sh bilioni 432 na ikalipa mishahara sh bilioni 246.70 na kubaki na ziada ya sh bilioni 185.40.

  "Uchambuzi huu unaonyesha dhahiri kuwa serikali inayo mapato ya kutosha ambayo yanakidhi kulipa mishahara ya watumishi wa serikali kwa ukamilifu na tunayo ziada ya kutosha kugharamia shughuli nyingine za serikali… kwa kawaida serikali inatumia fedha taslimu kulipa gharama zake.

  "…Kwa hiyo mapato ya Desemba yanalipa mishahara na matumizi ya Januari. Mapato ya Januari yanalipa matumizi ya Februari na kadhalika, kwa utaratibu huu hakuna hata mwezi mmoja ambao wafanyakazi wa serikali wamekosa mshahara.

  "Wanaotoa uongo huo wanatafuta umaarufu wa kisiasa, wamekosa uzalendo kwa taifa lao," alisisitiza Mkulo na kuongeza kwamba posho mbalimbali za wabunge zimelipwa kwa wakati licha ya ongezeko la wawakilishi hao na kutaja stahili zao kuwa ni kwa ajili ya shughuli za kamati za Bunge, posho majimboni, mishahara na mafuta ya kila mwezi.

  Aliongeza kuwa mwezi uliopita mishahara ya wabunge ilitolewa Aprili 22 mwaka huu na fedha kwa ajili ya posho mbalimbali nazo zimeshatolewa kwenye ofisi za Bunge. Hivyo alisisitiza na kuelewesha umma kuwa serikali haijashindwa kulipa mishahara ya wabunge na posho zao tofauti na taarifa zilizotolewa na Zitto akidai wabunge hawajalipwa.

  Akizungumzia mikopo ya serikali na malengo yake, Mkulo alisema pamoja na kutumia mapato ya ndani kugharamia shughuli zake, hukopa kutoka vyanzo mbalimbali ili kugharamia shughuli za maendeleo. Mikopo hiyo inahusisha ile yenye masharti nafuu na kibiashara.

  "Kwa mfano katika mwaka wa fedha wa 2010/2011 serikali ilipanga kukopa kiasi cha dola za Marekani milioni 525 ambapo kati hizo dola za Marekani 250 zitagharamia miuondombinu wakati kiasi cha dola za Marekani milioni 175 zitatumika kununua mitambo ya kufua umeme wenye uwezo wa kuzalisha megawati 100 kwa ajili ya Dar es Salaam na megawati 60 kwa ajili ya Mwanza," alisema.

  Mkulo alisema ameamua kutoa ufafanuzi huo ili kuonyesha kwa kifupi kuwa serikali ina uwezo wa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake, mishahara na gharama zote za kuendesha Bunge kutokana na mapato yake ya ndani. Sio kweli na ni upotoshaji wa makusudi wenye malengo ya kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

  Alipoulizwa hatua gani atachukuliwa Zitto kutokana na kutoa taarifa za uongo kwa Watanzania, alijibu kuwa yeye alichofanya ni kueleza kile ambacho ndicho sahihi kwa serikali na kwamba wanaoweza kumchukulia hatua Zitto kwa kusema uongo ni Bunge lenyewe. Kutokana na ufafanuzi huo, Mkulo alisema kuwa kikubwa kinachotakiwa hata kama ni mtu wa chama chochote cha kisiasa ama kiongozi kuchuja mambo na kuangalia athari zake kwa kina na si kukurupuka kwa kutafuta umaarufu ambao hauna tija kwa taifa zaidi ya kusababisha matatizo.  My Take:

  1. Mkulo anataka kutuaminisha kwamba kazi ya mapato ya serikali ni kulipa mishahara basi. Sasa sijui hata hivyo vikao vya bajeti wanakaa kwa ajili ya nini.

  2. Kwa takwimu za mkulo ina maana mpaka sasa serikali ina ziada ya shillingi bilioni elfu moja mia mbili na nane au Shillingi Trilioni 1 na bilioni mbili

  3. Inakuwaje sasa serikali yenye ziada ya mihela yote hiyo halafu inaenda kukopa tena?

  4. Hivi huu si uwendawazimu? Februari mwaka huu walikusanya sh bilioni 430 na ikalipa mishahara sh bilioni 266 na ikabaki na ziada ya sh bilioni 163.70 . Mishahara tu ni 62%, hiyo serikali iakuwaje na hela?

