Msaada: Nasumbuliwa na tatizo la moyo

Boeing787-8

JF-Expert Member
Aug 16, 2018
798
843
Hope mko poa. Miaka ya nyuma Kama 10yrs ago wakati wa utoto, nilipenda sana kucheza Mpira, nilipokuwa nakimbia Sana nilikuwa nasikia Kama Kuna kitu kinabana kwenye moyo afu kinaacha Basi nikawa nachukulia poa, kwa kua haikunizuia kufanya kazi zangu za kila siku.

Miaka ilienda nkawa Kama muda mwingine napumbua kwa shida yaani hewa inabana na kuachia, mie nilichukulia poa kwa kua haikuwa serious, nilikuwa nadhani labda Nina nyama kwenye pua maana na mother yangu pua take zilikuwa zinabana.

Lakini siku moja moja nilikuwa na experience Kama mapigo ya nguvu ya moyo, mie nachukulia poa, nilikuwa nachukulia poa kwa sababu nilikuwa siumwi chochote, afu nilikuwa busy na kusoma hizo miaka.

Mwaka 2020 mwishoni nilikuwa nafanya mapenzi na demu wangu nkaisi Kama naishiwa pumzi, Basi nili notes kuwa ntakuwa na shida kwenye moyo, nkajipanga kutafuta hela niende hospital kubwa

Mwezi wa pili 2021 kabla sijaenda hospital nilipata mapigo ya moyo yanayoenda mbio kinyama, moyo ulikuwa unadunda Kama utachomoka, Basi moyo ukaanza kuuma yaani nilishituka hatari, Basi nkatafuta hela nkaenda hospital kwa specialist wa moyo.

Nilipima vipimo viwili, electrocardiogram na echocadiogram. Majibu yalikuwa hivi

Valves zote ziko vizuri, Ejection fraction Ni 86% wakati kwa normal heart Ni 75%, Diastolic disyfunctional grade one(I) afu nilikutwa na hypertrophic cardiomyopathy.

Doctor Ali conclude kuwa moyo wangu umetanuka, especially left ventricle (LH) nilikuwa Sina nguvu ata, ATA kunyanyua kikombe nilikuwa siwezi, moyo wangu ulikuwa unauma Sana, nilikuwa naisi kizunguzungu hatari, nilikuwa na difficult I breathing. Na kifua kubana nkitembea haraka au kunyanyua kitu ATA ndoo.

Nilianza dozii ya vidonge vya losartan na lasix. Nilipangwa kuuzulia kriniki kila baada ya wiki mbili, afu Sina bima Sina kazi. Nilimeza vidonge kwa 5months, nkaacha kwenda clinic maana ukienda unapewa vidonge hivyo hivyo na kupimwa pressure.

Badae Kuna watu washawai kupatwa na moyo kutanuka, wakanishauri nitumie na dawa za kienyeji.baada ya mwaka wa kutumia dawa za kienyeji na za hospital ( baada ya 5 months niliacha dawa za hospital nkaanza za kienyeji) haya ndo matokeo.

  • Difficult in breathing imeisha napumua vizuri
  • Nguvu ninazo natembea, sio Kama zamani sema siwezi kukimbia maana moyo utauma
  • Moyo kuuma imeisha, labda nikimbie au kubeba vitu vzito
  • Moyo kwenda mbio imeacha

Matatizo mapya
- yaani siwezi kufanya physical exercise, nkikimbia kidogo moyo utaenda mbie na ku feel uncomfortable

- kufanya mapenzi labda goli moja, sijawa stable

- Tatizo kubwaaaa Ni mkono wa kushoto na bega la kushoto, yaani mkono wa kushoto nkiufanyisha kazi utasababisha niumwe na kifua, na moyo kwenda mbio hatari, upande wa mgongo chini ya bega la kushoto ukifanya kazi kidogo au kubeba vitu vizito, au kufanya mapenzi kwa muda utasikia maumivu uko mgongoni upande wa kushoto.

Kutopona kunanifanya nakuwa na depression hatari mawazo kama yote, na pressure kupanda Mara kwa Mara,

Hapa nilipo Sina amani Wala furaha na maisha,dawa nilizozitumia zimewaponyesha watu wengi ninao wafahamu sahivi wanaendelea na life, Mimi sijui Ni ugonjwa gani huu, mwaka mzima siponi, sijui nimerogwa au Nini, wenzangu niliowakuta hospital kwa tatizo la moyo kutanuka washapona, sio wanyonge Kama Mimi, yaani nkitembea haraka shida, kukimbia shida, kunyanyua kitu kizito shida, ku sex shida khaaa.

Msaada wakuu,
 
Umeshapata Kazi?

Hayo Mawazo ndio yanapelekea usipone Moyo uzidi kuuma.

Endelea na Dawa za Kienyeji na Kisunna, acha kujifikiria kua wewe ni Mgonjwa, ondoa hayo mawazo kabisa na ujione uko sawa ila ni changamoto ndogo ndogo. Achana na Mafuta na punguza kiwango cha Chumvi,

Mazoezi fanya ila yasiwe mazito, jipumzishe kwa muda kwenye kufanya mapenzi hadi utakapo pona hayo mawazo uliyokua nayo.

Badili Hospital ukapime upya.
 
Umeshapata Kazi??
Hayo Mawazo ndio yanapelekea usipone Moyo uzidi kuuma,

Endelea na Dawa za Kienyeji na Kisunna, acha kujifikiria kua wewe ni Mgonjwa, ondoa hayo mawazo kabisa na ujione uko sawa ila ni changamoto ndogo ndogo,
Achana na Mafuta na punguza kiwango cha Chumvi,

Mazoezi fanya ila yasiwe mazito, jipumzishe kwa muda kwenye kufanya mapenzi hadi utakapo pona hayo mawazo uliyokua nayo,

Badili Hospital ukapime upya.
Wewe mdada mbona Kama umepiga mulemule, yaani Nina msongo mkubwa namaanisha mkubwa wa mawazo mpaka sometimes pressure inapanda, kazi sijapata ndo nasubiria Tamisemi wafungue Dirisha niombe, uchumi mbaya, kwenda hospital bila bima Ni shida, naomba Sana mungu nipate ajira ya ualimu (Tamisemi) ili nipate bima.

Mazoezi labda nifanye ya kutembea haya mengine bado...Ila umenifungua macho
 
Kuwa serious boss siweza kusema hapa hilo tatizo tafuta tiba mbadala ila tumezika mwezi wa kwanza bro wangu mtoto wa mjomba.
 
Wewe mdada mbona Kama umepiga mulemule, yaani Nina msongo mkubwa namaanisha mkubwa wa mawazo mpaka sometimes pressure inapanda, kazi sijapata ndo nasubiria Tamisemi wafungue Dirisha niombe, uchumi mbaya, kwenda hospital bila bima Ni shida, naomba Sana mungu nipate ajira ya ualimu (Tamisemi) ili nipate bima.

Mazoezi labda nifanye ya kutembea haya mengine bado...Ila umenifungua macho
Mchawi wako ni hayo mawazo, kumbuka Mawazo na Masononeko hutanua Moyo,, ukipata kazi ukawa busy hutasikia Moyo wala Figo kila kitu mwilini kitakua poa utakua mwenye furaha na amani,

Wakati wasubiri hizo ajira tafuta taasisi yoyote ukajitolee, kujitolea kuna fungua sana rizki kuliko kukaa tu kusubiri ajira ikufate nyumbani.
 
Mchawi wako ni hayo mawazo, kumbuka Mawazo na Masononeko hutanua Moyo,, ukipata kazi ukawa busy hutasikia Moyo wala Figo kila kitu mwilini kitakua poa utakua mwenye furaha na amani,

Wakati wasubiri hizo ajira tafuta taasisi yoyote ukajitolee, kujitolea kuna fungua sana rizki kuliko kukaa tu kusubiri ajira ikufate nyumbani.
Shukrani dada angu
 
Back
Top Bottom