Mkono wangu umekosa nguvu - Msaada

BinAd

JF-Expert Member
Sep 2, 2016
214
115
Mimi ni mtu mzima over 50, kwa miezi miwili sasa mkono wangu wa kulia hauna nguvu yaani huwa nashindwa hata kupeleka chakula mdomoni mpaka niusaidie.

Inakuwa tabu hata kuvaa shati au fulana, pia hata kupokea au kutoa kitu kwa kutumia huu mkono inakuwa taabu sana (haunyooki vizuri).

Naweza kuutumia kwa kunyanyua kitu chochote kizito kama ndoo ya maji na kuipeleka sehemu nyingine. Nasikia viungo vya bega kama vinama/kuchoka? (not pain).

Nimekwenda Hospital na kupiga x-ray mara mbili tofauti ninaonekana niko safi. hii x-ray ya pili dr aliniambia kuwa inaweza kuwa gout.

Najua huu ugonjwa unaweza kuwa umewapata nanyi/jamii yenu. Naomba msaada kutoka kwenu.
 
Pole sana
Nashukuru kwa maoni na ushauri wenu, wakati bado nasubiri maoni na ushauri Zaidi naomba kuongezea kidogo kuhusu afya yangu.
Mimi bado najiona ki akili na kufikiri niko sawa kabisa na naendelea kufanya kazi (ajira) yangu kama kawaida. Hali yangu wanaoifahamu ni wale niliowaambia tu. Sio rahisi kuona tofauti ya mikono yangu mpaka pale ninapotaka kuutumia mkono huu Zaidi kama nilivyoeleza hapo awali. Natumia mikono yote miwili kufanya kazi za ofisini kama vile kuandika na kusaini (mkono wa kulia), kutumia key board n.k.
Kuhusu hospital, naomba kwenu wadau kama mnamfaham daktari mjuzi wa magonjwa haya mnifahamishe.
 
Nenda hospital kubwa tatizo lako linahitaji matibabu ya kina wala sio blabla...Dalili za gout huanza kunekana au ishara, ni maumivu ya miguu due to gravitation Influence maana chumvi au urates hutengeneza deposits kwenye miguu, na vidole gumba vya miguu huvimba na kuwa red.Narudia tena nenda hospital unahitaji matibabu ya kina si blabla.ila pole sana ndugu
 
Mimi ni mtu mzima over 50, kwa miezi miwili sasa mkono wangu wa kulia hauna nguvu yaani huwa nashindwa hata kupeleka chakula mdomoni mpaka niusaidie. Inakuwa tabu hata kuvaa shati au fulana, pia hata kupokea au kutoa kitu kwa kutumia huu mkono inakuwa taabu sana (haunyooki vizuri). Naweza kuutumia kwa kunyanyua kitu chochote kizito kama ndoo ya maji na kuipeleka sehemu nyingine. Nasikia viungo vya bega kama vinama/kuchoka? (not pain).
Nimekwenda Hospital na kupiga x-ray mara mbili tofauti ninaonekana niko safi. hii x-ray ya pili dr aliniambia kuwa inaweza kuwa gout!
Najua huu ugonjwa unaweza kuwa umewapata nanyi/jamii yenu. Naomba msaada kutoka kwenu.
kama ni gauti nasikiaga kutafuna zile mbegu za mlonge zinasaidia sijui hali hiyo inatokea kukiwa na baridi sana au hali.ya kawaida tu
 
Minor stroke labda. Jitahidi na mazoezi ufuate na ushauri wa daktari. Pole.
 
Pole sana mkuu,endelea kujitahidi kutafuta wataalamu wa afya ili waweze kukusaidia katika hilo tatizo pia jitahidi kumshirikisha Mungu katika hili kulingana na imani yako ili kama ni nguvu za giza zishinde kabisa.
 
Back
Top Bottom