  5. Kwa mapato hayo na matumizi hayo kwa mishahara tu, si ni indicator ya wazi kabisa kwamba tuna liserikali likuubwa tena lisilo na manufaa yeyote.

  6. Hiyo trend ya matumizi hainekani kabisa kwamba jamaa wanajali kubana matumizi wao ni kutumia tu!

  7. Kama hizi data nni za kweli, basi Mkulo, JK and the government are failing us miserably.

  8. Bunge linaingiajae hapa kumchukulia hatua Zitto kama amesema uwongo?
   
 2. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkulo na serikari ya jk wanahaha!
  Zitto ametufumbua macho.
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani ukisoma btn the lines hayo maelezo yake ni kwamba hali ni mbaya kuliko hata alivyoielezea Zitto!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 10, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Nyambala nimerudia hizo hesabu na kujiuliza:

  Mwezi Disemba mishahara 243.80 bilioni
  Mwezi Januari mishahara
  240 bilioni (punguzo la bilioni 3)
  Mwezi Machi Mishahara
  249 bilioni (ongezeko la bilioni 9)
  Mwezi Aprili Mishahara
  246.70 (punguzo la bilioni 3 hivi)

  Najiuliza kulikuwa na tatizo gani la Ajira huko serikalini? wanaajiri sana au wanatimuana sana? Au mishahara inabadilika mara kwa mara? au hii inajumlisha na posho zote n.k? Vyovyote vile ilivyo sijui kama hesabu hizi zinaakisi ajira halisi iliyopo serikalini.
   
 5. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,988
  Likes Received: 20,391
  Trophy Points: 280
  Binafsi naamini kukopa si jambo baya na hasa kama serikali inakopa kwa minajili ya shughuli za maendeleo, tatizo linakuja unakopa wapi na kwa ajili ya nn, serikali inapoamua kukopa katika mabenki ya ndani inazuia watz kukopa katika mabenk haya, Mkapa na mabaya yake tutamkumbuka kama kiongozi aliyeondoa mtindo wa serikali kukopa ndani na aliwalipa wazabuni waliokuwa wakiidai serikali lakini kina Mkullo na JMK wamekuwa ni mabingwa wa kukopa benk za ndani na leo anakuja na data zinazoonesha serikali ina ziada kubwa ya fedha lol.

  Anachofanya Mkulo ni kudanganya umma ili waonekane kuwa kuna kitu wanafanya kumbe ni watu wasiojaribu kuvipa kazi vichwa vyao:bange:
   
 6. f

  fisi 2 JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 524
  Trophy Points: 280
  Tatizo la mawaziri wa Tanzania ni wanadhani wamepewa nafasi hizo ili tu WAKANUSHE madai ya kweli yanayoletwa dihidi ya serikali.

  Zitto amesema ukweli mimi ni mfanyakazi wa serikali nina madai ya muda mrefu wiki iliyopita nimefuatilia nikaambiwa na mwajiri kuwa sasa hivi hakuna pesa kabisa LABDA HADI Mwezi wa 9 baada ya bajeti. Wale wote waliopata promotion kuanzia mwezi februari hawajalipwa stahili zao hata mmoja.

  MKULLO ANAONYESHA JINSI GANI ALIVYO MJINGA KUKANUSHA TUUU.
   
 7. B

  Bobby JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  I guess you are right Nyambala, hali yetu inawezekana ikawa mbaya zaidi. Kwanini anaonesha as if matumizi pekee ya serikali ni mishahara?

  Eti kila akitoa mishahara balance ni ziada wakati kila mtu anajuwa hii ni serikali ya per diems, washa, semina elekezi, makongamano na posho zingine?

  Leave alone safari za ndani na nje za rais, makamu, first ladies, mawaziri na wakuu wengine na kila mmoja serikalini. Kwa mfano juzi ndugu zetu wa EWURA walizurura almost dunia nzima kwenye first class na posho USD lukuki kwa kila mmoja actually kama USD 500 per person per day.Lakini pia kama mna hali nzuri kihivyo kwanini mlipe mishahara tarehe 40?.

