Mkubwa na Wanawe - Ya Moto

Mkubwa na Wanawe - Ya Moto

Video zao zitendewe haki.Hii ni kwa sababu aina za nyimbo wanazoimba zinahitaji uchezaji mahiri hasa.Wako poa kabisa!
 
nilikuwa nauliza kama wimbo huu unafaa kwa akina sie na yale mambo yetu yalee, ama?
 
Hii ngoma naipenda sana kwa kweli. Hao madogo wana vipaji haswa.

Dogo Aslay kaiua hiyo aya ya kwanza.

Beka naye kaitendea haki kabisa hiyo aya ya pili.

Maromboso naye kafanya kweli.

Halafu hako kabinti kalikovaa spandex na kikaptula cha jeans juu yake nimetokea kukapenda. Yaani kanavyonengua..aaah.

Yaani wimbo umetulia kuanzia mashairi, mpangilio wa ala, hadi dance routine.

Kisura wangu ingawa haelewi wanachoimba lakini anaipenda sana hiyo choreography.



Kukupenda, imekuwa kero
Kutwa kucha kunitenda, mi mwana wa mwenzio

Nachofanya mi sikioni, ila masikio yanasikia wee
Nachofanya mi sikioni, ila masikio yanasikia wee

Kupenda na kupenda kweli, ah sikatai
Uwepo wako ni mzuri, maishani nafurahi
Kupenda na kupenda kweli, ah sikatai
Uwepo wako ni mzuri, maishani nafurahi

Ila ya moto, ya moto mapenzi
Mapenzi ya kitoto, ya kitoto mie siwezi
Ila ya moto, ya moto mapenzi
Mapenzi ya kitoto, ya kitoto mie siwezi


Karibu mwaka sasa umepita tokea nibandike hilo bandiko.

Nafurahi kuona nilikuwa sahihi.

Changamoto iliyopo sasa kwa hao vijana ni kuweza kuendelea kama kundi manake mara nyingi makundi ya hivi huwa yanaishia kusambaratika tu.

Licha ya hivyo, muda utatueleza.

Nadhani baada ya kutoka Uingereza safari ijayo itakuwa Marekani.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom