Mkulo anatuongopea?

Mkulo anatuongopea?

Jamani tukubaliane kuwa Waziri kama waziri hawezi kuja na hoja ya kuipinga ama kuididimiza serikali aliyomo ndani yake.

Yawezekana kweli kuna tatizo ila hawataki kuweka wazi wakihofia mwonekano hasi kutoka kwa jamii na Taifa kwa ujumla

kutokana na hesabu niliziona hapo kwa mtoa mada juu ya makusanhyo,kunatatizo kubwa la matumizi ya fedha na kama lisipo angaliwa kimakini chochote cha weza tokea mbele ya safari
 
Yawezekana watumishi wa serikali wanafariki kila mwezi na wengine wanaajiliwa vilevile!

Nyambala nimerudia hizo hesabu na kujiuliza:

Mwezi Disemba mishahara 243.80 bilioni
Mwezi Januari mishahara
240 bilioni (punguzo la bilioni 3)
Mwezi Machi Mishahara
249 bilioni (ongezeko la bilioni 9)
Mwezi Aprili Mishahara
246.70 (punguzo la bilioni 3 hivi)

Najiuliza kulikuwa na tatizo gani la Ajira huko serikalini? wanaajiri sana au wanatimuana sana? Au mishahara inabadilika mara kwa mara? au hii inajumlisha na posho zote n.k? Vyovyote vile ilivyo sijui kama hesabu hizi zinaakisi ajira halisi iliyopo serikalini.
 
Je hayo makombo ya vijisenti yanafaa kitu kwenye miradi maelfu ya maendeleo? je gharama za uendeshaji serikali? Anyway, tatizo sio mkulo na umbumbu wake... Hata kikwete mwenyewe anatudharau watz,sembuse huyo mtoa povu mdomoni? imekula kwetu watz,kama hatuwezi kuingia mtaani basi tuwe wapole hadi 2015
 
Yeye uzalendo anautoa wapi. Raia wa Malawi ajifanye anaipenda Tanzania inawezekana vipi, au ndo amepatia pa kusema ili naye aonekane kwenye macho ya watu kuwa anaipenda nchi hii. Huyu jamaa nakumbuka alishawahi kuwatukana matusi ya nguoni waandishi wa Times fm wakati wanamuhoji. Atueleze ile kesi iliishia wapi kama yeye ana uzalendo.
 
one of the most incompetent minister we have in this cabinent
 
Unapokuta makusanyo ya kodi ni kwa ajili ya mishahara tu, jua huko mbele lazima tutakwama! Kama ni uchumi basi huku ni kudesa onto bila kuwa uwezo kujua unachokidesa!

You said it all mkuu. Inabidi uwe na ujasiri sana kuthubutu kusimama mbele ya wananchi na kuwaambia kuwa kodi yenu tunaitumia kujilipa mishahara na posho. Hakuna shughuli za maendeleo?
 
Kama mishahara tu inakula zaidi ya asilimia hamsini tuna tatizo katika ukusanyaji mapato aua katika utumiaji...
 
Kwa wastani hapa ni kuwa kila mwezi serikali hutumia 244.875bn kwa mishahara....ikiwa tufanye wastani wa mishahara kwa kada zote ni 1,000,000 ina maana serikali ina watumishi 244,875?

Gd analysis, mkuu kama ulkikuwepo ndani ya kichwa changu!
 
Mheshimiwa zitto inabidi uitishe press conference kujibu madai aliyoyatoa kuwa ulichokizungumza hakina ukweli na unastahili kuzomewa which is stupid thing kwa waziri mzima kupendekeza kitu kama hicho licha ya yote mheshimiwa inabidi ujibu hoja kwa kuwa umeshamweka mkulo on defensive mode pale ambapo naamini ndipo ungelipenda awepo.
 
Watumishi wako around 500,000 kama ulifuatilia hotuba ya Raisi alipoongea na wazee wa DSM wakati anajibu madai ya Vyama vya Wafanyakazi

Anywayz mkuu tunaweza pia kwenda na hiyo namba, assume kuna wafanyakazi 10,000 wanaopata hiyo av. ya mil. nne. Total hapo ni bilion 40.

Hao wanaobaki ukichukua hiyo bil. 200 ukagawa kwa 490,000 unapata 408,000 kila mtu way far from 135,000 wanayolipa kima cha chini na ambao watakuwa kama 80% ya wafanyakazi wote wa serikali. Kifupi ni kwamba hela nyingi kati ya hiyo itakuwa inaenda kwenye posho, na ni kakikundi labda 5% ndiyo wanafaidi. Tukirudi nyuma unakuta madai ya kina Mgaya yalikuwa sahihi kabisa!
 
Achaneni na Mkulo huyo. Anatumiwa tu kama vibaraka wengine!

Mishahara wanalipa kwa kubangaiza. Mwezi wa kwanza mwaka huu katika Wilaya niliyoko walileta mshahara ukiwa na nakisi ya Shs.28 Mil!!! Halmashauri ikabidi ijazie kutoka deposite!! Bajeti za mwaka ujao za DADPs zimekatwa kwa asilimia 50%!!! Kipengele cha ugani wamekata kabisa!!! (Kilimo kwanza oyee!!!). Halafu anasema Serikali ina hela za kutosha!!!!

Mr. Mkulo tell it to the mountains!!!!
 
Hata mimi ningeweza kumsaidia Zitto kwenye hilo. Kuna thread niliwahi kuweka hapa ya kuipongeza benki ya NMB kama miezi 3 iliyopita watu hawakuilewa vizuri. Serikali yetu ina OD facility ikae kimya tu itaumbuka.
 
atajibiwa tu....... kwani mkulo naye si mmoja wa wanamagamba!!!!!!!!!! hawana lolote.
 
Topic zingine Bana..hata hujui vipi tuzijadili.... Hadithi za muuza kahawa hizi.
 
Nyambala nimerudia hizo hesabu na kujiuliza:

Mwezi Disemba mishahara 243.80 bilioni
Mwezi Januari mishahara
240 bilioni (punguzo la bilioni 3)
Mwezi Machi Mishahara
249 bilioni (ongezeko la bilioni 9)
Mwezi Aprili Mishahara
246.70 (punguzo la bilioni 3 hivi)

Najiuliza kulikuwa na tatizo gani la Ajira huko serikalini? wanaajiri sana au wanatimuana sana? Au mishahara inabadilika mara kwa mara? au hii inajumlisha na posho zote n.k? Vyovyote vile ilivyo sijui kama hesabu hizi zinaakisi ajira halisi iliyopo serikalini.

Kwa nnavyoijua Tanzania unaweza kukuta si JK wala Mkulo wala Katibu wa wizara na hata kamishna wamewahi kushangaa kuhusu hili. Uthibitisho ni pale Mkulo anapotoa maelezo yenye discrepancies za namna hii na wala hazitolei maelezo. In another way siyo issue!
 
Mkulo angesema pia mbona serikali haijalipa annual increments na mishahara huwa inachelewa sana?
 
Wakuu ni kwa vile niko mobile ninge weka link ya thread yangu nilianzishaga ya kuipongeza banki ya NMB hapa 3 months ago.
 
Back
Top Bottom