  Mzee Mkullo unao ujasiri wa kwenda mbele zaidi na kutueleza matumizi yote ya serikali versus mapato? Afichaye ugonjwa kifo kitamfichua, ninyi endeleeni na hii tabia then muingize hii nchi shimoni. Kwanini kila siku mnazungumzia kuongeza makusanyo ya kodi pasipokukemea matumizi mabaya ya hizo kodi?
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Unapokuta makusanyo ya kodi ni kwa ajili ya mishahara tu, jua huko mbele lazima tutakwama! Kama ni uchumi basi huku ni kudesa onto bila kuwa uwezo kujua unachokidesa!
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Eeeeh,rafiki zangu wawil wananiambia kua hadi sasa wanadai misahara ya miez miwili,hawajalipwa nao ni watumishi wa serikalini
   
 10. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,686
  Likes Received: 21,949
  Trophy Points: 280
  Zitto haya yanayosemwa na wanajamvi yachukue na kuyafanyia kazi kwa kuitisha press conference au jukwaani kuyaeleza ili Serikali na Mkulo waumbuke mbele ya Watanzania
   
 11. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Huu ni muda muafaka wa kuhangaika na sekta binafsi. Msiogope eti security ya kazi
   
 12. K

  Kishalu JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 850
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Kwa maelezo inaonekana ni pamoja na posho zote maana hiyo tofauti ni kubwa sana na inabidi kumshukuru sana Zitto kutufumbua haya maana wengine tusingejua
   
 13. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Kwa wastani hapa ni kuwa kila mwezi serikali hutumia 244.875bn kwa mishahara....ikiwa tufanye wastani wa mishahara kwa kada zote ni 1,000,000 ina maana serikali ina watumishi 244,875?
   
 14. B

  Bobby JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Ni kweli Raia tell them. Halafu hii kitu ya security mm nadhani iko overrated, security gani ya malipo kidogo na yasiyolipwa kwa wakati? Huu ni uongo mtupu hakuna securityyeyote hapo tena kwa aina ya viongozi hawa tulionao ndio kabisa.
   
 15. MANI

  MANI Platinum Member

  #15
  May 10, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,413
  Likes Received: 1,873
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo ndio pagumu maana hakuna figure halisi ya mshahara pengine ni yale maruhani(mishahara kwa watumishi hewa) huwa yanakuwepo mwezi huu na mwingine hayapo.
   
 16. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #16
  May 10, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,209
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na wengi kuwa alichosema Zitto ni ukweli mtupu tena usiotiliwa shaka. Kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu mimi kama mtumishi wa serikali ninayo madai yangu tangu nilipoajiriwa. Kila nikidai naambiwa hali ni mbaya labda mpaka bajeti ijayo. Hii ni sawa na serikali kuanza matumizi ya bajeti ijayo kabla ya wakati.

  To me there are two options: Kumwamini Mkulo ikiwa nimelipwa au kumwamini Zitto kwa kuwa sijalipwa na mwajiri wangu amethibitisha hilo, so Zitto amesema ukweli mtupu
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  May 10, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  hivi mshahara ni deni la wafanyakazi kwa serikali (mwajiri wao) au ni haki yao? Wafanyakazi wakianza kudai kwa nguvu serikali inaweza kuwazuia wasidai haki hiyo au inawakopa nguvu kazi yao?
   
 18. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #18
  May 10, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tatizo ninaloliona mimi ni kwamba jana kikwete amewaagiza wawe wanajibu mapigo. sasa wao bila kujipanga wanakurupuka na matokeo yake ndio haya. Mh. Zito ni mbunge na ni ushahidi tosha kwamba hawajalipwa posho kwa sababu serikali ina ukata. angekuwa amelipwa posho asingesema hayo. Je Mh. zito akiamua kuanika mengine kuhusu ukata wa serikali sijui Mkulo atajibuje!!!!!
   
 19. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #19
  May 10, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,172
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280
  Ningekuwa mimi ndio CAG ningeanzia hapa ku audit (Kukagua) Mishahara ya watumishi wa Umma. Haiwezeka kuna kupanda na kushuka kwa ajabu namna hii. Kuna ufisadi mkubwa hapa.

  Halafu Mkulo anataka kutuambia kipaombele kwa serikali ni kulipa mishahara tu wakishamaliza basi inayobaki ni akiba? Nachoweza kusema hapa kwa staili hii ya Mkulo tutegemee maumivu siku si nyingi usoni
   
 20. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #20
  May 10, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Watumishi wako around 500,000 kama ulifuatilia hotuba ya Raisi alipoongea na wazee wa DSM wakati anajibu madai ya Vyama vya Wafanyakazi
   
Loading...